TANESCO: Rationing is back!

mhando mtamuonea bure mtu wa watu. Nchi hii inaendeshwa kisiasa mno. Bila political will and support tanesco haiwezi kufanya chochote wala haiwezi kuthubutu kwenda huko unakokusema ili ikadai madeni. Zitapigwa simu na mwishowe waziri wa nishati atampigia mhando na kumuamru kuachana na hayo mambo ya kudai idara nyeti!

Nasema tena kwamba generator ziondolewe maofisi ya serikali: Kazi zisifanyike na posho zisilipwe. Generator ziondolewe kwenye nyumba za serikali. Generator ziondolewe ikulu. Generator ziondolewe kwenye nyumba za mawaziri wote ili watoto wao waone adha ya kulala bila viyoyozi wawalilie baba zao na mama zao. Wake/waume walie kwa kuwa usiku hawakulala usingizi mororo, kesho wakienda kwenye mkutano wa baraza la mawaziri watakuwa wana mawazo ya kutatua tatizo la umeme. Kuondoa generator kwa mhando ni tamko lisilo na chembe ya tija hata kidogo.
mkuu hizi ndio wanaita visioni twente twente 2020.......... Jamani sio kila jambo mnaliweka kisihasa daah wakati mwngine naingia uoga na uwezo wa wawakilishi wangu huko mjengoni ............
 
infinite solution ni kuachana na umeme wa dharura baaaaasi ... Haya mambo mengine sie pale slab tulikuwa tunayaita chai tu ......... Siasa kwenye fani za watu mbaya sana nakuonea huruma mhandisi mwenzagu mhando daah
 
Zitto anaonyesha jinsi gani anakurupuka kutoa maamuzi.
Mhando si yeye alisebabisha hizo pesa sizitoke na wala hana uwezo wa kushinikiza serikali impatie hizo pesa.
Pia kumbuka huyo ni CEO wa TANESCO anazo benefits na heshima yake kama boss wa TANESCO. Angelikuwa kaweka genereta za kubwa za Tanesco kwake sawa, lakini hii kapewa kama part of his perks. Anastahili kabisa kama CEO.

Hii ni embarrasment kwa CEO na kutaka kumdhalilisha kwa manufaa yako binafsi na uzembe wa kufikilia na kuharakisha kutoa maamuzi.

Haya ndiyo mawazo na uwezo wa Mtu anayetaka Urais kwa udi na uvumba...

Hivi anashindwa kuelewa root cause ya matatizo ya umeme ni ufisadi ambao watuhumiwa wake ndiyo wanamtumia kwa sasa kuivuruga CDM especially Rostam?
 
Yaani kwake anajivunia jenereta ambapo anajaziwa mafuta kutokana na pesa za walipa kodi
 
Zitto ni mnafki tu Hana jipya.
Actually ni ujinga wa kutupwa kumwondolea jenereta mkuu wa shirika la Tanesco maana inaelekea hiyo ni hatua ya chuki binafsi tu.
It is also a populist move with no positive effects to the whole power problem.
Waziri wa uchukuzi akaendeshe dala dala mwenyewe basi ili kupunguza tatizo la usafiri DSM
Magufuli je? ashike sululu na kujenga barabara mwenyewe
Na Waziri wa elimu akafundishe mpaka kieleweke.

Hili ndio tatizo la kuwa na wabunge wasio na solutions za nchi wala hawajui wachangie vipi kutatua matatizo yetu.

Mbaya zaidi ndio waakuwa wa kwanza kukimbilia kutaka Urais!
Je tutafika?
 
Na Zitto hana Genereta nyumbani kwake? kama angekuwa na Uchungu pia ama analo aliondoe pia
 
Maamuzi ya wabunge kuelekeza hoja yao kwa Mkurugenzi haina mshiko hata kidogo, maana huyu ni bangusilo. Niliyasema haya miaka 6 iliyopita kuhusu swala la Umeme Dar na Tanzania ya kwamba hata huo umeme wa dharura ulokusudiwa bado ulikuwa hautoshi. Na nilipinga wazo la kununua mitambo ya Dowans kwa sababu nilijua haiwezi kubadilisha kitu chochote mbali kabisa na scandal kubwa iliyotokana na mkataba mbovu..Kilichofanyika ni usanii mtupu wa JK na Lowassa kutuhadaa wananchi.

