Tamthiliya ya Zahanati ya kijiji. Nimeamini Tanzania kuna vipaji vya waigizaji aisee kiukweli wamefanya kazi kubwa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,038
18,014
Sikuwahi kuwa mpenzi wa movie za kibongo au series za kibongo ila hii ilikuwa ni series ya moto sana

Nimeamini Tanzania kuna vipaji vya waigizaji aisee kiukweli wamefanya kazi kubwa

Nilikuwa namkuta wife akifatilia hii series mwanzoni nikaona matani ila kiukweli hii series daaah

Imevaa uhusika kwa kitanzania kabisa zile blah blah za Bongo movie tulizozoea kuona humu hamna!!

Nilikuwa na mentality ya kuamini kuwa za nje ndo poa ila to be honest hii series ilikua noma na ya moto sana

Wamefanya kazi kubwa sana nadhani hii ndo series bora ya mwaka wanastahili tuzo hawa watu
 
Niliiangalia kwa kujificha sana ili wanaume wenzangu wasijue nafatilia filam za wamama ila nakiri ilikua Kali sana
Nashukuru Mungu hakuna alienishtukia Kama nilikua nafatilia
Hahahaha mkuu usiishi kwa kuogopa watu ilimradi unachofanya ni sahihi huvunji sheria za nchi na wala hufanyi machukizo mbele za Mungu kumbuka hata kufa kaburini utaenda mwenyewe hao washkaji zako hawatokusindikiza huko
 
Mimi ni mvivu kuangalia movie yoyote ile iwe ya bongo au Nje, Ila siku Moja nilikuwa, kwa bro mara gafla naona muda wote kuanzia bro, wife na, watoto wametulia utadhani wimbo wa Taifa unaimbwa kwa dharura.

Kumbe muda wa movie ilikuwa startimes inaitwa Brothers, aisee nilishangaa sana.

Mimi napenda kusoma vitabu zaidi..

Ila, Haya maisha kila mtu Ana chaguo lake
 
Ngoja niuanze mchakato,ila kila ijumaa watakuwa wananikosa, ni siku ya kunywa bia
Nalog off
 
Back
Top Bottom