Tanganyika Law Society: TAARIFA YA DHARURA juu ya Muswada wa Katiba

Invisible, nimeanzisha similar thread with attachments of the same content.

Tafadhali muiondoe ile ya kwangu ku-avoid unnecessary multiplications.

Well said, mwingine angeanza kulalama. Kweli wewe ni GT.
 
Imewakilishwa kwa niaba ya Chama cha Mawakili Tanzania Bara
Francis K. Stolla
RAIS

Siasa hizoo! Sijui ulipata ridhaa yao?
 
Thank you TLS,tumewasikia,mda mwingi tumekwazika sana kwa sheria yetu kupindishwa na wenye nia mbaya na wtanzania walio wengi
 
Hapa TLS kweli mmetimiza majukukumu yenu ya msingi, acheni kukaa kimya hata kwenye Miswaada mingine mibovu ambayo wabunge wa CCM hutumika kama rubber stamp tu ya kuhalalisha upuuzi wowote unaopelekwa bungeni.
 
Tunashukuru TLS kuingilia suala la muswada wa mabadiliko ya katiba mkiwatazama watanzania tulio wengi. Hatukukosea kuwapeleka shule vijana wetu. Ninyi ni macho yetu.
 
Sina Uhakika kama Werema alikuwa anajua anachokiandika na kukileta kama mswada. Sio wa kitaalamu naona kama wanakosoa IQ yake ilivyo. Waweza tumiwa vibaya na wanasiasa halafu kumbe inaondoa credibility yako kabisa.
 
Wako sawasawa na maoni yangu katika thread juu ya madudu ya muswada huu. Nadhani pia hawa wanasheria walipaswa kujikita katika interpretation section 3 ambayo haija-define president ninini au ni nani?
 
Jamani huu(kwenye RED) ndio mwisho wa fikra za wanasheria wetu as far as Zanzibar concerned?
[/LIST]

Tamko linahusu muswada wa sheria ya marekebisho ya katiba ambao ulisomwa bungeni kwa mara ya kwanza tarehe 5 April 2011. Muswada huyo, amabao tayari umewekwa hapa jukwaani, unazungumzia vitu kadhaa vitakavyoundwa na taratibu za kelekea kwenye katiba mpya.
 
Wameonesha uzalendo.

Lakini pia tayari wameshachakachuliwa akili...
Vipi wao wanajiita watanzania bara, Tanzania mainland...hapa nashindwa kuwaelewa hawa wasomi wetu-
Chama chao kinaitwa Tangayika law society...lakini wanajiita watanzania mainland....wajameni si ndio wamekubali kuchakachuliwa hawa.

Bora wabadilishe jina kutoka Tanganyika law society to Tanzania mainland law society. It will make sense.
:: Tanganyika Law Society Official Website ::
Halafu hakuna mtanzania bara wala mtanzania visiwani..kuna mtanzania tu ambaye ama ni mtanganyika au mzanzibari.
These "msomis" iko confuse us!
They are confused or brainwashed and they want to confuse us.

Jina la chama kisheria ni Tanganyika Law Society lakini memebers wake ni wanasheria wa Tanzania bara kwa sababu wanasheria wa Zanzibar wana chama chao kinachoitwa Zanzibar Law Society
 
Upande mwingine wa shilingi ni kuwa kuna majaribio ya kufanya suala la Katiba kuwa ni suala la "wasomi". Kama vile tunavyomkatalia Rais nguvu ya kuweza kuamua Katiba inakuwaje viile vile tunawakatalia Wasomi na wanasiasa kuteka hoja ya Katiba Mpya na hivyo kujipa wenyewe madaraka ya kuandika Katiba mpya kwa sababu wao ni "wasomi". Tayari nimeshaanza kuona dalili za watu wasio wasomi au wanakijiji "wenzangu" kuanza kutengwa kwa kisingizio kuwa "hawajui Katiba" au "hawawezi kujadili kwa kina".
 