Jamani Dar inakua haraka sana, na huwezi kuboresha kitu chochote bila kuwepo msingi bora..Ujenzi wa majengo makubwa yanayohitaji nguvu kubwa ya Umeme, ongezeko kubwa la biashara na huduma mjini, hivi vyote vinahitaji umeme ambao pia unahitaji vyanzo iwe gas au generators kuongeza kiwango cha nguvu za umeme ktk grid ya taifa kulingana na maendeleo yenyewe. Hizi fikra za kuongeza ajira wakati miundo mbinu haitoshelezi mtaweza vipi kuzalisha hizo ajira na huduma za kudumu?.. Hivi kweli mnafikiria kosa ni la Tanesco? hamuoni matumizi makubwa ya umeme nchini yanavyoongezeka kupita uzalishaji wake?.

Mimi nadhani kuna tatizo ndani ya Bongo zetu, tuna mapungufu makubwa sana ya uwezo wa kufikiri kiuchumi na ndio maana reli ya kati hadi leo imelala ati nguvu kubwa inawekwa kuingiza malori nchini kama ndio usafiri wa kuaminika. Tazameni traffic barabarani yaani mtu huwezi fanya mambo mawili kwa wakati mmoja, huwezi tembelea maduka mawili sehemu mbili tofauti isipokuwa kila mmoja wetu ananunua vitu kwa machinga barabarani kwa sababu hatuna Mall sehemu ambayo mtu anaweza ku shop kwa mara moja vitu tofauti. Majimbo hayajitoshelezi kwa kila kitu na bado yanapanuka kwa kasi ambayo miundombinu ni ile ile toka tupate Uhuru..

Badala ya kumwadhibu Mkurugenzi wa Tanesco, mimi ningeshauri - Makao makuu yahamie Dodoma, tuondoe vurugu za viongozi wenyewe kwanza Dar na wabunge wote rudini majimboni kwenu na muishi na wananchi mnao wawakilisha nanyi mlijue joto la jiwe..kwa nini nyote mna makazi Dar tuu?..Kila mbunge anayeingia madarakani lazima atafute nyumba Dar acha wale waliotangulia..Huko kwenu mnakowakilisha hamtaki kuishi kwa nini..
 
Tunapoongelea suala la TANESCO inabidi tukae na tutafakari kwa kina kuhusu haya tunayoongea na implications zake kwetu sote kama Wananchi. Uhusiano wa TANESCO na Serikali ni ule wa Baba na Mwana! TANESCO hawezi kufanya kitu chochote pasipo kumshirikisha baba yake ambaye ni Serikali, na ni Serikali kupitia kwa mdogo wake Wizara ya Nishati na Madini. Na TANESCO inawajibika moja kwa moja huko. Sasa kama Serikali haimruhusu kufanya maamuzi yake peke yake unategemea kitakachofuatia ni nini? Suala la umeme wa TANZANIA halijaanza leo kuwa na matatizo, limeanza mbali sana kwenye historia ya nchi yetu.TANESCO ni shirika ambalo lina wataalamu wengi sana, lina engineers wa kutosha, lakini hawapewi nafasi ya kujiendesha wenyewe kama lenyewe, Siasa na pressures za wanasiasa ni nyingi sana, na hayo muheshimiwa mwenyekiti wa kamati Zitto Kabwe anayozungumza ni propaganda tu kwa sababu ukweli halisi anaufahamu, na mimi binafsi sioni msingi wake haswa. TANESCO hawawezi kufanya makubaliano yoyote au kusaini mkataba wowote,bila kuishirikisha serikali. Na ni serikali hiyo hiyo leo ndio inaibana TANESCO kwa mambo ambayo wao wenyewe ndio chanzo cha yote hayo, wapi na wapi?Suala la jenereta la CEO wa TANESCO, ni incentive ambayo amepewa yeye akiwa kama mkuu wa kampuni, akiambiwa achukuliwe jenereta ili aone makali ya mgao wa umeme mimi binafsi nachukulia kama manyanyaso na masimango, i don not expect kuwa hana uwezo wa kununua standby generator yake mwenyewe kwa pesa zake endapo zipo hata kariakoo kwa bei nafuu tu. Nadhani kama ni ukali wa mgao uanzie kwa watendaji wakuu wa Serikali, na ofisi zake ndio ishuke chini mpaka kwa CEO...Zaidi sana inawezekana kuna watu wanaona anafaidi sana, so ni chuki tu, maana kusema ili na yeye aone uchungu, so much of hating...Cha msingi ni Serikali kuchukua wataalamu na kukaa na kuzungumza nao na kuwasikiliza na kufuata ushauri wa kitaalamu and not just some other person ambaye hata sio mtaalamu wa umeme ndio ambaye anatoa ushauri na kutoa maagizo. Je, wataalamu wanasemaje? Wenzetu nchi zingine wanathamini sana ushauri wa wataalamu wao na wanawasikiliza, and then ndo wanaproceed na mambo mengine. Kusema sijui generator lifanyweje doesnt solve anything.Naomba kuwasilisha
 
Analo lakini halilipiwi kwa kodi zetu kama la Mhando mkuu!

Mkuu linalolipiwa na kodi zetu liko magogoni kule.. La Mhando linalipiwa na Tanesco ambayo inafanya biashara ya umeme japo kwa hasara.. Na usisahau ni moja ya incentives kwa cheo cha CEO.. La Zitto kama analo ndilo linalolipiwa kwa kodi zetu.. Maana hata kama anatoa yeye hela mfukoni lakini unatokana na mshahara wake ambao kwa kazi yake ambayo haiingizi faida inabidi agharamiwe na kodi zetu..
 
Hii nami naunga mkono kwani wanatuchezea na huu umeme utafikiri kuwa na umeme ni fadhila bana..




Monday, 26 March 2012 20:23
lizimwe.jpg
Mkungenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando (katikati), akiwa na baadhi ya maofisa wa shirika hilo wakiwasiliana kuhusu kurekebisha ripoti kabla ya kuingia katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) jijini Dar es Salaam jana. Picha na Fidelis Felix

Boniface Meena


KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma(POAC), imeagiza Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuondoa jenereta la dharura lililopo nyumbani kwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, William Mhando kuanzia leo ili naye ajue machungu ya kukatika umeme mara kwa mara.

Wakati POAC ikiagiza kuondolewa kwa jenereta hilo, taarifa zinaeleza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Jenerali Mstaafu, Robert Mboma amemwandikia Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja akihoji sababu za kutokutekelezwa kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete la kulipatia shirika hilo kiasi cha Sh408 bilioni kwa ajili ya kujiendesha.
Barua ya Mboma ya Machi 20, mwaka huu kwenda kwa Ngeleja, ambayo gazeti hili imefanikiwa kuiona, ilisema mnamo Machi, 8 mwaka huu, Rais Kikwete aliagiza Tanesco ipewe haraka mkopo huo wa Sh408 bilioni lakini akasema hadi sasa amri hiyo ya Amiri Jeshi Mkuu haijatimizwa.

“Mheshimiwa Rais tarehe 8 Machi aliagiza kuwa mkopo huo wa Sh408 bilioni upatikane haraka. Lakini, sisi tunazunguka na hivyo kushindwa kutii amri ya Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania. Katika hali ya kawaida, tunatakiwa tufanyekazi usiku na mchana kwa nia ya kukamilisha maagizo halali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano," inasema sehemu ya barua hiyo ya Mboma.

Katika sehemu nyingine ya barua hiyo, Mboma alisisitiza: "Hali ya mabwawa yanayotegemewa ya Mtera na Nyumba ya Mungu ni mbaya sana. Ukosefu wa mafuta utatulazimu tutumie maji hayo... hii maana yake ni kuwa mwakani tutalazimika kukodi mitambo mingine ya dharura kwa sababu mitambo ya sasa, muda wake utakuwa umekwisha. Watanzania hawatatuelewa na Tanesco italaumiwa bure kwa sababu tuko ambao hatutii amri za ngazi za juu."

Mboma katika kuhakikisha agizo hilo la Rais linatekelezwa, aliomba kikao kati yake na Waziri Ngeleja, Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, wajumbe wawili wa bodi, menejimenti ya shirika hilo na wajumbe wengine ambao waziri huyo angeona wanafaa.

“Lengo liwe ni kutafuta njia za kufanya ili turekebishe kasoro. Wakati huohuo; napendekeza Katibu Mkuu wetu azungumze na mwenzake wa Hazina. Hii iwe baada ya menejimenti ya Tanesco kumjulisha juu ya mazungumzo yao,” ilisisitiza barua hiyo na kuongeza:

“Itapendeza kama Katibu Mkuu (WNM) atakuwa amezungumza na mwenzake wa Hazina kabla ya kikao chetu. Baada ya hapo, naona tuone jinsi ya kuzungumza na mheshimiwa Rais. Suala hili ni zito."

Nakala ya barua hiyo ilipelekwa pia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Ofisi ya Rais, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu Nishati na Madini, Msajili Hazina na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco.

Msimamo wa POAC

Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe akizungumzia suala la jenereta alisema ni lazima liondolewe kwa kuwa linatumia mafuta ya Serikali na ndiyo maana mkurugenzi huyo hawezi kujua adha iliyopo kwa wananchi pindi umeme unapokatika.

“Tumemtaka Jenerali Mboma afanye hivyo kwa kuwa haiwezekani mkurugenzi wa huyo awekewe jenereta kwani kwa kufanya hivyo inadhihirisha kwamba hawana umeme wa uhakika,” alisema.

Zitto alisema wameagiza hilo lifanyike haraka na kama mkurugenzi huyo anataka kuwa na jenereta anunue la kwake binafsi na si kutumia la umma na mafuta ya Serikali.

Alisema Tanesco imeendelea kuelemewa na mzigo wa kununua umeme kutoka makampuni binafsi na imepata hasara ya Sh47 bilioni kutoka Sh43 bilioni mwaka 2009.

Zitto alisemza mwaka 2010, Tanesco ilitumia kiasi cha Sh211 bilioni kununua umeme wa dharura kutoka kampuni binafsi na asilimia 90 ya fedha hizo zimetumika kwa Songas na IPTL… “Songas wametumia kiasi cha Sh127 bilioni na Sh64 bilioni zimetumika kwa IPTL.”
Alisema kutokana na hali hiyo wameitaka Tanesco kuanzia Mei mwaka huu, waache kutumia mitambo ya IPTL baada ya mtambo wao mpya wa Jacobsen unaojengwa Ubungo, Dar es Salaam kuanza kufanya kazi na kuzalisha megawati 100.

Zitto alisema hivi sasa Tanesco wamepunguza gharama za uendeshaji lakini wanatumia Sh499 bilioni kuzalisha na umeme ambao wakiuza wanapata Sh466 bilioni na ukiongeza gharama nyingine za mishahara unakuta wanapata hasara ya Sh47 bilioni kila mwaka.

Kuhusu kuwepo kwa mgawo wa umeme Zitto alisema Tanesco imekubali kuwa kuna mgawo usio rasmi na hiyo inatokana na kukosa dhamana kutoka serikalini ya kupata mkopo wa Sh408 bilioni ili iweze kununua umeme wa dharura na kuondokana na tatizo la umeme.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alisema hali ndani ya shirika hilo ni mbaya kwa sababu haina fedha za kuliendesha na kwamba hawawezi kununua vipuri.

Alisema kutokana na hali hiyo umeme unaokatikakatika ni mgawo lakini shirika hilo limekuwa likikanusha kwa sababu uwezo limekuwa likipokea malalamiko mengi yanayohusu ukatikaji huo hasa Dar es Salaam.

“Hali ya mabwawa kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Jenerali Mboma inaeleza kuwa ni mbaya kwani Mtera lina mita 1.24 tu juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa na sasa bado mita 5.26 kufikia kima chake cha juu,” alisema Zitto na kuongeza:

“Nyumba ya Mungu ina mita 3.22 juu ya kina cha chini kinachoruhusiwa na ni mita 9.76 kufikia kina cha juu cha bwawa hilo hivyo maji kwenye mabwawa hayo ni kidogo hasa kama mvua haitanyesha maeneo ya Mbeya Dodoma, Arusha Kilimanjaro, Singida na Tanga.”

Alisema ukosefu wa fedha za kununulia mafuta utalazimu watumie maji hayo kidogo ili wasifanye mgawo wa umeme na hiyo maana yake ni kuwa mwakani watalazimika kukodi mitambo mingine ya dharura kwa sababu ya sasa muda wake utakuwa umekwisha.

Zitto alisema kutokana na hali hiyo, wamemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kushughulikia suala hilo ili fedha hizo zipatikane.

“Mtambo wa Aggeko umezimwa na IPTL pia ambayo yote kwa ujumla huzalisha megawati 150,” alisema.

Awali, kabla ya kuhojiwa na POAC Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi William Mhando alisema tatizo la umeme katika Mkoa wa Dar es Salaam litakwisha baada ya wiki nne kwa kuwa wahandisi wa shirika hilo wanafanyia kazi matatizo yaliyopo.Alisema kukatika umeme mara kwa mara hasa maeneo ya Mbagala, Temeke na Kigamboni kunatokana na mfumo wa umeme uliopo kuchakaa na ili kutatua tatizo hilo wameagiza transfoma nne za dharura.

“Hali ya umeme si mbaya tunamudu mahitaji kwa kutumia maji japokuwa si mengi na pia tunatumia gesi. Mifumo yetu ya umeme si mizuri kwa kuwa imechakaa,” alisema Mhando.
 
Analo lakini halilipiwi kwa kodi zetu kama la Mhando mkuu!

Wabunge wetu badala ya kudeal na cross cutting issues za energy policy na implementation yake wnaanza kudeal na petty issues za kupoteza muda wao wa kufikiri!
This must stop maana Mhando and co. wakipewa jenereta na kulipiwa na kodi zetu so what!
Tumewaajiri ili wafanye kazi usiku na mchana, ili tuio gizani tuondokane na tatizo hilo.
Ukiona mwana siasa anaanza kushughulikia petty issues basi huyo hatufai katika kushughulikia matatizo ya kitaifa.
 
Jenerata lenyewe huwa ni kama mzigo kwa sababu lain anayokaa jamaa huwa umeme haukatiki ni kma ikulu kwa hiyo bado siyo suluhisho la tatizo la mgawo wa umeme kwa watz
 
Kama ninavyoona Genereta la Zitto Kable na la Mkurugenzi wa Tanesco yoote yanawaumiza walipa kodi masikini nchini

Sababu Zitto Mshahara wake na Marupurupu yoote yanatokana na Walipakodi Sawa na huyo Mkurugenzi...

Kama ni Mimi natoa Uamuzi woote wasingetumia Genereta; Hivyo kungeongeza Ufanisi na Uvumbuzi wa kutatulia Tatizo la

Umeme haraka iwezekanavyo...
 
Sawa kabisa, sasa hawa wabunge wasiishie hapo. Kila waziri au mbunge atumie huduma za sekta anayosimamia. Kwa mfano waziri wa afya atibiwe Muhimbili na siyo Ulaya, waziri wa elimu asomeshe watoto wake katika shule anazozisimamia na siyo za seminari au zilizoko nje ya nchi, mgawo wa umeme uwe kwa viongozi wote na usiishie kwa mkurugenzi wa TANESCO tu; hapa naona wabunge wamejichagulia mbuzi wa kafara. Huenda viongozi wakiupata uchungu wa uzembe unaofanyika katika maeneo wanayoyasimamia akili zitawarudia na wataanza kufanya kazi badala ya kufikiria kuzurura na kuiingiza nchi kwenye mikataba mibovu.
Je, wabunge wetu wanaiweza hii kazi?
 
hizo hela bilion 280 zingetosha kujengea mabwawa
hata matatu madogo ya kuzalisha hata megawati 80 kwa kila moja
nchi inaongozwa na vilaza wote. upuuzi mtupu
bora hiyo wizara ibinafsishwe tujue moja,
 
Back
Top Bottom