TANESCO: Rationing is back!

Tanesco bana, walijishaua sana eti kukatikatika huko sio mgawo bali ni matatizo ya ufundi wapiii.Tanesco kwa uongo ni kama chama cha magamba vile,sawa ufumbuzi nilionao,ili nisikwame kufanya kazi nanunua tablet angalau masaa matano kazi zangu nitakuwa nimeshafanya, clients wa nje ukiwaambia nashindwa kumaliza kazi sababu hakuna umeme hawakuelewi,unabaki kuulizwa are you serious?loh hawa Mapacha watatu kweli wametukomoa,halafu eti ndio tunaambiwa ''ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu linalongojea kulipuka''ovyoooo.Panapo uhai tutaonana kwenye kisanduku cha kura,itakuwa kumkoma nyani girani
 
Kama Zitto na January wana ubavu waamuru jenereta za Ikulu zitolewe. Au jenerator za pale Hazina anakofanyia Mkullo ziondelewe. Hapo nitaamini kweli wanataka kutatua tatizo la umeme. Otherwise wanataka kutuondoa kwenye mjadala wa umri wa urais baada ya kuona public reaction.

Kwa watu wanataka kutuaminisha kuwa wana 'uelewa' mkubwa kwenye mambo ya utawala inakuwaje wanashindwa kujua nafasi na uwezo wa mkurugenzi mkuu wa Tanesco katika kushughulikia umeme hapa nchini? Mhando anajidhamini mwenyewe kuchukua mkopo bank? Au Tanesco imeshindwa kuilipa Agreko kwa sababu ya jenereta ya Mhando?

Kwa nini hawataki kusema Tanesco imekuwa cash-cow wa Dowans na miradi mingine ya wakubwa?
 
Tatizo wananchi wa Tanzania tunaonewa sana na kunyanyasika na huu mfumo wa kifisadi wa serikali ya CCM, ishu ya umeme kwa nchi yetu ni mradi wa wakubwa wa nchi na wanauendesha kisiasa zaidi kuliko kitaalamu hapo ndo tatizo kubwa lilipo kama ikiwezekana wataalamu wakawa centred ktk ishu ya umeme naona tutaweza kumove. maana tukianzia Richmond,Dowans,Iptl na makampuni mengine mengi ya dharura hayana msaada badalayake ni mzigo kwa Tanesco na wananchi wa Tanzania.
Kuhusu hiyo kauli ya bwana Zitto imekaa kisiasa zaidi hata wakimwondolea jenerator huyo mkurugenzi tatizo la umeme litakuwa solved?
 
hivi ile kauli ya ngeleja kwamba mgao wa umeme utakua historia umeishia wapi?

Unaweza kutafsiri kwa pande mbili positive na negative. Inaweza kuwa historia kwa maana kwamba utachukua muda mrefu sana hadi kuja kumalizika kabisa. Kwahiyo itakuwa ni historia.
 
Zitto ni mnafki tu Hana jipya.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Tuwe na msimamo wa pamoja kwamba mtu anapofanya jambo la kustahili kupongezwa tufanye hivyo akikosea tunamkosoa. Kwa hapa Zitto na timu yake wanastahili pongezi za dhati kabisa kwa maamuzi hayo mazito si jambo dogo hata kidogo. Hongera Zitoo na timu yako kwa hili. Acha naye ajuwe makali ya mgawo pengine atashughulikia vizuri miradi ya TANESCO na kulitoa shirika hilo mikononi mwa Songas na Agrekko wanaolinyonya kwa mtindo wa kumkamua panya.
 
hivi ile kauli ya ngeleja kwamba mgao wa umeme utakua historia umeishia wapi?
Kwani huwajui magamba? Ndiyo hapo mimi nikisema natamani mapinduzi watu wananipinga. Kwa serikali ya kihuni kama hii hivi kwanini mtu usitamani mapinduzi. Bora kuongozwa na wanajeshi kuliko kuongozwa na walevi kama akina JK. Huu ni mwezi wa tatu tu, wanatangaza mgao wa umeme ilihali mabwawa bado yamejaa, hivi itakapofika mwezi wa kumi na moja hali itakuwaje? Na watatuambiaje wapo serious na suala la kupunguza umasikini?
 




Monday, 26 March 2012 20:23

lizimwe.jpg
Mkungenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando (katikati), akiwa na baadhi ya maofisa wa shirika hilo wakiwasiliana kuhusu kurekebisha ripoti kabla ya kuingia katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) jijini Dar es Salaam jana. Picha na Fidelis Felix

Boniface Meena


KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma(POAC), imeagiza Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuondoa jenereta la dharura lililopo nyumbani kwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, William Mhando kuanzia leo ili naye ajue machungu ya kukatika umeme mara kwa mara.

Wakati POAC ikiagiza kuondolewa kwa jenereta hilo, taarifa zinaeleza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Jenerali Mstaafu, Robert Mboma amemwandikia Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja akihoji sababu za kutokutekelezwa kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete la kulipatia shirika hilo kiasi cha Sh408 bilioni kwa ajili ya kujiendesha.
Barua ya Mboma ya Machi 20, mwaka huu kwenda kwa Ngeleja, ambayo gazeti hili imefanikiwa kuiona, ilisema mnamo Machi, 8 mwaka huu, Rais Kikwete aliagiza Tanesco ipewe haraka mkopo huo wa Sh408 bilioni lakini akasema hadi sasa amri hiyo ya Amiri Jeshi Mkuu haijatimizwa.

“Mheshimiwa Rais tarehe 8 Machi aliagiza kuwa mkopo huo wa Sh408 bilioni upatikane haraka. Lakini, sisi tunazunguka na hivyo kushindwa kutii amri ya Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania. Katika hali ya kawaida, tunatakiwa tufanyekazi usiku na mchana kwa nia ya kukamilisha maagizo halali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano," inasema sehemu ya barua hiyo ya Mboma.

Katika sehemu nyingine ya barua hiyo, Mboma alisisitiza: "Hali ya mabwawa yanayotegemewa ya Mtera na Nyumba ya Mungu ni mbaya sana. Ukosefu wa mafuta utatulazimu tutumie maji hayo... hii maana yake ni kuwa mwakani tutalazimika kukodi mitambo mingine ya dharura kwa sababu mitambo ya sasa, muda wake utakuwa umekwisha. Watanzania hawatatuelewa na Tanesco italaumiwa bure kwa sababu tuko ambao hatutii amri za ngazi za juu."

Mboma katika kuhakikisha agizo hilo la Rais linatekelezwa, aliomba kikao kati yake na Waziri Ngeleja, Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, wajumbe wawili wa bodi, menejimenti ya shirika hilo na wajumbe wengine ambao waziri huyo angeona wanafaa.

“Lengo liwe ni kutafuta njia za kufanya ili turekebishe kasoro. Wakati huohuo; napendekeza Katibu Mkuu wetu azungumze na mwenzake wa Hazina. Hii iwe baada ya menejimenti ya Tanesco kumjulisha juu ya mazungumzo yao,” ilisisitiza barua hiyo na kuongeza:

“Itapendeza kama Katibu Mkuu (WNM) atakuwa amezungumza na mwenzake wa Hazina kabla ya kikao chetu. Baada ya hapo, naona tuone jinsi ya kuzungumza na mheshimiwa Rais. Suala hili ni zito."

Nakala ya barua hiyo ilipelekwa pia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Ofisi ya Rais, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu Nishati na Madini, Msajili Hazina na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco.

Msimamo wa POAC

Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe akizungumzia suala la jenereta alisema ni lazima liondolewe kwa kuwa linatumia mafuta ya Serikali na ndiyo maana mkurugenzi huyo hawezi kujua adha iliyopo kwa wananchi pindi umeme unapokatika.

“Tumemtaka Jenerali Mboma afanye hivyo kwa kuwa haiwezekani mkurugenzi wa huyo awekewe jenereta kwani kwa kufanya hivyo inadhihirisha kwamba hawana umeme wa uhakika,” alisema.

Zitto alisema wameagiza hilo lifanyike haraka na kama mkurugenzi huyo anataka kuwa na jenereta anunue la kwake binafsi na si kutumia la umma na mafuta ya Serikali.

