Takwimu zinaonyesha ccm ni chama zaifu sana

JUST

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
552
234
Ni wazi kuwa kauli ya kuwa CCM ni chama kilichokomaa zimekuwa zikitolewa kila uchao na makada wake. Baadhi ya watu walio wengi wamekuwa wakiubeba usemi huo kama ulivyo na bila ya kuufanyia utafiti na kuusimamia kuwa ni kweli. Ni ukweli kuwa nguvu ya chama cha siasa hupimwa zaidi nyakati za chaguzi hasa kuitia matokeo ya uraisi maana ni mahali amabapo huonyesha kukubalika kwa chama husika kwa wananchi.

kwa bahati nzuri kumbukumbu zitatusaidia kuonyesha ya kuwa CCM ni chama dhaifu sana na hakikubaliki kwa wananchi wa Tanzania kama wanavyojigamba. yafuatayo ni uchambuzi mfupi wa matokeo ya chaguzi kuu nchini Tanzania kwa nafasi ya raisi.


1. Mwaka 1995 CCM ilipata kura 4, 026,422 nusu ya waliojiandikisha kupiga kura 8,929,969. wakati huo watanzania walikuwa zaidi ya milioni 23.

2. Mwaka 2000 CCM ilipata kura 5,863,201 nusu ya walijiandikisha kupiga kura 10,088,484. wakati huo watanzania walikuwa wanakadiriwa kuwa milioni 30

3. Mwaka 2005 CCM ilipata kura 9,123,952 robo tatu ya waliojiandikisha kupiga kura 16,442,657. hapa walipata matokeo yaliyowastajabisha na wakati huo watanzania walikuwa wanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 35


4. Mwaka 2010 CCM ilipata kura 5,276,827 robo ya waliojiandikisha 20,137,303. wakati huo watanzania wnakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 40

Kwa mujibu wa takwimu hizo ni kuwa CCM yenye miaka 50 ya kujijenga kichama ni dhaifu sana maana kwa wastani wa wapiga kura milioni 5 ukilinganisha na muda wa miaka hamsini ya kujijenga ni wazi kuwa bado hakijakonga nyoyo za wananchi na hakina tofauti na vyama vya upinzani vilivyoanza miaka 20 iliyopita zaidi ya kutawala dola.


Nawasilisha.
 
Wakiongozwa na Mwenyekiti- Dhaifu
ot1.jpg
 
mwenyekiti anakanusha hakiende kufa, so hizo takwimu anazijua na hofu ya kufa anaifahamu ndiop maana anakanusha CCM Haifi, ukiona mwenyekiti anakanusha kuhusu kufa ama la,, ujue kuna walakini..
 
KOMBAJR hiyo picha haujaipambanua yaani umeniacha na maswli mengi
 
mwenyekiti anakanusha hakiende kufa, so hizo takwimu anazijua na hofu ya kufa anaifahamu ndiop maana anakanusha CCM Haifi, ukiona mwenyekiti anakanusha kuhusu kufa ama la,, ujue kuna walakini..

huu usemi wako unanikumbusha msemo wa sikio la kufa halina dawa
 
toeni siasa zenu za maji taka humu,dhaifu ni chadema na udhaifu wameuonyesha kabla hawajachukua nchi wakichukua itakuaje, si ndo watuletea mambo ya (hitla)..watu wote tunajua kuwa chadema bila ndesambulo haipo
 
toeni siasa zenu za maji taka humu,dhaifu ni chadema na udhaifu wameuonyesha kabla hawajachukua nchi wakichukua itakuaje, si ndo watuletea mambo ya (hitla)..watu wote tunajua kuwa chadema bila ndesambulo haipo

usiwe mmoja wa wale wapambe wanaowadangaya viongozi kwa kupindisha ukweli. Takwimu hizi ni nzuri kwa CCM kuona upepo unavyokwenda na kujitathimini kwa mabadiliko kwa manufaa yake yenyewe
 
Back
Top Bottom