Kisonoko Mlamba ukoko
Member
- Dec 2, 2023
- 6
- 15
Kinachofanyika Kibaha Kidimu ni dhuruma ya mabavu ya waziwazi, watu wanapokonywa umiliki wa maeneo yao hata baada ya kuyamiliki kwa zaidi ya miaka ishirini na kuambiwa wayanunue, wakati wapo watu waliouziwa na wenyeji kwa usimamizi wa serikali ya kijiji na wamefanya maendeleo ya kudumu vikiwemo makazi na biashara!
Fikiria watu wapo pale zaidi ya miaka ishirini, wameishi na kufanya shughuli zao muda wote huo,serikali za vijiji zikaimarishwa, shule na zahanati vikajengwa, barabara zakachongwa,umeme ukafikishwa, ajabu leo tuje kuambiwa kuwa maeneo yale ni ya serikali wananchi tumevamia!
Kama ni maeneo ya serikali, sheria inasemaje juu ya umiliki na matumizi ya ardhi? Serikali ilikuwa wapi miaka yote hiyo mpaka waje waibuke leo hii na kuleta usumbufu wote huu?
Ni kama kuna watu wachache wameona kuna fursa ya kupiga fedha kwa wananchi wanyonge, wameamua kututingisha na kutumia udhaifu wa ulalahoi wetu kutuvuna watakavyo.
Leo hii mtu akanunue eneo lake alililokwisha kuuziwa chini ya serikali ya kijiji kwa ushahidi wa nyaraka rasmi za serikali? Tunauziwa kwa bei ya kukomolewa kana kwamba sisi ni walowezi tusio na kwetu!
Upigaji umetawala manispaa, utaratibu wa malipo ni wa kubumba, bili zinazotolewa hazilipwi kwa control number, zinalipwa kwenye akaunti ya benki ya manispaa ya Kibaha, ushahidi wa namba ya akaunti na jina vipo, ni malipo gani ya serikali yanayolipwa kwa bank account kwa sasa badala ya namba ya malipo?
Hizi fedha zinakwenda wapi? Watu wamepoteza viwanja kwa kuuziwa watu wengine baada ya kushindwa kulipia,watu wamebomolewa majumba chini ya usimamizi wa askari wenye silaha na msafara wa viongozi wa manispaa.
Baraza ka madiwani linahusika katika kupitisha maovu haya, wananchi wanyonge wanabaki wakilialia tu na kunung'unika pembeni wasijue la kufanya.
Tafadhali tunaomba msaada ya kisheria katika hili, tusaidieni kupaza sauti tuokoe viwanja na nyumba zetu.
Pia soma:
= Majibu ya Halmashauri ya Kibaha kuhusu tuhuma za Rushwa katika urasimishaji viwanja
= TAKUKURU chunguzeni Halmashauri ya Mji wa Kibaha pananuka wizi kuhusu ardhi