Tamko la CHADEMA kuhusu Mabomu ya Gongo la Mboto

Ukisikia viongozi hawana dira ndio hawa ,yaani baada ya kuitisha uchunguzi unakurupuka na kusema nani na nani wajiuzulu,basi huyo msemaji nae ajiuzulu ,wacheni uhuni,yaani unarukia watu wajiuzulu wakati hujui ni nini chanzo cha tukio.

Wandugu mkisikia watu wanajiuzulu huko majuu msifikiri wanakurupuka tu na kuachia ngazi kuna stage mbalimbali hupitwa na ndio kufikia ni nani wa kujiuzulu.

Mi nilifikiri katika taarifa hiyo CDM wamefanya uchunguzi na kugundua chanzo na sababu ni ya wakuu flaniflani ,kumbe hamna kitu ni mazungumzo baada ya habari.
Kwa ufupi tahadharini na habari za mitaani na kuzivalia njuga ,mtakuja kuumbuka baadae,embu wekeni kitengo cha uchunguzi na muwe mnazifanyia uchunguzi habari kabla hamjazitilia ubavu, yaani mkiulizwa suali la papo kwa papo kwa nini hao wajiuzulu sijui mtajibu dudu gani ? Zaidi mtasema ni uzembe ,mkiulizwa uzembe gani mtaanza kutafuna kucha.
WaCDM wacheni hizo karata za magarasa tumieni turufu ,natumai nimeeleweka.




Huyu jamaa anajiita mwiba mimi nadhani hayuko sawa, hivi ni uchunguzi gani unataka ufanyike wakati mabomu yameua innocents tanzanians..tena ni zaidi ya mara moja imetokea.. maboma yamelipuka ni uzembe wa wahusika au uniambie yale ya mbagala CCM walisema nini Tatizo, au kuna mtu yeyote aliwajibishwa? usilete ushabiki wako wa CCM wakati suala hili very serious..wewe labda ni Fisadi au mtoto wa fisadi au kibaraka fulani, njoo maeneo ya Gongo la mboto alaf uongee ujinga wako kama utatoka mzima..
 
Na nyie wananchi mnaopenda kuishi karibu na hayo madude inabidi mbadilike,nyie ni sawa na wale wa mabondeni...
 
Nadhani hizo intelijensia zingesaidia sana kwenye masuala kama haya badala ya kutumika kuua raia wasio na hatia wala silaha kwenye maandamano ya amani. Kila mtu alitarajia tukio la mbagala lingetoa funzo kwa wahusika kuchukua hatua stahiki lakini hawakufanya hivyo mbali ya kukataa kujiuzulu. Sasa tunapoteza watu wasio na hatia na wengine kupata ulemavu. Huu ni UZEMBE WA HALI YA JUU. Rais, Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Majeshi LAZIMA WAJIUZULU.

Ama kweli hizo interijensia zai zitumike kwa mambo kama hayo na sio tuwapeleke kusoma na kulitumikia jeshi na wao wanarudi kuwa vibaraka na makada wa CCM.

Imefika wakati Viongozi wa juu wajuwe wajibu wao kwa Taifa na sio mzaha kila mara, Kwanza nataka kujua wapi Report ya kwanza wakati wa mabomu ya mbagala, Waliweka mikakati ipi kutokujirudia kwa hilo tatizo la mabomu kulipuka, Je ni jinsi gani walijipanga kuhifadhi siraha zote katika maghara yenye usalama na usio tishia maisha ya wanajeshi na raia . Nini Kazi ya kitengo cha majanga kinachofanya maana kuwajibika kwao ni mpaka maaafa yatokeee?

Maana kuto kufanyiwa kazi kwa report ya kwanza ndiko chanzo cha tatizo la pili na kama wakitoa report ya pili na kuihifadhi kwenye Computer na makablasha yao basi kutatokea janga lingine la tatu then watatuma salamu za lambilambi kama mwanzo Jamani Serikali acheni mzaaaa hao ndio wananchi walio wapa kura na mkawa hapo kwa hayo madaraka na sio kushangaaa tuu kila mara mwonekane kwa runinga na huku hakuna mnacho kifanya juu ya usalama wa wananchi wenu.

Je serikali kama serikali imejipanga vipi swala la ulinzi na usalama maaana tukivamiwa ndani ya nchi yetu kweli hatuna mwelekeo wa wapi pa kujificha au kukimbilia kwani imejidhihirisha tu kwa hali ya mbagala na gongo la mboto wananchi wamepotezana (Familia) ndugu na jamaa. Najua hii iko wazi Jeshi letu lina mapungufu sana, Linatakiwa kujipanga upya si shangai kwanini mwalimu alitaka wananchi wawezi kujifunza mbinu za kijeshi kabla hujaingia vyuo vikuuu au Makazini ila kukapita hapo siasa za kinafika na kidhalimu na kifisadi na ndio haya sasa viongozi hawana maadili wala uzalendo kabisa na kushindwa kuwajibika.

Twahitaji vikosi maaarumu kwa ajili ya hali kama hizi na tuache siasa humu ndani ya nchi na tuwafanyie kazi wananchi wetu, Maana nchii(Serikali) yetu kila ikikumbwa na janga lolote yenyewe inakuwa mstaari wa nyuma kabisa kukimbilia kuwaokoa wananchi wake jamani khaa.

 
Na nyie wananchi mnaopenda kuishi karibu na hayo madude inabidi mbadilike,nyie ni sawa na wale wa mabondeni...

Msauzi ,

Hapo nitawatetea wananchi kwanza kwani City Planning kama ilikuwa ni mbovu na ilijua kabisa miji inakuwa na ramini za mipango miji wanazo kwanini waliwagawia viwanja wananchi katika maeneo ya Jeshi, viwanja vya ndege na maeneo muhimu ambayo raia hawatakiwi kuishi? Hizo zilikuwa ni njaaa za viongozi wa awamu zote na makosa hayo serikali inayajua na wanaogopa kuwajibika kwani uozo uliokuwepo ndio wao walioubaliki sasa wananchi ndio wana patwa na matatizo,

Hili ni funzo kwa viongozi waandamizi wasiopenda kuwa very creative na kuwa proactive into National Matter wao ni kujali matumbo yaooo ndo haya yaja hata huku mikoani kwetu mipangomiji ni jambo amabalo latakiwa kupewa kipaumbele na sio mzaha kabisa. tujaribu kubadilika jamani Changes ni lazima tu zije na nilazima tuzikubali kwani siku hazigani bali zinakimbia sana. Utache kuwa wazembe na kufanya mipango madhubuti kwaaji ya kuwapa wananchi wetu maisha bora na sio porojo na si ha sa.

 
Ni jambo la kusikitisha na kushangaza sana! Kwanza kabisa nawapa pole sana kwa wote walioathirika mojakwa moja na milipuko ya mabomu na wale tulioathirika indirectly.

Kwa akili yangu kidogo niliyonayo maafa kama haya kutokea katika kipindi cha miaka mitatu ni aibu kubwa kwa nchi na hasa serikali iliyoko madarakani. 2008 mabomu yaliwahi kulipuka hapao hapo gongolamboto, April 2009 yakalipuka mbagara, February 2011 yamelipuka tena Gongolamboto! Ukiangalia series ya matukio haya kwa wanasiasa ni bahati mbaya kwangu mimi nasema this is a planned & coordinated tragedy! Kwa nini? Tangia enzi za akina Newton na wengineo kilichofuata imekuwa ni kujifunza na kuboresha zaidi, na historia itabakia hivyo. Hii mara ya tatu sasa hatujasikia kiongozi yeyote akichukua hatua tofauti na kuunda tume na ripoti hatujawai kuziona na amiri jeshi mkuu kuridhika na hilo.

Haya yote yanatokea kwa kuwa hakuna wakumwajibisha mwenzake na tutabaki kuchekeanachekeana mpaka mwisho. Watu huwa wanaresign si kwamba ni baada ya uchungunzi na tumwe kuundwa, mosi watu hu-resign kwa kujutia maovu yaliyotokea chini ya uongozi/usimamizi/utawala wao, kutoa nafasi ili kama kunahitajika kufanyika uchunguzi wa kubaini chanzo cha tatizo uweze kuwa wa huru na haki na tatu kupisha watu wenye uwezo zaidi kuweza kukabiliana na maovu yaliyotokea chini ya utawala/usimamizi/ na uongozi wao. Kitendo cha serikali yetu kuona maafa kama haya yanatokea mara tatu na hakuna hata mmoja anajutia ni cha aibu kukubwa mno, kinatishia usalama wa raia na ndo maana nasema ni mambo ambayo jeshi la wananchi na amiri jeshi mkuu hawawezi kukwepa lawama. Hivi tukisema serikali ya Tanzania hupima uwezo wa vifaa vya kijeshi iliyonavyo kwa kuwaangamiza wananchi wake nani anaweza kupinga hili?

Watanzania usalama wetu u mikononi mwetu na si mikononi mwa vyombo vya ulinzi na usalama kama tulivyozoea, Mbagara, Arusha, Mbeya na sasa Gongo la Mboto ni vielelezo tosha. Ni dhahiri kabisa kuwa kuna haja sasa kwetu wananchi kuamua mstakabali wa maisha yetu na kukabidhi nchi yetu kwa watu watakaoongoza taifa na kuwalinda wananchi wake kihuai, kiuchumi, kiafya n.k kwa vinginevyo tutazidi kuuawawa na pesa zitazidi kutumika kwa ajiri ya tume bila ufumbuzi wowote maana tume siku hizi ni mradi, ikilipuka Gongolamboto, billion kadhaa tume itatumia! Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchuuzi (serikali)!
 
Hivi baada ya Tamko, waliotakiwa kujiuzulu wamejiuzulu? Kwenye maandamano ya Chadema bado wanadai viongozi wajiuzulu, lakini sioni tija ya hayo madai.
 
Back
Top Bottom