Taifa likiingia vitani leo,Itakuwaje?

Mi nataka tuende vitani ili badala ya hela kutumika kumzungusha JK kwenye nchi mbalimbali tuzitumie hizo hela kwenye jeshi na vijana wetu inabidi wapate practice jamani mtu anakua mwanajeshi miaka 25 lakini hajui vita ikoje
 
Tena itokee, tutashirikiana na Malawi kuwang'oa CCM kama Waganda walivyoshirikiana na Tanzania kumng'oa Amin mwaka 1978.
 
Nimejiuliza sana swali hili bila majibu. Nisaidieni.

Mwaka 1978 tuliingia vitani na Uganda chini ya Idd Amin, lakini tulipambana kama Taifa vita ile kwa pamoja yaani viongozi wetu, makamanda, askari, Taasisi mbalimbali na Raia wote hadi tukashinda.

Sasa hivi hatuna tena maelewano ya aina ile. Tunachokiona ni uhasama kati Bunge na Serikali, Serikali na Raia wake, Taasisi na Taasisi na hata Askari na Raia. Ufisadi umeshika kasi ndani ya Taasisi muhimu za Umma kiasi kufikia kununua vifaa vya kijeshi vinavyodhaniwa kuwa viko chini ya kiwango (fake) hasa tukikumbuka vitu kama Helicopter zinazoanguka hovyo na mabomu yanayolipuka hovyo.

Jee kwa hali kama hiyo, ikitokea nchi jirani kushambulia mipaka yetu tunao uwezo wa kuhimili mapigo kama ule wa mwaka 1978 kama Taifa? Ama tutaita wawekezaji wa kijeshi kutulindia mipaka yetu huku sisi tukiendelea kupiga soga la malumbano?

Mie natamani sana waje watupige baada ya hapo ndio uzalendo na uwajibikaji wa kila mmoja wetu kwa nafasi yake ndo utarejea vinginevyo tunajidanganya tu.
 
Nimejiuliza sana swali hili bila majibu. Nisaidieni.

Mwaka 1978 tuliingia vitani na Uganda chini ya Idd Amin, lakini tulipambana kama Taifa vita ile kwa pamoja yaani viongozi wetu, makamanda, askari, Taasisi mbalimbali na Raia wote hadi tukashinda.

Sasa hivi hatuna tena maelewano ya aina ile. Tunachokiona ni uhasama kati Bunge na Serikali, Serikali na Raia wake, Taasisi na Taasisi na hata Askari na Raia. Ufisadi umeshika kasi ndani ya Taasisi muhimu za Umma kiasi kufikia kununua vifaa vya kijeshi vinavyodhaniwa kuwa viko chini ya kiwango (fake) hasa tukikumbuka vitu kama Helicopter zinazoanguka hovyo na mabomu yanayolipuka hovyo.

Jee kwa hali kama hiyo, ikitokea nchi jirani kushambulia mipaka yetu tunao uwezo wa kuhimili mapigo kama ule wa mwaka 1978 kama Taifa? Ama tutaita wawekezaji wa kijeshi kutulindia mipaka yetu huku sisi tukiendelea kupiga soga la malumbano?

Tutaita wanajeshi kama 1000 na zaidi yoka Iran. Maana ya hii serikali ya akina "liwalo na liwe" imekaa kikuomba omba misaada sana.
My view:
Kwa kuwa watakaopigana ni wanajeshi, nadhani hakuna tatizo. Ila sema adui anaweza kutumia mgawanyiko wa wananchi kupata intelijensia ( maana watu kwa sasa hatulipendi jeshi, serikali ya CCM na biongozi baadhi, polisi hatuwapendi, ma dakitari hawapendwi kuanzia na serikali mpaka raia- hivyo majeruhi wa vita watakosa wa kuwatibu, n.k..)
 
Duh...watu kweli mmepinda.
Hivi jwtz wana mitumbwi mingapi ya kijeshi pale lake malawi?
 
"..People are lonely because they build walls instead of bridges" Joseph. F.Newton
 
kwa sasa vita haitufai sababu;
1. Jeshi letu sasa ni la kibiashara na ufisadi km vile linajishughulisha nakuuza matrekta kugawana vyeo kwa misingi ya kujuana badala ya kupitia ngazi mbalimbali za mafunzo.
2. Vijana wanaingia jeshini kufuata ajira na si kwa vigezo stahili kama zamani.
3. Kilimo kwanza kule jeshini kinalimaliza jeshi kwa ufisadi maana maafisa wanashindana kuchuma, na kuhamisha fedha.
 
Tena itokee, tutashirikiana na Malawi kuwang'oa CCM kama Waganda walivyoshirikiana na Tanzania kumng'oa Amin mwaka 1978.
Hata mie wasiwasi wangu ni huo kwa jinsi watu walivyo jikatia tamaa. Walio madarakani waliangalie hili kwa jicho kali zaidi kwani mara nyingi uasi wa raia unatokana na jinsi serikali yao inavyo watendea.
Ukiwatendea raia wako kama adui zako lazima watakurudi tuu wakipata nafasi.
 
Sio Jambo jema kushangilia vita lakini ikifika wakati unaweza ukaipenda vita kwa sababu ya ujinga uliopo nadriki kusema hivyo kwa sababu Watanzania tumewahi kuionja adha ya vita pale tulivyopigana na Uganda hadi kumtoa kwenye utawala marehemu Iddi Amin Dada aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo.Tanzania baada ya vita hiyo Askari wetu wameingizwa kwenye mifarakano ya nchi kadhaa za Afrika kama, Somalia, Dafur, Jibuti, Madagaskar, na kwingineko mifarakano ambayo haikuwa ya lazima ndugu zetu askali tunadhani wamepoteza huko kwani vita haina macho kuchagua huyu ni askari mwema na huyu hafai, lakini kibaya zaidi Watanzania kwa mamia na mamilioni tunapata taabu kwenye nchi yetu kutokana na hali ngumu ya maisha wenzetu wapo tu kwani wenzetu wananunua bidhaa bila kodi inayo wakabili wtz kwa maneno mengine wenzetu wanaishi maisha ya raha.watu wanatoka nje wanabeba nyara zetu kwa ndege wenzetu wapo tu sasa ni wakati kuonyesha wanawajibika kwenye mipaka yetu.
 
Kama amri jeshi mkuu ameshidwa vita ya ufisadi hiyo ndio ataweza?
 
Back
Top Bottom