Tangu Magufuli aingie madarakani ni mambo mawili tu ninayompongeza

Kwanza niseme tu wazi kwamba Magufuli sikumpigia kura na wala sitakuja nimpigie kura hata hiyo 2020. Japokuwa nilijua atashinda na ninajua pia hata 2020 atashinda na safari hii nahisi atashinda kwa kishindo.

Ila kiukweli pamoja sikumpa kura yangu kuna mambo mawili tu nampongeza tangu aingie madarakani. Kuna vingi kafanya ,mfano kanunua ndege,kabana matumizi,kazuia safari za nje kwa wateule wake,kajenga airport huko Chato,mapato TRA yameongezeka,kazuia mianya ya rushwa na wizi.

Kaleta mahakama ya mafisadi japo haina wafungwa,kaondoa wanafunzi na wafanyakazi hewa,,aisee ni mengi kafanya. Ila mimi hayo yote hayanihusu maana sio mwajiriwa wa mtu wala wa serikali na sifikilii kuajiliwa.kwa hiyo hayo hayanihusu kabisa. Mimi alichonifurahisha ni

1: Kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa,kwa kweli nampa hongera raisi,kwa sababu hii mikutano inaleta uongo na kudumaza akili za watanzania,ni mikutano hiihii ilisema Lowassa ni mwizi na fisadi papa,na ni mikutano hiihii ikaja kusema Lowasa sio mwizi bali ni mwanamabadiliko. Kwa hiyo kitendo cha rais kuzuia hii mikutano ni cha kupongezwa na kila mweye akili timamu. Hii mikutano haikuwa na tija bali ni kupoteza muda tu na kusemasema wau

2: Kuzuia bunge live kwa kweli amecheza kama pele. maana ilifikia hatua wabunge wanatafuta umaarufu tu bungeni ila majimboni kwao hawana cha maana. Sasa safari hii wakae wafanye maedeleo majimboni, yale mambo ya kupata ubunge kwa sababu tu ya umaarufu wako hayapo tena. Maana kuna watu ni wabunge tu ila wanajulikana Tanzania nzima ova ni mbunge wa taifa. Sasa safari hii ubunge wataupata kutokana na maedeleo wanayoleta majimboni na sio kwa umaarufu tu. Na natamani rais asilegeze kamba,ashikilie hapohapo.
HUU NI UFINYU MKUBWA SANA WA MAWAZO, wamarekani wote wangekua na mawazo ya Trump Dunia ingekwisha
 
Mkuu mambo ambayo umempongeza mh rais ndiyo mambo ya msingi ambayo mi binafsi sikubaliani nayo. 1.Tunahitaji shughuli za kisiasa ziendelee, juu ya kile kitakachosemwa wananchi wataamua wenyewe. Maana kusema,kusikilizwa,kushauri,kukosoa na kupongeza ni haki ya kila mtanzania. Suala lakufanya siasa halina msimu ndio maana serikali inatoa ruzuku kwa vyama kila mwezi.2.Suala la bunge kuonyeshwa "live" ni haki yetu. Ni moja ya njia ya kujua uwajibikaji wa wabunge tuliowachagua.kwa kifupi shughuli za kisiasa zinaisadia kuongeza uwajibikaji serikalini
Hata hili la ruzuku ni shida, litazamwe upya. Ikiwezekana ifutwe, vyama vijiendeshe vyenyewe. Ruzuku inaweza ikawa ni kibinyo cha hiyo demokrasia yao lakini pia mamluki wangekwisha kwenye huu mchezo mchafu.
 
Kwanza niseme tu wazi kwamba Magufuli sikumpigia kura na wala sitakuja nimpigie kura hata hiyo 2020. Japokuwa nilijua atashinda na ninajua pia hata 2020 atashinda na safari hii nahisi atashinda kwa kishindo.

Ila kiukweli pamoja sikumpa kura yangu kuna mambo mawili tu nampongeza tangu aingie madarakani. Kuna vingi kafanya ,mfano kanunua ndege,kabana matumizi,kazuia safari za nje kwa wateule wake,kajenga airport huko Chato,mapato TRA yameongezeka,kazuia mianya ya rushwa na wizi.

