TANESCO watorosha Maji Bwawa la Nyerere, na kuharibu mazao Kwa mafuriko

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Licha ya TANESCO kutoa adhabu ya kugawa Umeme Kwa wananchi wa TANZANIA na kuendeleza mateso hawajaridhika na sasa wameamua kufungulia maji ya bwawa la nyerere na kusababisha mafuriko makubwa na uharibifu wa mazao katika vijiji vilivyopo mkondo wa chini wa bwawa hilo.

Maji hayo ambayo yanatoroshwa na TANESCO yalipaswa kutumika katika uzalishaji wa Umeme, hata hivyo kutokana na usimamizi mbovu wa shitlrika, Mradi huo umeshindwa kukamilika Kwa wakati na hivyo kupelekea maji yaliyojazwa yasiwe na kazi yoyote ya maana kwani ni mashine moja tu inayotembea ambayo inahitaji maji kidogo.
Ulimbukeni wa TANESCO katika kukimbilia kujaza bwawa wakati wanajua maji hayatatumika huku wakijua fika masika inakuja ni makusudi tu. Ni afadhali na Bora wakati wa kiangazi wangeruhusu maji ,ili masika ikija ndo maji yajae kwa kasi na kuzuia mafuriko.

TANESCO Walikwepa kuhamisha wanakijiji wa mkondo wa chini ili kukwepa kuwalipa fidia hivyo Sasa hivi wanakijiji wanakomeshwa Kwa ufunguliaji maji.

TANESCO ilisema na kutoa Hadi kuwa itakuwa ikiachia maji kiasi Cha cubic MITA 200 Kwa sekunde ili kulinda ekolojia, lakini kinyume chake Sasa hivi tunapoongea maji yanayotoroshwa ni cubic mita 6000 kwa sekunde sawa na sim Tank 600 za lita 10000 kwa sekunde ,maji yote yameelekezewa kwa wapiga kura wakaogelee.

TANESCO wamesema wataendelea kufungulia maji Hadi mwezi wa Tano, Sasa hii Ina maana gani. Mazao hamna, Umeme hamna, fidia hamna, bado tu tunapiga mwingi.

[3/17, 4:52 PM] Green:
View: https://youtu.be/_KtwmwYstjA?si=Weiy0RfEGyVI7uVA

[3/17, 5:02 PM] Green:
View: https://youtu.be/WUgFXBz6raI?si=TBZ8ExKk6pkg1c0w
 
Tunapoteza sana maji, utasikia miaka miwili baadaye kuna ukame bonde la Rufiji maji yote yamekwenda baharini.

Ilitakiwa kuwepo mpango kuyavuna maji haya kwa kutumia bwawa la pili .


Maktaba :


2022 17 November

MTO RUAHA MKUU / GREAT RUAHA UKAME WALETA UPUNGUFU WA MAJI TISHIO KWA MRADI WA BWAWA LA JNHPP NA KILIMO


View: https://m.youtube.com/watch?v=PYusp9vNzkE
Waziri wa Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Said Jafo akiongozana na mawaziri wa kisekta, wakuu wa Mikoa kutoka mikoa mbalimbali ya nyanda za juu kusini na viongozi wengine katika Ziara ya siku moja kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa lengo la kuangalia hali ya Ukame mwaka 2022 unaoikabili Hifadhi hiyo ambao unahatarisha ustawi wa mto Ruaha mkuu.
 
Wajinga wapo madarakani usitarajie ufanisi kwenye jambo lolote.
 
Back
Top Bottom