Alisema Tanesco imeendelea kuelemewa na mzigo wa kununua umeme kutoka makampuni binafsi na imepata hasara ya Sh47 bilioni kutoka Sh43 bilioni mwaka 2009.

Zitto alisemza mwaka 2010, Tanesco ilitumia kiasi cha Sh211 bilioni kununua umeme wa dharura kutoka kampuni binafsi na asilimia 90 ya fedha hizo zimetumika kwa Songas na IPTL… “Songas wametumia kiasi cha Sh127 bilioni na Sh64 bilioni zimetumika kwa IPTL.”
Alisema kutokana na hali hiyo wameitaka Tanesco kuanzia Mei mwaka huu, waache kutumia mitambo ya IPTL baada ya mtambo wao mpya wa Jacobsen unaojengwa Ubungo, Dar es Salaam kuanza kufanya kazi na kuzalisha megawati 100.

Zitto alisema hivi sasa Tanesco wamepunguza gharama za uendeshaji lakini wanatumia Sh499 bilioni kuzalisha na umeme ambao wakiuza wanapata Sh466 bilioni na ukiongeza gharama nyingine za mishahara unakuta wanapata hasara ya Sh47 bilioni kila mwaka.

Kuhusu kuwepo kwa mgawo wa umeme Zitto alisema Tanesco imekubali kuwa kuna mgawo usio rasmi na hiyo inatokana na kukosa dhamana kutoka serikalini ya kupata mkopo wa Sh408 bilioni ili iweze kununua umeme wa dharura na kuondokana na tatizo la umeme.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alisema hali ndani ya shirika hilo ni mbaya kwa sababu haina fedha za kuliendesha na kwamba hawawezi kununua vipuri.

Alisema kutokana na hali hiyo umeme unaokatikakatika ni mgawo lakini shirika hilo limekuwa likikanusha kwa sababu uwezo limekuwa likipokea malalamiko mengi yanayohusu ukatikaji huo hasa Dar es Salaam.

“Hali ya mabwawa kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Jenerali Mboma inaeleza kuwa ni mbaya kwani Mtera lina mita 1.24 tu juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa na sasa bado mita 5.26 kufikia kima chake cha juu,” alisema Zitto na kuongeza:

“Nyumba ya Mungu ina mita 3.22 juu ya kina cha chini kinachoruhusiwa na ni mita 9.76 kufikia kina cha juu cha bwawa hilo hivyo maji kwenye mabwawa hayo ni kidogo hasa kama mvua haitanyesha maeneo ya Mbeya Dodoma, Arusha Kilimanjaro, Singida na Tanga.”

Alisema ukosefu wa fedha za kununulia mafuta utalazimu watumie maji hayo kidogo ili wasifanye mgawo wa umeme na hiyo maana yake ni kuwa mwakani watalazimika kukodi mitambo mingine ya dharura kwa sababu ya sasa muda wake utakuwa umekwisha.

Zitto alisema kutokana na hali hiyo, wamemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kushughulikia suala hilo ili fedha hizo zipatikane.

“Mtambo wa Aggeko umezimwa na IPTL pia ambayo yote kwa ujumla huzalisha megawati 150,” alisema.

Awali, kabla ya kuhojiwa na POAC Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi William Mhando alisema tatizo la umeme katika Mkoa wa Dar es Salaam litakwisha baada ya wiki nne kwa kuwa wahandisi wa shirika hilo wanafanyia kazi matatizo yaliyopo.Alisema kukatika umeme mara kwa mara hasa maeneo ya Mbagala, Temeke na Kigamboni kunatokana na mfumo wa umeme uliopo kuchakaa na ili kutatua tatizo hilo wameagiza transfoma nne za dharura.

“Hali ya umeme si mbaya tunamudu mahitaji kwa kutumia maji japokuwa si mengi na pia tunatumia gesi. Mifumo yetu ya umeme si mizuri kwa kuwa imechakaa,” alisema Mhando.

Tumechoshwa na huu ubwekaji wa mbwa ambao hawaumi wala kuwazuia waizi kuiba, Tired na story hizi Tanzania, very tired in deed. Naomba kuwasihi vyombo vya habari, msiwemnapoteza muda wenu kuandika habari za kipuuzi kama hizi wakati watanzania tunategemea kusikia maamuzi yenye mazito yenye kutatua kero zetu.
 
