Chuo Kikuu cha Mzumbe chakiri Wanafunzi zaidi ya 500 wanadai malipo ya 'refund' chuoni hapo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Baada ya malalamiko kutoka kwa memba wa JamiiForums kuwa kuna Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe ambao walijilipia Ada wakati wa kujisajili kabla Bodi ya Mkopo kuingiza malipo ya mkopo wao, hivyo wakaahidiwa kurejeshewa kiasi cha fedha kilichozidi lakini hali imekuwa tofauti, ufafanuzi umetolewa.

Madai yalieleza kuwa Wanafunzi walitumia fedha za kujikimu kulipa Ada wakiamini watarejeshewa baada ya muda mfupi lakini imepita miezi kadhaa kimya na chuo kimekuwa kikitoa ahadi zisizotimia, hivyo imekuwa changamoto kwao kumudu gharama za maisha nje ya chuo

Ikadaiwa kuwa idadi ya Wanafunzi ambao wana madai hayo ni zaidi ya 500.

Andiko la malalamiko hili hapa: Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe wadai kucheleweshewa pesa yao waliyolipa kwa ajili ada kabla ya Serikali kuwaongeza mkopo

MAELEZO YA CHUO KIKUU CHA MZUMBE
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mzumbe, Lulu Mussa anafafanua kwa kusema:

“Ni kweli kuna changamoto hiyo ya baadhi ya Wanafunzi wanaodai ‘refund’, malalamiko au mafaili yaliyopokelewa kudai kurejeshewa fedha ni 1,211, Wanafunzi ambao wameshalipwa mpaka sasa (Seotemba 22, 2023) ni 634

Ambao wanatarajiwa kulipwa hadi kufikia Ijumaa ya Septemba 29, 2023 ni 246, ukijumlisha idadi hiyo na ukatoa ambao wameshalipwa (634) na ukajumlisha ambao malipo yao yapo njiani hadi kufikia wiki ijayo, ambao watakuwa wanaendelea kudai ni 331.

“Hatua mbalimbali zinaendelea kwa ajili ya malipo kwa hao wengine, changamoto ilikuwa ni masuala ya uhakiki, kupitia taarifa zote muhimu.”
 
Nasisi wa vyuo vingine tunazidi kusubirishwa tu izo refund
 
Back
Top Bottom