Kaleta mahakama ya mafisadi japo haina wafungwa,kaondoa wanafunzi na wafanyakazi hewa,,aisee ni mengi kafanya. Ila mimi hayo yote hayanihusu maana sio mwajiriwa wa mtu wala wa serikali na sifikilii kuajiliwa.kwa hiyo hayo hayanihusu kabisa. Mimi alichonifurahisha ni

1: Kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa,kwa kweli nampa hongera raisi,kwa sababu hii mikutano inaleta uongo na kudumaza akili za watanzania,ni mikutano hiihii ilisema Lowassa ni mwizi na fisadi papa,na ni mikutano hiihii ikaja kusema Lowasa sio mwizi bali ni mwanamabadiliko. Kwa hiyo kitendo cha rais kuzuia hii mikutano ni cha kupongezwa na kila mweye akili timamu. Hii mikutano haikuwa na tija bali ni kupoteza muda tu na kusemasema wau

2: Kuzuia bunge live kwa kweli amecheza kama pele. maana ilifikia hatua wabunge wanatafuta umaarufu tu bungeni ila majimboni kwao hawana cha maana. Sasa safari hii wakae wafanye maedeleo majimboni, yale mambo ya kupata ubunge kwa sababu tu ya umaarufu wako hayapo tena. Maana kuna watu ni wabunge tu ila wanajulikana Tanzania nzima ova ni mbunge wa taifa. Sasa safari hii ubunge wataupata kutokana na maedeleo wanayoleta majimboni na sio kwa umaarufu tu. Na natamani rais asilegeze kamba,ashikilie hapohapo.
Pumbavu : nadhani utakuwa hujui pia km hii nchi ni ya kidemikrasia
 
Wakati unajirusha na boom tena ukiandamana eti ndogo hukujua kama ni mkopo utakaokuja kukatwa hapo mbele?
Shida sio kukatwa we dogo...shida ni kutoka 8% mpaka 15% bila mpangilio... mbona nimekatwa for the last 7 years sijawahisema ni tatizo? Whatz wrong witchu
 
Wenye akili zao watakujua tu wewe ni CCM,
2020 alazma ashinde kwa kishndo,
Unapongeza no bunge live,
Unapongeza no harakati za kisiasa
Umeonyesha uwezo wako wakufkr
 
Hata hili la ruzuku ni shida, litazamwe upya. Ikiwezekana ifutwe, vyama vijiendeshe vyenyewe. Ruzuku inaweza ikawa ni kibinyo cha hiyo demokrasia yao lakini pia mamluki wangekwisha kwenye huu mchezo mchafu.
Ruzuku ni vema iendelee, kama kuna watu wanaikwapua kwa shughuli binafsi utaratibu mwingine uangaliwe ili washughilikiwe kijinai. Na pia ruzuku haiwezi kubinya demokrasia mkuu
 
Hahahaah ulikuwa bado? Me nimemaliza juzijuzi sijakutana na hiyo 15%
Dogo si tumesoma wote iweje we umalize kabla yangu....au naibiwa? Hebu nipe namna ya kuona bado sh ngapi nadaiwa nikamalizane nao waache kunilamba hela ya mama yeyoo
 
Bora leo umejionyesha rangi yako halisi afu huwa unajiita chadema bila aibu.....

Unasahau ni mikutano hyo hyo ilizaa mchakato wa katiba mpya, ilizaa uwajibikaji baada ya kuibuliwa tuhuma nyingi za kifisadi ambazo watu kma mramba na yona wakachukuliwa hatua....

ilizaa kukosoa serikali ili ijirekebishe mfano gharama za safari za nje na ukubwa wa baraza la mawaziri na mengi sana yenye tija kwa maendeleo anyway kma unaona KUZUIA MIKUTANO YA kukosoa na kuisimamia serikali kwenye uwajibikaji ni swala la kupongezwa basi sawa tena mwambie na 2020 apunguze gharama kwa kutoweka uchaguzi aendelee tu hadi atakapojiskia.
Amejionesha rangi yake kivipi? Haujui kuna CHADEMA-ASILIA (ya akina Dr Silaa) na CHADEMA- LOWAS (ya akina Lowasa & Sumaye)? Yeye bila shaka ni chadema asilia, tena damu damu, na wewe bila shaka ni chadema lowasa mabadiliko, tena damu damu vile vile!! Ni kama ilivyo CUF sasa hivi. Kuna CUF-LIP na CUF-SEF. Umeona eeh?
 
Bora leo umejionyesha rangi yako halisi afu huwa unajiita chadema bila aibu.....

Unasahau ni mikutano hyo hyo ilizaa mchakato wa katiba mpya, ilizaa uwajibikaji baada ya kuibuliwa tuhuma nyingi za kifisadi ambazo watu kma mramba na yona wakachukuliwa hatua....

ilizaa kukosoa serikali ili ijirekebishe mfano gharama za safari za nje na ukubwa wa baraza la mawaziri na mengi sana yenye tija kwa maendeleo anyway kma unaona KUZUIA MIKUTANO YA kukosoa na kuisimamia serikali kwenye uwajibikaji ni swala la kupongezwa basi sawa tena mwambie na 2020 apunguze gharama kwa kutoweka uchaguzi aendelee tu hadi atakapojiskia.
Sure brother
 
Back
Top Bottom