Taifa stars yaleyaleeeeeeeeeee

KELVIN GASPER

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,066
454
Hivi tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?.Usemi huu wa mzee ruksa unaonekana haujatupa fundisho lolote walimu na wachezaji wa timu yetu ya taifa. Jana tumecheza na msumbiji mechi maalum kwa ajili ya ufunguzi wa uwanja wa kisasa uliojengwa na wachina huko msumbiji timu yetu imefungwa 2-0. najua wakirudi sababu lukuki tusubiri.
 
Nilipoiona first 11 nikajua tunachezea kichapo!!!!ile sicho kikosi utawapelekea Mamba hata siku moja!!!labda Malawi huko
 
Ndugu zangu binafsi hile mechi niliicheki tokea kuzindua uwanja mpaka mchezo unaisha,yafuatayo niliyaona;
uwanja wao unafanana na wetu kwa kiasi kikubwa japo wao haujafunikwa wote, katika kuzindua wenzetu walifanya kweli, waliandaa mpaka mashindano ya mbio, hotuba zilikuwa za kumwaga, wakati wa halftime wanariadha walizunguka mbio (100m&200), waliwasha mafataki uwanja mzima (kama S.A 2010 world cup), n.k baada ya hapo niliwaza sana huku kwetu TFF mbona haikuandaa haya ama ndo low creativity? for sure TFF haikutenda haki kwa uwanja wetu na kwa watanzania
kimchezo wapiganaji wetu wengi hawakuwepo, baada ya Ndihire kuchomwa mshale aliingia Kaseja naye akachomwa jingine,mabeki wetu walijisahau sana,mastriker wetu walishindwa kujipanga pasi zikawa zinaishia kwa mabeki
nadhani tunahitaji kutengeneza vijana zaidi yawezekana hawa wa sahivi wamechoka na hawana tena uwezo wa kutumia mbinu mpya
 
Ndugu zangu binafsi hile mechi niliicheki tokea kuzindua uwanja mpaka mchezo unaisha,yafuatayo niliyaona;
uwanja wao unafanana na wetu kwa kiasi kikubwa japo wao haujafunikwa wote,katika kuzindua wenzetu walifanya kweli,waliandaa mpaka mashindano ya mbio,wakati wa halftime wanariadha walizunguka mbio (100m&200),waliwasha mafataki uwanja mzima (kama S.A 2010), niliwaza sana huku TFF mbona haikuandaa haya ama ndo low creativity? for sure TFF haikutenda haki kwa uwanja wetu na kwa watanzania
kimchezo wapiganaji wetu wengi hawakuwepo, baada ya Ndihire kuchomwa mshale aliingia Kaseja naye akachomwa jingine,mabeki wetu walijisahau sana,mastriker wetu walishindwa kujipanga pasi zikawa zinaishia kwa mabeki
nadhani tunahitaji kutengeneza vijana zaidi yawezekana hawa wa sahivi wamechoka na hawana tena uwezo wa kutumia mbinu mpya
 
Hii taifa stars kama Arsenal, tunacheza vizuri tunafungwa sie, reebok stadium tutatoka? kwa wale wenzangu mechi inaanza saa 12.00 jioni. tumeishikilia nafasi ya pili kwa kipindi kirefu. mechi zimebaki 5 tumeshuka nafasi moja nyuma badala ya kukea juu kwenye ubingwa, kazi kwelikweli.
 
Hivi wale vijana wa Academy bado tu jamani? We need them now, coz it has been a while since they joined the school. Taifa Star bado ni mzigo kwa watanzania, tutaendelea kuwa wateja wa ligi za wanzetu wakati vichwa tunavyo ila hatutaki kuvisumbua kuboresha ya kwetu. Utasikia oooh mi niko Nigeria mara mi Brazil mara Ujeruman! TFF fanyeni kazi acheni uvivu.

Mfano: Hivi kwa nini tiketi huwa mnaziuza kwa madewaka nao wanaanza kuturushia bei kama 3000 inakuwa 5000? Huu nao ni ufisadi. Take care!

Tunahitaji creactive minds kwenye kila sector siyo michezo tu jamani, mtu anataka kuwa kiongozi ili awe tajiri na haridhiki na mshahara wake utegee kuna ubunifu hapo? Never! ni majungu tu kwenda mbele.
 
Ile timu ya Julio U23 ndiyo ingeenda Msumbiji ni timu nzuri sana na ina vijana wanaojituma

hili li timu lina wazee tupu na cha kushangaza ni wazee ambao Marximo aliwakataa sasa wamerudishwa kwa mlango wa nyuma na TFF

TFF hamna kitu, hawaweze kuplan kitu chochote kizuri kwa Tanzania. wachezaji wazuri wapo, funding zipo(wadhamini na pia wananchi wapo tayari kulipa viingilio kwa mechi nzuri), ari ya football kwa tanzania ipo juu sana. maskini Tanzania
 
Nilipoiona first 11 nikajua tunachezea kichapo!!!!ile sicho kikosi utawapelekea Mamba hata siku moja!!!labda Malawi huko

We! We! We! Timu ya taifa ya Malawi unaijua au unaisikia? Kama hujui soka la Afrika ni vyema ukakaa kimya, kati ya timu bora ukanda ule wa kusini Malawi ni mojawapo, hata Misri wanaujua mziki wao,..
 
Mimi nashindwa kuwaelewa WAKUU. Mbona huwa mnajitokeza tukifungwa tu. Tulipoifunga Afrika ya Kati. Wachangiaji tulikua wachache sana. Mpira ni pamoja na kufungwa, droo, na ushindi. Kimsingi timu yetu, imekua ikikua...hapa namaanisha kila kitu; si kama kipindi cha fat. Pia timu iliyokwenda haikuwa na mastaa wetu, nizar, mrwanda, henry joseph, babi, idrissa rajab....mimi nawapongeza tff hapo zamani hatukupata hata mwaliko sasa tunaalikwa na misri, msumbiji.....we are cooming up " raha ya mpira si kushinda tu" na kufungwa pia
 
Ni wewe...acha upuuzi,haiwezekani mtanzania mzalendo ukakosa kumjua kocha wa stars...</b></font>
Acha pumba, kocha wa stars sio rais mpaka wazalendo wote wamjue!, hana tofauti na kocha wa darts, bao au draft, ambao hata wewe huwajui!, wengine hapa tukiona mpira tunashangaa kuona watu wanapagawa kwa mchezo wa kijinga!, hebu jiulize, kuna raha gani mtu mzima na akili zake akikimbia na mpira unaodunda dunda?, si upuuzi huo? Mwenye akili hawezi kuwa shabiki wa mpira wa miguu, bora hata mpira wa kiume!
 
Tatizo letu kubwa lipo kwa viongozi wa TFF hawataki kuwa wawazi kusiana na swala zima la Team yetu ya Taifa, kwani huu sio mda wakuendelea kuwakumbatia wachezaji wazee hapana sio mahali pake kabisa kwasasa imefika wakati sasa tunatakiwa kuwapa vijana nafasi hasa kwa kuanzisha Academic katika mikoa yote ya Tanzania ili tuweze kuwapata vijana watakaweza kutupeleka huko tunakokutaka Watanzania. tusitegemee ndoto za hali nacha kabisa katika mchezo huu wa soka ambao nchi nyingi zipo juu sana kisoka hivo basi tunahitaji maandalizi mazuri sana ya kuwapata vijana watakaotutoa kidede hasa katika mchezo huu maalufu wa Soka Duniani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom