Nyamesocho
JF-Expert Member
- May 5, 2023
- 476
- 1,244
Ni janga la wanafunzi kuacha shule, sijui kama Serikali inalijua hili
Wakati nchi nyingi duniani zinahakikisha wananchi na watoto wote wanapata elimu bila kumuacha hata mmoja ili kukabiliana na maendeleo ya sayansi na teknolojia hali ni tofauti nchini Tanzania.
Watoto wanaoandikishwa kuanza shule huwa ni wengi mfano shule X inaweza kuandikisha wanafunzi 120 wanaoanza darasa la kwanza lakini watakao hitimu darasa la saba ni 60,wanafunzi wengine 60 hawajulikani walipo ,imagin hapo ni shule moja je vipi hali ya nchi nzima?
Achana na shule za msingi tunakuja secondary zetu za kata,shule X ilipokea wanafunzi 200 kuanza kidato cha kwanza lakini watakaofanya mtihani wa Taifa kidato cha nne ni 80,je hao 120 wameenda wapi?
Kwa sasa kuna kasi sana ya wanafunzi kuacha shule kuanzia msingi mpaka sekondari,je profesa Mkenda analijua hili?
Cha ajabu zaidi watoto wa kiume wanaongoza kuacha shule,kusoma wameachiwa watoto wa kike!
Tutakuja kuwa na Taifa la kipekee duniani,Taifa la kijima la watu wasio na elimu?