TANESCO: Rationing is back!

USANII KILA MAHALI! MSANII KILA MTU!
Watazamaji wa sanaa hii ni Watanzania walipa kodi, Watanzania ambao kila kukicha wanakamuliwa kwa kodi na mfumko wa bei.

Mimi ninamuonea haya Mungu kumwambia "Mungu Ibariki Tanzania!"
 
Vipi watu wangu, hamjambo? Nasikitika kuwajulisha kuwa TANESCO wametangaza mgao wa umeme tena rasmi leo. Utaisha lini??.... mimi na wewe hatujui! Lakini tusiwe na shaka, taa ya ajabu(crankbox) pamoja na moonlight solar zipo kwa ajili yako. Mwanga utapata, mawasiliano utapata, kwa bei nafuu, wakati wowote, popote ulipo.
CB_New.jpg
Taa Ya Ajabu - Tshs: 40,000/=
moonlight.jpg
Moonlight Solar - Tshs: 35,000/=
Hizo bei ni za mwisho (fixed price).

ZINAPATIKANA MBEZI BEACH KITUO CHA SAMAKI INDEPENDENT INTERNET CAFE
K/KOO MTAA WA MAFIA & SWAHILI DUKA LINAITWA WINO WORKS...
KARIBUNI SANA...
 
Vipi watu wangu, hamjambo? Nasikitika kuwajulisha kuwa TANESCO wametangaza mgao wa umeme tena rasmi leo. Utaisha lini??.... mimi na wewe hatujui! Lakini tusiwe na shaka, taa ya ajabu(crankbox) pamoja na moonlight solar zipo kwa ajili yako. Mwanga utapata, mawasiliano utapata, kwa bei nafuu, wakati wowote, popote ulipo.
View attachment 50291
Taa Ya Ajabu - Tshs: 40,000/=
View attachment 50292
Moonlight Solar - Tshs: 35,000/=
Hizo bei ni za mwisho (fixed price).

ZINAPATIKANA MBEZI BEACH KITUO CHA SAMAKI INDEPENDENT INTERNET CAFE
K/KOO MTAA WA MAFIA & SWAHILI DUKA LINAITWA WINO WORKS...
KARIBUNI SANA...

Conflict of interest::::For promotional use only
 
Nilijua hili litakuja kutokea toka siku ile Ngeleja alipowasilisha kwa mara ya pili bajeti yake ikiambatana ule mpango wa mipesa mingi tena ya kukopa!
Hivi utekelezaji wake mbona siuoni?
Maana tuliambiwa baada ya miezi 6 tu tutaanza kuona mabadiliko lol

Ule mpango ulikuwa wa kikanjanja tu ili bajeti ipite, maana leo hii ni inatia kinyaa tunaendelea kuahidiwa dharura.
Dharura inaahidiwa jamani? Naomba wataalamu wa BAKITA watupe tafsiri mpya ya neno dharura.

Hilo la jenereta la mkurugenzi wa Tanesco ni sehemu ya mbwembwe za hawa wenyeviti wa hizi kamati, wanabodi mmesahau mbwembwe za Mrema kwa wakurugenzi wa halmashauri.
 
Hivi Mhando akijua uchungu wa magawo atachukua pesa toka mfukoni kwake na kuziingiza TANESCO? Wanasiasa wetu wana mambo kweli siku hizi. Kila mtu anakimbilia umaarufu kwa kutoa tamko ambalo litawafurahisha wapiga kura.

kwa nini wasiseme jenereta ziondolewe kwa Waziri wa Fedha, Ikulu kwa Waziri wa nishati na madini nk.?

Umeliona hili Mkuu eeh.. Nimeshangazwa sana na kauli hiyo ya wabunge.. Kwanza wana mandate hiyo ya kuingilia mipangilio ya hw tanesco wanapeana privileges..? Au ndo yale ya taasisi na viongozi kutojua mipaka yao ya kazi..? Halafu itatatua vipi tatizo lililopo la umeme..? Kwa nini wasiseme mpaka lile la pale Ikulu litolewe nalo..? Wakati umefika sasa kwa hawa viongozi kuacha kutoa kauli za kisiasa.. political stunts hazitasaidia...
 
Sijasikia mpango endelevu bado, nilitegemea kusikia mazungumzo ya Uranium hapa. Kama hatujafikiria kuomba msaada tutumie uranium yetu bado naona tutakuwa na dharura kila mwaka.

Watz tulishangilia sana tuliposikia kuwa katika nchi yetu kuna GESI; lakini baada ya mradi wa Songosongo kuanza hakuna tofauti na ndio kwanza mgao unaongezeka. Hivyo sidhani kama Uranium itasaidia hapa zaidi ya kuleta ulaji kwa baadhi yetu madarakani.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kwa kuanzia ni uamuzi mzuri ila uendelee mpaka kwa Ngeleja,katibu wa wizara iyo,jamaa aliyeibiwa mabegi yenye madini moro hotelini.
Thereafter kama maji hayatoshi watuambie what is the way forward!
 
Zitto anaonyesha jinsi gani anakurupuka kutoa maamuzi.
Mhando si yeye alisebabisha hizo pesa sizitoke na wala hana uwezo wa kushinikiza serikali impatie hizo pesa.
Pia kumbuka huyo ni CEO wa TANESCO anazo benefits na heshima yake kama boss wa TANESCO. Angelikuwa kaweka genereta za kubwa za Tanesco kwake sawa, lakini hii kapewa kama part of his perks. Anastahili kabisa kama CEO.

Hii ni embarrasment kwa CEO na kutaka kumdhalilisha kwa manufaa yako binafsi na uzembe wa kufikilia na kuharakisha kutoa maamuzi.

Uko sahihi,tatizo halianzii hapo kwa huyo kibopa kujiwekea bali mfumo/utaratibu mzima na ufafanuzi wa maslahi benefits&fringes zinazoendana na post hiyo,tunarudi kule kule serikali ya ccm ndo mchawi ilipaswa kuona hayo! Zaidi ya hapo ni mtu/mwanasiasa kujitafutia umaarufu tu
 
TANESCO kwa visingizio hamchoki?ina maana ile bajeti ya ngeleja ilikua usanii tuu?agreko agreko inasikitisha sana!
 
shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiit, inaniuma sana kuona ****** anakenua meno tu na kuongea na wale vizee vya ccm bongo huku Tz ikiwa hoi.
 
Watz tulishangilia sana tuliposikia kuwa katika nchi yetu kuna GESI; lakini baada ya mradi wa Songosongo kuanza hakuna tofauti na ndio kwanza mgao unaongezeka. Hivyo sidhani kama Uranium itasaidia hapa zaidi ya kuleta ulaji kwa baadhi yetu madarakani.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Mkuu nakumbuka kauli iliyotoka serikalini.. Kwamba gharama za kuzalisha umeme zitapungua kwa karibu nusu.. Halafu wangesambaza gesi mpaka majumbani kwa watu.. Na wange-introduce magari ya kutumia gesi kwa ajili ya kunusuru hela nyingi za kigeni zinazotumika kununulia mafuta toka nje.. Yaani wanatufanya kama sie wote ni watoto wadogo.. Hatuna kumbukumbu..!
 
Kuna waziri mmoja wa Elimu Uingereza alifukuzwa kazi simply alimuhamisha mtoto wake kutoka shule ya SERIKALI kwenda shule ya BINAFSI. Hiyo tu ilikuwa SCANDAL ya kumuachisha kazi. Kama waziri hana imani na elimu inayotolewa na shule za serikali ambazo anazisimamia, Je atafanya jitihada ya kuboresha hiyo elimu kama mtoto wake anamuhamisha?

Hayo ndiyo ya Mhando kwamba hana uhakika na umeme wa TANESCO ambao yeye ndiye msimamizi wake mkuu. Tena wangeanda mbali kumpiga STOP hata ya kuweka generator kwa pesa yake because hiyo nyumba ni mali ya TANESCO. Kama anataka akaweka generator kwenye nyumba yake.

Lakini hawa POAC wasiishie hapa, waihoji TANESCO kwanini haikusanyi madeni yake kutoka kwa wadai wakubwa sugu kama JWTZ, ZESCO?

Mhando mtamuonea bure mtu wa watu. Nchi hii inaendeshwa kisiasa mno. Bila political will and support TANESCO haiwezi kufanya chochote wala haiwezi kuthubutu kwenda huko unakokusema ili ikadai madeni. Zitapigwa simu na mwishowe Waziri wa Nishati atampigia Mhando na kumuamru kuachana na hayo mambo ya kudai idara nyeti!

Nasema tena kwamba generator ziondolewe maofisi ya serikali: Kazi zisifanyike na posho zisilipwe. Generator ziondolewe kwenye nyumba za serikali. Generator ziondolewe Ikulu. Generator ziondolewe kwenye nyumba za mawaziri wote ili watoto wao waone adha ya kulala bila viyoyozi wawalilie baba zao na mama zao. Wake/Waume walie kwa kuwa usiku hawakulala usingizi mororo, kesho wakienda kwenye Mkutano wa Baraza la Mawaziri watakuwa wana mawazo ya kutatua tatizo la umeme. Kuondoa Generator kwa Mhando ni tamko lisilo na chembe ya tija hata kidogo.
 
Umeliona hili Mkuu eeh.. Nimeshangazwa sana na kauli hiyo ya wabunge.. Kwanza wana mandate hiyo ya kuingilia mipangilio ya hw tanesco wanapeana privileges..? Au ndo yale ya taasisi na viongozi kutojua mipaka yao ya kazi..? Halafu itatatua vipi tatizo lililopo la umeme..? Kwa nini wasiseme mpaka lile la pale Ikulu litolewe nalo..? Wakati umefika sasa kwa hawa viongozi kuacha kutoa kauli za kisiasa.. political stunts hazitasaidia...

Mkuu yaani siku hizi ni vurugu tuu! Kila mtu anatoa tamko na kukemea bila hata kujua mipaka yake. Bunge ni oversight institution sasa leo linaenda front na kutoa maagizo kwa watendaji ambao si wanasiasa. Nchi imefika pabaya. Kila mwenyekiti wa Kamati ya Bunge anadhani ni mtendaji. Wanatakiwa wakajifunze majukumu ya oversight institution kama Bunge. Waelewe governance processes.

Leo utamsikia Mwenyekiti huyu anaamuru mtu afutwe kazi mara moja. Hivi wao wana mandate ya kufuta kazi.
 
'Dunia yako, dunia yangu, chagua umeme wa uhakika........'; William ngeleja.. Waziri wa nishati na madini - tz.
 
nilishasema kuwa Zitto ana unafiki uliopitiliza. sasa ameshajua kuwa serikali haijapipa Tanesco dhamana ya kupata hizo hela za umeme.wa dharula.
kumpora Mhando genereta ndo kunasolve lipi kati ya deni la aggreko na uhaba wa maji wa Hivi tu mwenyekiti wa kamati ya bunge, akiwa raisi ndo tutaona vimbwanga
 
hivi ile kauli ya ngeleja kwamba mgao wa umeme utakua historia umeishia wapi?
 
Back
Top Bottom