Tamko la mtandao wa wanafunzi nchini "tsnp" na university of dar es salaam human right association .

Aug 31, 2011
35
27
WAZIRI PINDA APEWA SIKU SABA ATOE RIPOTI YA TUME YA KUCHUNGUZA UFELI WA KIDATO CHA NNE CHA MWAKA JANA.

kuna tamko ambalo mtandao wa wanafunzi nchini "TSNP" wAKISHIRIKIANA na uNIVERSITY OF DAR ES SALAAM human right Association "UDHRA" Walilitoa hapo jana tareh 15 november 2013. tamko hili lilisomwa na Mkurugenzi wa TSNP, Ndugu Alphonce Lusako. WADAU WA ELIMU. NI MUDA WA KUCHAMBUA KIUNDANI TAMKO HUSIKA. tunaomba kama mnamaoni au mnaunga mkono hoja hii. TUSHIRIKIANE KWA HATUA ZITAZOFUTA.

tamko husika.

TAMKO LA MTANDAO WA WANAFUNZI NCHINI “TSNP” NA UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM HUMAN RIGHT ASSOCIATION “UDHRA”. KUMTAKA WAZIRI MKUU “ MH. MIZENGO PINDA” ATOE HADHARANI, RIPOTI YA TUME YA KUCHUNGUZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE ALIYOIUNDA MWAKA JANA.

Ndugu waandishi wa habari:

Pamoja na juhudi zote zinazofanywa na serikali katika kuimarisha elimu ndani ya taifa letu, tunapenda kutoa masikitiko yetu, mbele ya watanzania juu ya uwepo wa janga la kitaifa katika sekta ya elimu kwa muda mrefu sasa. Lakini pia kwa niaba ya watanzania na wadau wa elimu waliowengi tunasikitishwa na usiri wa tume ya kuchunguza matokeo ya kidato cha nne iliyoundwa na waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda na iliyoongozwa na profesa Mchome, mwanzoni mwa mwaka huu,{machi-june}

Ikimbukwe kwamba, mda huu tunavyoongea, wadogo zetu wa kidato cha nne wapo kwenye mitihani yao ya mwisho lakini bado tume iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza madhaifu ya mitihani ya kidato cha nne mwaka uliopita bado imekuwa ni siri ya tume na waziri mkuu.
Ikumbukwe, matokeo ya mwaka jana ya kidato cha nne, yalionyesha kuwa watahiniwa 60.6% walipata sifuri, watahiniwa 5.16% ndio waliofaulu na wengine 26.02% wakiwa wamepata daraja la nne katika mtihani huo. wakati wanafunzi wa shule walikuwa 397,136 na 68,806 walikuwa wanafunzi wa kujitegemea.

Kutokana na hali husika, wananchi na wadau mbali mbali wa elimu katika taifa hili walitaka kuandamana nchi nzima kumtaka waziri wa elimu na viongozi mbali mbali wa sekta hii kujiuzulu. Ndipo Mh. Mizengo Pinda akacheza kete ya kuunda tume ya kuchunguza matokeo ya kidato cha nne, iliyoanza kufanya kazi kuanzia machi hadi june mwaka huu, ili kupooza hatua za makusudi za wananchi na wadau wa elimu walizotaka kuzichukua kwa wakati huo. Wadau wa elimu kwa kuheshimu na kuiamini kauli ya waziri mkuu, walisitisha mikakati yao na kusubiri majibu ya tume ambayo mpaka hivi sasa tume husika imeingia mitini, na haijatoa majibu yake hadharani.

MAUDHUI.

Kwa sababu tume ilishafanya kazi yake ya uchunguzi, mnamo tarehe 15 june mwaka huu ilikabidhi ripoti ya tume husika kwa Waziri Mkuu.

1. Tunamtaka waziri mkuu, Mh. Mizengo Pinda. ndani ya wiki moja, atoe ripoti ya tume hadharani. Juu ya madhaifu yaliyopatikana, wakina nani wamehusika na madhaifu husika, mapendekezo ya tume husika ili yasijirudie tena kwa wadogo zetu wa kidato cha nne, wanaofanya mitihani yao sasa

2. Tunaitaka tume husika, iliyoongozwa na profesa Mchome, aliyekuwa katibu mtendaji wa taasisi ya vyuo vikuu Tanzania “TCU” ambaye kwa sasa amepandishwa cheo kuwa katibu mkuu wa wizara ya elimu. Ijitokeze hadharani naitoe ripoti husika kwa watanzania.

3. Tunawataka viongozi wa taasisi zifuatazo: taasisi ya elimu Tanzania {TET}, Baraza la mitihani Tanzania {BAMITA}, Wakaguzi wa shule {wizara}, ambao kwa mda mrefu wanatupiwa lawama, kwa madhaifu ya kiutendaji. Wajipime kama wanasifa za kuendelea kushikilia nafasi zao.

4. Tumesikitishwa sana na mkanganyiko uliojitokeza hivi karibuni, juu ya uwepo wa division “ 0” na divisheni “5”. Kati ya katibu mkuu wa wizara ya elimu Prof. Mchome na naibu waziri wa elimu Mh. Philipo mlugo. Hasa katika wakati huu ambao wadogo zetu wa kidato cha nne wanafanya mitihani yao ya mwisho.

Badala ya wizara ya elimu, kujikita kuondokana na umahututi wa mfumo wa elimu ndani ya taifa letu, na kuweka mfumo bora wa elimu, utaowatoa watanzania katika giza nene walilo nalo, utaowafundisha watanzania stadi za maisha. Wizara inaongelea mambo ya divisheni “5”. Ni hatari sana watanzania.

MAADHIMIO YETU.

Endapo waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda, hatatoa ripoti yake ndani ya wiki moja tuliompa, na pia endapo tume iliyoongozwa na prof. Mchome, haitatoa ripoti hadharani. Tutachukua jukumu la kuwaunganisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini, asasi zisizo za kiserikali, wadau mbali mbali wa elimu, vyama vya siasa, wazazi na watanzania kwa ujumla wake ambao wameugua na umahututi wa mfumo wetu wa elimu, kufanya maamuzi ili kunusuru elimu ya nchi yetu

HITIMISHO.

Historia inatukumbusha kuwa, tume nyingi huundwa, hutumia kodi za watanzania lakini hazitoi majibu ya tume husika. Mfano tume iliyoundwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. J. Kikwete, iliyoongozwa na Prof. Maboko, ambaye ni naibu makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam. Ili kuchunguza matatizo ya bodi ya mikopo,mpaka leo, imekuwa siri ya tume yenyewe.

Watanzania, Itikadi yetu ni utanzania kwanza, suala la mabadiliko ya elimu, si suala la serikali peke yake, si suala la kuwaachia wanasiasa peke yao, ni suala la watanzania kwa ujumla wake. Hivyo tunawaombeni watanzania tushirikiane kwa hili. Elimu itabadilishwa na watanzania na pia elimu itauwawa na watanzania.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.

BY alphonce Lusako
mkurugenzi wa mtandao wa wanafunzi nchini
TSNP "TANZANIA STUDENTS NETWORKING PROGRAMME.
 
Wana hoja wasikilizwe,kuna umuhimu gan wakuunda tume then majibu hayatolewi?,tumwamini waziri au Katibu mkuu wa elimu?,kuna uwezekano form 5 wa mwakan wakawa hawajui kuandika tusubil tuone,naona harufu ya uchakachuz wa matokeo kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea Tanzania

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom