Tanga: Hospitali ya Mji Korogwe (Magunga) yabainika kuhifadhi Damu kwenye Mafriji ya Nyumbani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,516
8,419
Mwezi mmoja baada ya kubainika jokofu la matumizi ya nyumbani kuhifadhia damu katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, hilo limebainika tena mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali (Tamisemi), Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Dk Rashid Mfaume akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika Mkoa wa Tanga amebaini jokofu la matumizi ya nyumbani likitumika kuhifadhia damu katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Korogwe (Magunga).

Kutokana na hilo, Dk Mfaume ameelekeza kufanyika utaratibu wa haraka wa upatikanaji wa jokofu maalumu kwa ajili ya kuhifadhia damu.

"Hili jokofu ambalo mnatunzia damu ni kama tulilolikuta kule na hii tumeletewa na mdau, tumetoka kule Shinyanga, Mwalugulu tumewasema tukajua huku mmejifunza mtahangaika. Hatutaki kuona haya yanayofanyika huku tuyaone sehemu nyingine,” amesema.

“Mnaonekana Korogwe TC (Halmashauri ya Mji) mna wataalamu wa kununua majokofu ya nyumbani, maabara tumeenda tumekuta majokofu sita," amesema Dk Mfaume.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom