Kwa wale wenye magari ambao hawapendelei kununua used spair parts kama matairi yaliyotumika na kuchongwa, na kuamua kujikamua kununua tairi mpya toka dukani, kuna haja ya kuwa makini hasa katika kujua tairi hilo jipya lilitengezwa lini. Wenzetu wa magharibi wanaanza kufikiria kuwa "aging" yaani umri wa tairi unaweza kuwa sababu tosha ya kusababisha matairi kujimenya na kusababisha ajali na kupendekeza miaka isizidi sita ya tairi toka kutengenezwa mpaka kununua. Wasiwasi wangu ni kwamba kama sheria hizi zikipita huku kwao basi kuna uwezekano mkubwa na matairi yaliyokaa muda mrefu kutupiwa sisi ili yatumalize.
Je unawezaje kutambua umri wa Tairi toka lilipotengenezwa?
Jibu rahisi sana, kila tairi lina namba na trade mark zake ila kuna namba ambazo ninaamini wengi wetu hatuzijui ni za nini, namba hizo zinaweza kuwa tatu au nne zimezuungushiwa round kila moja. Hizi ndizo namba zinazoonesha tairi limetengenezwa lini japo ni jipya.
Mfano:-
1. namba 519: hii inaonesha tairi limetengenezwa wiki ya 51 mwaka 1999
2. namba 236: hii inaonesha tairi limetengenezwa wiki ya 23 ya mwaka 1996
3. Namba 4107: inaonesha tairi imetengezwa wiki ya 41 ya mwaka 2007
4. Namba 1708: inaonesha tairi imetengenezwa wiki ya 17 ya mwaka 2008.
Kwa hiyo tusisubiri mpaka TBS huenda hawajui haya kutuambia ila unaweza kujiridhisha mwenyewe kuwa unanunua kitu cha lini na kwa thamani bora ya pesa na usalama wa maisha yako.
unaweza kujifunza zaidi toka HAPA

Last edited: