Tamko la CHADEMA kuhusu Mabomu ya Gongo la Mboto

Ukisikia viongozi hawana dira ndio hawa ,yaani baada ya kuitisha uchunguzi unakurupuka na kusema nani na nani wajiuzulu,basi huyo msemaji nae ajiuzulu ,wacheni uhuni,yaani unarukia watu wajiuzulu wakati hujui ni nini chanzo cha tukio.

Wandugu mkisikia watu wanajiuzulu huko majuu msifikiri wanakurupuka tu na kuachia ngazi kuna stage mbalimbali hupitwa na ndio kufikia ni nani wa kujiuzulu.

Mi nilifikiri katika taarifa hiyo CDM wamefanya uchunguzi na kugundua chanzo na sababu ni ya wakuu flaniflani ,kumbe hamna kitu ni mazungumzo baada ya habari.
Kwa ufupi tahadharini na habari za mitaani na kuzivalia njuga ,mtakuja kuumbuka baadae,embu wekeni kitengo cha uchunguzi na muwe mnazifanyia uchunguzi habari kabla hamjazitilia ubavu, yaani mkiulizwa suali la papo kwa papo kwa nini hao wajiuzulu sijui mtajibu dudu gani ? Zaidi mtasema ni uzembe ,mkiulizwa uzembe gani mtaanza kutafuna kucha.
WaCDM wacheni hizo karata za magarasa tumieni turufu ,natumai nimeeleweka.
 
Sawa tamko zuri, lakini experience inaonyesha huwa hawajiuzuru kwa kuwaambia! guys let go to the streets, source iwe mabomu lakini impact yake iwe kuiondoa CCM yoote madarakani, we have many reasons now!
 
MAAFA YA GONGO LA MBOTO: WAZIRI WA ULINZI NA MKUU WA MAJESHI WAJIBIKE!

TAARIFA KWA UMMA
DODOMA, FEBRUARI 17, 2011

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeeleza kushtushwa na kusikitishwa na taarifa za milipuko ya mabomu katika Ghala la Kuhifadhi Silaha la Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika eneo la Gongo la Mboto, Dar es Salaam jana jioni.

Aidha, kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imewapa pole ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote wa Tanzania kwa sababu ya maafa haya. Pia Kambi hiyo imezitaka mamlaka zote za umma zinazohusika kuchukua hatua za haraka kuhakikisha wananchi wote walioathirika na maafa haya wanapatiwa huduma zote wanazohitaji katika kipindi hiki cha msiba huu. Hii ni pamoja na kuwapatia huduma za maziko wale wote waliofariki, matibabu kwa waliojeruhiwa na hifadhi kwa wale waliopoteza makazi yao. Aidha, ni muhimu kwa vyombo vya usalama kuhakikisha ulinzi wa mali za wananchi katika maeneo yote yaliyoathirika na ambazo zitakuwa hazina ulinzi baada ya wananchi kukimbia maeneo yao.

Taarifa ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeeleza kwamba tukio hili ni la kushtusha na kusikitisha hasa kwa kuzingatia kwamba haijapita miaka miwili tangu tukio la aina hiyo hiyo litokee katika Ghala ya Silaha ya Kambi nyingine ya JWTZ katika eneo la Mbagala, Dar es Salaam, ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu thelathini na uharibifu mkubwa wa mali za umma na za wananchi binafsi. Aidha, milipuko ya Mbagala ilipelekea Serikali kutumia mabilioni ya fedha za umma kwa ajili ya malipo ya fidia kutokana na vifo, majeruhi na uharibifu wa mali binafsi za wananchi.

Akielezea tukio la milipuko ya Gongo la Mboto, Msemaji wa Ulinzi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh. Joseph Selasini alisema: "Milipuko ya Gongo la Mboto inaonyesha dhahiri kwamba Serikali ya Awamu ya Nne ya Chama cha Mapinduzi (CCM) haijajifunza lolote kutokana na maafa yaliyotokea Mbagala mwaka juzi. Maana kama Serikali ingejifunza kutokana na maafa hayo ingeshachukua hatua za dharura na za haraka kuhakikisha kwamba maafa ya aina hii hayatokei tena." Mh. Selasini alizitaja baadhi ya hatua hizo kama ni pamoja na kuhamisha maghala yote ya silaha na mabomu yaliyo karibu na maeneo wanayoishi raia na kuyapeleka katika Kambi za JWTZ zilizoko mbali kabisa na maeneo ya raia. "Haiwezekani kwa Serikali kuendelea kuweka maghala ya silaha katika Kambi za Jeshi zilizo karibu na wananchi na hivyo kuhatarisha maisha yao namna hii", alisema Mh. Selasini.

Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imewataka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kujiuzulu mara moja ili kuwajibika kisiasa kutokana na maafa ya Gongo la Mboto na ili kupisha uchunguzi huru na wa kina wa chanzo na/au sababu za milipuko hiyo. Mh. Selasini alisema: "Dr. Hussein Mwinyi alikuwa Waziri wa Ulinzi wakati wa maafa ya Mbagala; na Jenerali Mwamunyange alikuwa Mkuu wa Majeshi. Maafa ya Mbagala yalitokea chini ya dhamana na/au usimamizi wao. Na mara baada ya maafa hayo, Waziri Mwinyi na Jenerali Mwamunyange waliliahidi taifa kwamba maafa ya aina hii hayatatokea tena. Sasa yametokea. Inaelekea, kwa hiyo, kwamba ahadi yao ilikuwa sio ya kweli na/au hawakuhakikisha kwamba inafanyiwa kazi ili iwe ya kweli. Viongozi hawa hawana budi kuwajibika kwa hiari yao wenyewe au kuwajibishwa kama itahitajika."

Mh. Selasini aliongeza kusema kwamba hadi leo hakuna taarifa yoyote rasmi iliyowahi kutolewa hadharani kwa wananchi na/au kwa wawakilishi wao Bungeni ya chanzo na/au sababu za maafa hayo. "Hadi leo hii wananchi na/au wawakilishi wao Bungeni hawajaambiwa kama kulikuwa na makosa ya makusudi na/au ya uzembe na/au kama hatua zozote za kinidhamu na/au za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya mtu yeyote kutokana na kusababisha na/au kuwajibika kwa maafa hayo. Jana maafa mengine ya aina hiyo hiyo yametokea tena na kwa kadri ya taarifa rasmi ya Serikali watu wengi wameuawa na wengi wengine kujeruhiwa na mali nyingi kuharibiwa. Kwa sababu hizo, huu ni wakati muafaka kwa Dr. Mwinyi na Jenerali Mwamunyange kuonyesha uadilifu wao kwa kujiuzulu nafasi zao ili kuwajibika kwa maafa haya."

Mwisho, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imependekeza iundwe Tume Huru ya Uchunguzi na/au Kamati Teule ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuchunguza kwa kina chanzo, sababu na madhara yote yaliyosababishwa na milipuko ya Gongo la Mboto. "Kwa kuzingatia historia ya uchunguzi wa milipuko iliyotokea Mbagala mwezi Aprili 2009, Tume Huru na/au Kamati Teule ya Bunge lazima itoe taarifa yake hadharani kwa kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", alishauri Mh. Selasini.

Hili halihitaji mjadala ni kuwajibika tu basi. Rais mstaafu Ndugu yetu mwenzetu na mpendwa wetu aAlhaj Ali Hassan Mwinyi baba yake mzazi Mh. Hussein Mwinyi alijiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani kwa kuuawa kwa watu 14 tu yeye akiwa Waziri. Lakini huyu mtoto sasa ni takribani watu 50 na bado anapeperusha Bendera ya Taifa!!. Tafadhali ndugu Hussein achia ngazi Watanzania tunakwisha.
 
Hivi jamani...hizi ghala zenye mabomu makubwa ya kivita zinafanya nini DSM??? Kweli sijaelewa kabisa... kambi nyingi za jeshi ziko porini..inakuwaje mnaweza ghala za mabomu mjini???? au ni kwa ajili ya waandamanaji??
 
kulikuwa na uchunguzi uliofanywa kuhusu mabomu ya mbagala. ripoti alipewa mwinyi akaifanya siri na nadhani hadi sasa wala bunge halijui ripoti hiyo ilisema nini. ndio utawala bora tulionao bongo. tutalalamika na kusahau dowans, mgao wa umeme na 2015 watapeta tena. kujiuzuru sio rais kwa serikali ya kikwete. taarifa zita chakachukiwa na vyombo vyetu vya habari ndio hivyo vilivyo. maisha yanaedelea.

macinkus
 
Ukisikia viongozi hawana dira ndio hawa ,yaani baada ya kuitisha uchunguzi unakurupuka na kusema nani na nani wajiuzulu,basi huyo msemaji nae ajiuzulu ,wacheni uhuni,yaani unarukia watu wajiuzulu wakati hujui ni nini chanzo cha tukio.

Wandugu mkisikia watu wanajiuzulu huko majuu msifikiri wanakurupuka tu na kuachia ngazi kuna stage mbalimbali hupitwa na ndio kufikia ni nani wa kujiuzulu.

Mi nilifikiri katika taarifa hiyo CDM wamefanya uchunguzi na kugundua chanzo na sababu ni ya wakuu flaniflani ,kumbe hamna kitu ni mazungumzo baada ya habari.
Kwa ufupi tahadharini na habari za mitaani na kuzivalia njuga ,mtakuja kuumbuka baadae,embu wekeni kitengo cha uchunguzi na muwe mnazifanyia uchunguzi habari kabla hamjazitilia ubavu, yaani mkiulizwa suali la papo kwa papo kwa nini hao wajiuzulu sijui mtajibu dudu gani ? Zaidi mtasema ni uzembe ,mkiulizwa uzembe gani mtaanza kutafuna kucha.
WaCDM wacheni hizo karata za magarasa tumieni turufu ,natumai nimeeleweka.
hv WANASIASA WOOTE WAJINGA KAMA WEWE!??
PUMBAVU WANASIASA NA WASHABIKI WAKE KAMA WEWE!
 
Nawapa pole nyingi sana Watanzania wote na pia watu wa Gongo la Mboto kwa maafa haya makubwa yaliyoleta mshtuko kwa taifa.Waliokufa Mungu awarehemu na majeruhi awape nafuu kwa mapenzi yake yeye Mungu.
 
Mh..Gurudumu, hebu toa mawazo yako..wewe unafikiri Chadema wafanye nini??

wanaweza kufanya mambo kadhaa kwa kuanzia.

1. kusaidia wahanga kushitaki serikali kwa uzembe. Hata wale wa mbagala walidhulumiwa na Lukuvi hakuna mtu aliyewatetea.

2. Kuzungusha petition wananchi wasaini kulitaka bunge kupitisha azimio la wahusika kujiuzulu

3. Kushirikiana na wananchi wa maeneo husika kukusanya taarifa sahihi za tukio zima. Kumbuka kilichotokea mbagala taarifa zilichakachuliwa hadi wahanga wakakosa haki

4............
5.............
6........

unaweza kuendeleza orodha kuwashauri wafanye nini. vitendo siyo tamko tu na kutulia. tumechoka na matamko
 
Ukisikia viongozi hawana dira ndio hawa ,yaani baada ya kuitisha uchunguzi unakurupuka na kusema nani na nani wajiuzulu,basi huyo msemaji nae ajiuzulu ,wacheni uhuni,yaani unarukia watu wajiuzulu wakati hujui ni nini chanzo cha tukio.

Wandugu mkisikia watu wanajiuzulu huko majuu msifikiri wanakurupuka tu na kuachia ngazi kuna stage mbalimbali hupitwa na ndio kufikia ni nani wa kujiuzulu.

Mi nilifikiri katika taarifa hiyo CDM wamefanya uchunguzi na kugundua chanzo na sababu ni ya wakuu flaniflani ,kumbe hamna kitu ni mazungumzo baada ya habari.
Kwa ufupi tahadharini na habari za mitaani na kuzivalia njuga ,mtakuja kuumbuka baadae,embu wekeni kitengo cha uchunguzi na muwe mnazifanyia uchunguzi habari kabla hamjazitilia ubavu, yaani mkiulizwa suali la papo kwa papo kwa nini hao wajiuzulu sijui mtajibu dudu gani ? Zaidi mtasema ni uzembe ,mkiulizwa uzembe gani mtaanza kutafuna kucha.
WaCDM wacheni hizo karata za magarasa tumieni turufu ,natumai nimeeleweka.

Acha upupu wewe! Unataka sababu gani zaidi ya hizo zilizotajwa?

Wakati wa maafa ya Mbagala Waziri wa ulinzi na Mkuu wa majeshi walishajinadi kuwa janga kama hilo halitatokea tena, lakini haijapita hata miaka miwili limetokea. Huoni kuwa hiyo pia ni moja ya sababu? Au utueleze unataka sababu gani?
 