Ni kwa nini wasifanye hivyo Magogoni? Maana kule ndio shina lilipo usipowaka umeme kule siku tatu mfululizo,nadhani mambo yataenda vizuri nchi nzima.
 
Watanzania dawa ya uwoga wetu imepatikana
1.maisha magumu kwa waadilifu na maisha bora kwa mafisadi
2.serikali legelege
3.mawaziri wasiokuwa na kitu kichwani ngereja,mponda,pinda,kawambwa,mwakyembe,mwandosya etc.
4.ongezea mwenyewe
mpaka mtaonea tu hapa ni mwisho wa reli
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Tuwe na msimamo wa pamoja kwamba mtu anapofanya jambo la kustahili kupongezwa tufanye hivyo akikosea tunamkosoa. Kwa hapa Zitto na timu yake wanastahili pongezi za dhati kabisa kwa maamuzi hayo mazito si jambo dogo hata kidogo. Hongera Zitoo na timu yako kwa hili. Acha naye ajuwe makali ya mgawo pengine atashughulikia vizuri miradi ya TANESCO na kulitoa shirika hilo mikononi mwa Songas na Agrekko wanaolinyonya kwa mtindo wa kumkamua panya.

kaka jitahidi kuelewa akili za viongozi wa bongo kama akina zito kabwe, hawa ni typical politicians ambao kusudi lao ni kuendesha ujinga wa watanzania kwa umaarufu wao, huwa hawapendi kufanya jambo bila wao kupata umaarufu!

Jukumu la kamati yao nikuhakikisha inamonitor namna tanesco na wizara kwaujumla inavyoendeshwa na wao kuwa sehemu ya kutatua matatizo yanayoikabili tanesco na sio kikwazo kwa utatuzi wa matatizo ya tanesco.

Kama kamati basi hakuna kamati mbovu kama hii ya watu wanotakakujitafutia umaarufu kwa vitu vidogo kama kumtolea jenereta mkurugenzi wa shirika kubwa kama tanesco badala yakujana suluhu ya matizo y umeme nchini, hivi kumtolea generator mkurugenzi taongeza megawati ngapi?

Ninaimani kutokana umuhimu wa sector hii ya umeme ilipaswa viongozi wa kamati za bunge kuwa walikuwa wanawasiliana na viongozi wa tanesco marakwa mara kuhakikisha maagizo ya bunge yanatekelezwa je! inamaana zito na mwenzake walikuwa hawajui kama kuna ugumu wowote katika kupata pesa hizo zinzotaka kukopwa na tanesco?
Kamati inapaswa kufatilia nikiasi gani maagizo ya bunge yametekelezwa, kiasigani bado, kuhoji kwanini bado na kutafuta suluhu pamoja.

Tuache kushabikia maamuzi ya wanasiasa uchwara wanaotafuta njia ya kuwarubuni watanzania kwaajiri ya umaarufu wao binafsi.
 
Laana ya wa Tz wanyonge ndiyo chimbuko la haya yote tuyaonayo leo hii. Na bado itaendelea kutuandama laana hii mpaka hapo tutakapokubali kubadili yaliyo ndani ya nafsi zetu na kutambuwa kuwa ipo jamii nyingine ambayo nayo inasitahili kuthaminiwa na kuishi maisha ambayo jamii nyingine inaishi. Mungu ibaliki Tanzania Mungu waangamize madhalimu wa Nchi hii kwa njia yoyote uijuayo.
 
Source Majira

Kumbe tunaendelea kuganganywa kuwa mitambo ni michakavu ndo maana kuta kukatika katika kwa umeme kumbe ni madeni yanayowafanya washindwe kuzalisha umeme hasa unaozalishwa na kampuni ya Aggreco (samahani kama nitakuwa nimekosea kuiandika) kuidai tanesco zaidi ya billion 300/=

hiyo imebainishwa na mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini mh January Makamba hapo Jana

Watanzania tunaisaidiaje tanesco kuibanafsisha tena au kuongezewa tena bei mpya
 
mhando tanesco2.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando,


Midraji Ibrahim

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando, amesema ingawa suala la kupatiwa umeme lipo kwenye stahili za mkataba wake, hawezi kubishana na uamuzi wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) wa kuondoa jenereta nyumbani kwake.

Akizungumza kufuatia agizo la POAC kuondoa jenereta hiyo nyumbani kwake jana, ili aonje uchungu wa kukatika kwa umeme, Mhando alisema alishtushwa na hatua hiyo kwa sababu ni suala la mkataba, lakini hawezi kubishana na kamati.

"Mkataba ninao jana (juzi) nilishtuka kuhusu agizo hilo kwa sababu niliajiriwa na bodi na mwenyekiti wangu alikuwapo tutakaa tuangalie, lakini siwezi kupingana na maagizo ya kamati," alisema Mhando.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa wa Bodi ya Tanesco, Jenerali mstaafu Robert Mboma, alisema watatii agizo la POAC la kuondoa jenereta la dharura lililopo nyumbani kwa mkurugenzi huyo.

"Tumeagizwa na kamati tutaangalia jinsi ya kulitekeleza agizo hilo la kuondoa jenereta, tupeni siku tatu au nne hivi mtaona," alisema Jenerali Mboma.

Alipoulizwa kama kuondoa jenereta hiyo haitakuwa kinyume na mkataba wa ajira unaoonyesha stahili za mkurugenzi huyo, Mboma alisema: " Unadhani tutafanya nini kama tumeagizwa tuiondoe, hatuna jinsi hata kama kuna mkataba sisi tutatekeleza tuliyoagizwa."

Mhando alisema suala la kukatika kwa umeme unaondelea hivi sasa, halisababishwi na menejimenti bali inatokana na kutokuwapo kwa uwekezaji muda mrefu kwenye shirika hilo, baada ya kuwekwa chini ya Shirika la Kubinafsisha na Kuuza Mashirika ya Umma (PSRC).

"Tangu mwaka 1999 hadi 2007 hakuna uwekezaji uliofanywa kwa Tanesco baada ya shirika kuwekwa chini ya PSRC, kwa hiyo kukatika kwa umeme kunaokoonekana hivi sasa ni matokeo ya ubinafsishaji uliolengwa," alisema.

Mkurugenzi huyo alisema kukatika kwa umeme kunatokana na uchakavu wa miundombinu, lakini siyo kuzidiwa na kwenye uzalishaji kwa sababu hivi sasa wanazalisha Megawati 782.51 ilhali mahitaji ni Megawati 772.15.

"Mfano pale City Center (katikati ya jiji), tulikuwa na transfoma mbili zote zimetumika zaidi ya miaka 30, Februari mwaka huu zimeharibika, tumeagiza kutoka Uturuki na sasa zimefika Dubai, tatizo ni miundombinu imechakaa," alisema.

Kuhusu Aggreko na Symbion Dodoma kuzima mitambo yao, Mhando alikiri kuwa hatua hiyo inatokana na deni ambalo linafikia Sh62 bilioni na kwamba, IPTL imepunguza uzalishaji kutoka Megawati 100 hadi 50. Aggreko inadai Sh58 bilioni na Symbion Dodoma Sh4 bilioni.

"Mgawo kwa maana ya uwezo wa kuzalisha hatuna, ila hii kukatikakatika kwa sababu ya transfoma hiyo ipo. Tupo kwenye hatua mbalimbali za kukarabati miundombinu hiyo na baada ya kipindi tatizo hilo litatoweka," alisema.

Mhando alisema hivi sasa wamepata dola 85 milioni za Marekani kwa ajili ya Dar es Salaam, Euro 25 milioni kutoka Finland na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) imetoa dola 40 milioni za Marekani.

Juzi, Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe, alisema lazima jenereta lililoweka nyumbani kwa mkurugenzi huyo liondolewe kwa sababu linatumia mafuta ya Serikali.

CHANZO: Mkurugenzi Tanesco asikitishwa uamuzi wa POAC

Mkuki kwa Nguruwe kwa Binadamu ni mchungu. Mkuu itabidi na wewe uonje Machungu ya Umeme wa Mgao.
 
Back
Top Bottom