The Next MP
Member
- Nov 15, 2023
- 37
- 43
Nawapa alarm TAKUKURU, Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoa wa Pwani inanuka wizi wa fedha za wananchi kupitia urasimishaji wa makazi na upimaji wa viwanja katika kata mbalimbali ndani ya Mji wa Kibaha hasa, Kata ya Pangani kwenye mitaa ya Kidimu, Lumumba na Mkombozi.
Kwanza awali wananchi walitakiwa kulipa milioni moja na laki sita (1,600,000TZS) ili warasimishiwe makazi yao kwa kupimiwa. Baada ya kuona wanagoma wakashusha mpaka laki sita (600,000TZS) kwa kila mwananchi mwenye eneo la 20x20, ukiwa na 20x20 mbili na gharama ni mara mbili na kuendelea.
Wizi unakuja hapa, mwananchi akishafika kuhakiki eneo lake anapewa fomu inayomwelekeza kuweka Shilingi laki nne na elfu hamsini kwenye account maalum, akimaliza malipo hayo ndipo atapatiwa Control namba kulipia Laki moja na elfu hamsini (150,000TZS) ambayo ndio kiwango cha Serikali. Sasa wananchi wanahoji hiyo pesa nyingine inakwenda wapi?
Mbaya zaidi waliohoji sana walikamatwa na kuwekwa ndani. Niishie hapa, naendelea na uchunguzi zaidi, next time nitaleta account namba na anayehold hiyo account pia nitaleta majina ya viongozi wote wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha wanaohusika na hujuma hizi.
==
Soma Majibu ya Halmashauri ya Kibaha kuhusu tuhuma za Rushwa katika urasimishaji viwanja