Nashukuru na wewe umeliona hilo. Tena hawa wanaojiita "wasomi", hao "learned brothers and sisters" nimeshaanza kuona vidalili dalili vya wao kujiweka kimbelembele.

Halafu mimi hii lugha ya eti 'muswada wa marekebisho' sijaipenda kabisa. Kwa nini isiwe 'muswada wa uundwaji' wa katiba mpya? Huwezi kurekebisha kitu kipya. Unarekebisha kile ambacho tayari kipo.

I don't know man...maybe it's just me. But something definitely ain't right somewhere but I just can't put my finger on it.
 
thanks mawakili wetu but kama mmechelewa vile, mlitakiwa kuamka mapema mjadala huu ulipo anza

Muswaada umesomwa na waziri tarehe 5 April 2011, hapo ndio kisheria muswada huo ulikuwa Public, statement imesomwa tarehe 9 April 2011, i.e four days laters. Wasingeweza kucomment kuhusu muswada amabao sio public. Kwa mawazo yako wewe unaona lini walitakiwa kutoa hayo mawazo? Kama wamechelewa je kuna madhara yoyote yaliyotokana na kuchelewa huko kwa siku nne? Lets say tayari muswada huo umekuwa sheria etc.
 
1. Kuhusu lugha ya Muswada: Chama kinapendekeza kwa msisitizo kwamba Muswada utangazwe katika lugha ya Kiswahili, kwa kuzingatia dhana ya haki kupatikana (jambo ambalo linamaanisha mtu wa kawaida kupata nakala na uelewa) kwa Watanzania wote (wanaoishi vijijini na mijini, wananchi wa kawaida, wenye mapato ya kati na wa matabaka ya juu), ikiwa ni sambamba na lugha inayotambulika ya toleo rasmi la Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya[/SIZE][/FONT] Tanzania, 1977 (kwa kifupi "Katiba");

Nyie "wasomi" aka "learned brothers and sisters" (sijui kwa nini mnajiita wasomi as if mnajiona mmesoma kuliko wenzenu - kuiga iga tu, anyway that's besides my point). Kwa nini msianzishe kampeni ya kuzibadili sheria zetu ambazo nyingi zimetungwa kwa lugha ya kigeni kwa misingi hiyo hiyo ambayo mnataka muswada utangazwe kwa Kiswahili?

Sheria si ni zetu wote? Sasa hebu jiulizeni wangapi katika Tanzania yetu hii wanaielewa hiyo lugha ya kigeni? Nyie wenyewe hamuielewi vizuri. Kazi kuunga unga tu. Muda umefika sasa wa sheria zetu zote zinazoiongoza jamii yetu ziwe kwenye lugha yetu inayofahamika na wengi.
 
Mimi siwadharau. Lakini si unaona mahakama zetu zinavyohukumu? Si unaona tunavyoingia mikataba yetu na kampuni za nje? Si unaona miswada ya ajabu inavyoandaliwa kupelekwa kwenye Bunge letu mbumbumbu? Sheria ni taaluma ya zamani sana nchi hii. Kuna haja ya kuwa na Bodi yao ya kitaaluma. Hizo BAR EXAMS ni vitu vidogo mno.

Naona hujaelewa mgawanyiko wa fani ya sheria, Mahakimu na Majaji hawapo chini ya TLS, Miswaada haitayarishwi na TLS bali hutayarishwa na kitengo cha kuandika sheria chini ya ofisi ya mwanasheria wa Serikali, Mikataba ya serikali haitayarishwi na wananchama wa TLS ( in their individual capacity) bali kuna wanasheria wao.

Kuna kitu kama" Bodi" , kinaitwa, Council for Legal Education amabao hushughulikia bar exams za kitaaluma , Council amabayo sio kitu kidogo kama unavyofikiri kuanzia composition mpaka kila kitu.
 
