Tanganyika Law Society: TAARIFA YA DHARURA juu ya Muswada wa Katiba

Mkuu.
Mimi nimefahamu unayosema ila nimesema kama hao wa Zanzibar wana ZLS hawa wa TLS hawapaswi kujiita Watanzania bara. wajiite wanasheria wa Tanganyika au wanapata ugumu katika hili...ndio nimesema wamekubali kuchakachuliwa?

Kuna Tanzania, hakuna Tanzania bara au Tanzania visiwani hii ndio hoja yangu.
Tanzania ina pende mbili, moja Tanganyika na ya pili ndio Zanzibar.

Na kwa hiyo, wapo watanzania walio watanganyika na wapo watanzania ambao ni wazanzibari. Is that so complicated?

Ndio nimekosoa vipengele vya 6 na 11 walivyovitolea ushauri. Ona post #26,hata hivyo nimewapa big up kwa kutoka usingizini.Ni mwanzo mzuri.

Wanasheria wa Tanganyika wanaposhindwa kuitetea Tanganyika, nani tena ataweza?

Katiba iko wazi ibara ya pili inasema:

Eneo la Jamhuri ya Muungano
(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Kwa mantiki hiyo hatuwezi kusema kuwa Tanzania ina pande mbili moja Tanganyika na ya pili ndio Zanzibar. Tanzania kisheria inaundwa na Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ( sheria ndivyo inavyosema sio mimi).
 
Mkuu
Huo ni upotoshaji wa hiyo sheria. Hakuna sehemu inayoitwa Tanzania bara, hii sehemu ina jina lake na ndio hilo wanalokwepa kulisema ,sijui tunamuogopa nani?, wala hakuna sehemu inayoitwa Tanzania visiwani.
Kama ipo Tanzania Zanzibar sielewi kwa nini isiwepo Tanzania Tanganyika.
Kwa hiyo hii ni sababu tosha ya kuandika katiba mpya na sio marekebisho ya katiba kwa sababu, Hii katiba iliyopo yenyewe ni hovyo kabisa.

Walipotengeneza jina Tanzania walisema Tanganyika na Zanzibar ni jina refu.kwa hiyo walifupishe sasa wanalirefusha tena. usanii per se!
Lakini nimekuelewa mkuu. Zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Back
Top Bottom