Hivi jamani...hizi ghala zenye mabomu makubwa ya kivita zinafanya nini DSM??? Kweli sijaelewa kabisa... kambi nyingi za jeshi ziko porini..inakuwaje mnaweza ghala za mabomu mjini???? au ni kwa ajili ya waandamanaji??

wanajeshi wetu wa ngazi za juu hawataki kukaa porini, wanataka kukaa oysterbay na masaki kisha waende kazini asubuhi kama waziri anavyofanya. hili ndilo lililotufikisha hapa kwamba vifaa vya kijeshi inabidi viwafuate wakubwa wa jeshi dar
 
mimi binafsi sifahamu huko jeshini mambo ya uongozi yanaendaje...sijui kama ni siasa au ni experience na utaalam ndio vinazingatiwa.....ila kwa upande wa waziri, ni lazima ajiuzuru. wapo wabunge wengi tu ambao wanaweza kumreplace waziri yoyote katika nchi hii.
 
Jamani hili la ajali lichukuliwe kwa uzito wake na si kwa ushabiki wa kisiasa...kiungwana nadhani zifanyike juhudi za haraka za kuokoa maisha ya wahanga wa tukio hili na zichukuliwe hatua za haraka kuhakikisha hakuna maafa zaidi baadaye...na baadaya hali kuwa shwari mamlaka husika zijipime kama kuna uzembe wowote katika hili uwajibikaji uwepo!

Kwani ni mara ya kwanza kutokea?? mbona janga kama hili limetokea mbagala si muda mrefu? serikali ilijifunza nini kutokana na maafa yale?? imerekebisha wapi??? Hii serikali imeshatuona wajinga na kufanya longolongo tu... wahusika wawajibike!!!!!!!!!!1
 
Ukisikia viongozi hawana dira ndio hawa ,yaani baada ya kuitisha uchunguzi unakurupuka na kusema nani na nani wajiuzulu,basi huyo msemaji nae ajiuzulu ,wacheni uhuni,yaani unarukia watu wajiuzulu wakati hujui ni nini chanzo cha tukio.

Wandugu mkisikia watu wanajiuzulu huko majuu msifikiri wanakurupuka tu na kuachia ngazi kuna stage mbalimbali hupitwa na ndio kufikia ni nani wa kujiuzulu.

Mi nilifikiri katika taarifa hiyo CDM wamefanya uchunguzi na kugundua chanzo na sababu ni ya wakuu flaniflani ,kumbe hamna kitu ni mazungumzo baada ya habari.
Kwa ufupi tahadharini na habari za mitaani na kuzivalia njuga ,mtakuja kuumbuka baadae,embu wekeni kitengo cha uchunguzi na muwe mnazifanyia uchunguzi habari kabla hamjazitilia ubavu, yaani mkiulizwa suali la papo kwa papo kwa nini hao wajiuzulu sijui mtajibu dudu gani ? Zaidi mtasema ni uzembe ,mkiulizwa uzembe gani mtaanza kutafuna kucha.
WaCDM wacheni hizo karata za magarasa tumieni turufu ,natumai nimeeleweka.

we unataka uchunguzi gani ufanyike? mbagala si tume iliundwa na ilitoa ripoti yake? hiyo ripoti nani alipewa na walijifunza nini katika hiyo ripoti? si walisema ya mbagala ni ajali na haitotokea tena? sasa mbona imetokea?

acha kufanya watu wote majuha wewe.. hapa tunaongelea maisha ya watu wasiokua na hatia kupotea na sio siasa za ushabiki wa simba na yanga
 
Kujiuzuru hapa kwetu inahitaji mpaka maandamano...............nakumbuka waziri wa elimu ktk awamu iliyopita alitangaza kuwa km mtihani ungevuja tena angejiuzuru na haikuchukua muda ukavuja hakujiuzuru tukabaki kuchekace\heka tu na kumpigia makofi kikwete.......sijui tutabadilika lini vile
 
Kuhusu kuwajibika mtu hapo mtakuwa mmechemsha,Mbona Slaa anatembea na mke wa mtu ,mngeanzia huko kwanza kuwajibishana maana hata dini yake hairuhusu kufanya kitendo hicho.Tuache hilo maana ni private ,nikiingia huku ambako mnakuja na ndoto za mchana ,muelewe tu hawezi kuwajibika mtu mpaka chanzo kimeeleweka na kuhakikiwa ,hizo sababu za waliochoka hazina mshiko,hata wanasheria wanakubali ,kuwa kujiuzulu kutokane na kisababisho ambacho kitamhusisha mhusika moja kwa moja.
Maana hata huko Mbagala hatukuwasikia kuweka madai bungeni kuidai ripoti,sasa hili la Gongo la Mboto imejulikana wazi kuwa Chadema inahusika kwani hamuitakii heri nchi,mnataka kuleta uhuni.
 
Back
Top Bottom