Upande mwingine wa shilingi ni kuwa kuna majaribio ya kufanya suala la Katiba kuwa ni suala la "wasomi". Kama vile tunavyomkatalia Rais nguvu ya kuweza kuamua Katiba inakuwaje viile vile tunawakatalia Wasomi na wanasiasa kuteka hoja ya Katiba Mpya na hivyo kujipa wenyewe madaraka ya kuandika Katiba mpya kwa sababu wao ni "wasomi". Tayari nimeshaanza kuona dalili za watu wasio wasomi au wanakijiji "wenzangu" kuanza kutengwa kwa kisingizio kuwa "hawajui Katiba" au "hawawezi kujadili kwa kina".

Hiyo ndio hoja ya kwanza kabisa:

Chama kinapendekeza kwa msisitizo kwamba Muswada utangazwe katika lugha ya Kiswahili, kwa kuzingatia dhana ya haki kupatikana (jambo ambalo linamaanisha mtu wa kawaida kupata nakala na uelewa) kwa Watanzania wote (wanaoishi vijijini na mijini, wananchi wa kawaida, wenye mapato ya kati na wa matabaka ya juu), ikiwa ni sambamba na lugha inayotambulika ya toleo rasmi la Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, 1977 (kwa kifupi "Katiba");
 
Kama lugha ya katiba ni Kiswahili nini kinachokwamisha sheria zingine ziwe kwenye Kiswahili?
 
Nashukuru na wewe umeliona hilo. Tena hawa wanaojiita "wasomi", hao "learned brothers and sisters" nimeshaanza kuona vidalili dalili vya wao kujiweka kimbelembele.

Halafu mimi hii lugha ya eti 'muswada wa marekebisho' sijaipenda kabisa. Kwa nini isiwe 'muswada wa uundwaji' wa katiba mpya? Huwezi kurekebisha kitu kipya. Unarekebisha kile ambacho tayari kipo.

I don't know man...maybe it's just me. But something definitely ain't right somewhere but I just can't put my finger on it.

Pendekezo la pili limezingatia hio, jina haliendanu na dhamira ya kuwa na katiba mpya
 
Jina la chama kisheria ni Tanganyika Law Society lakini memebers wake ni wanasheria wa Tanzania bara kwa sababu wanasheria wa Zanzibar wana chama chao kinachoitwa Zanzibar Law Society
Mkuu.
Mimi nimefahamu unayosema ila nimesema kama hao wa Zanzibar wana ZLS hawa wa TLS hawapaswi kujiita Watanzania bara. wajiite wanasheria wa Tanganyika au wanapata ugumu katika hili...ndio nimesema wamekubali kuchakachuliwa?

Kuna Tanzania, hakuna Tanzania bara au Tanzania visiwani hii ndio hoja yangu.
Tanzania ina pende mbili, moja Tanganyika na ya pili ndio Zanzibar.

Na kwa hiyo, wapo watanzania walio watanganyika na wapo watanzania ambao ni wazanzibari. Is that so complicated?

Ndio nimekosoa vipengele vya 6 na 11 walivyovitolea ushauri. Ona post #26,hata hivyo nimewapa big up kwa kutoka usingizini.Ni mwanzo mzuri.

Wanasheria wa Tanganyika wanaposhindwa kuitetea Tanganyika, nani tena ataweza?
 
Chama chao kinaitwa Tangayika law society...lakini wanajiita watanzania mainland....wajameni si ndio wamekubali kuchakachuliwa hawa.

Bora wabadilishe jina kutoka Tanganyika law society to Tanzania mainland law society. It will make sense.
:: Tanganyika Law Society Official Website ::
Halafu hakuna mtanzania bara wala mtanzania visiwani..kuna mtanzania tu ambaye ama ni mtanganyika au mzanzibari.
These "msomis" iko confuse us!
.

Jina la chama kisheria ni Tanganyika Law Society lakini memebers wake ni wanasheria wa Tanzania bara kwa sababu wanasheria wa Zanzibar wana chama chao kinachoitwa Zanzibar Law Society

Nonda dont get confused.
Tanganyika bado ina-exist.
Kumbuka na hili Medical Council of Tanganyika
 
Back
Top Bottom