Tahadharini na wafanyakazi wa ndani,H/G!

Nundu wa Selote ana point.
Kuna kitu inaitwa sleep Walk ni ugonjwa.

Mtu anaamka usiku,
anafungua jokofu,
anachua misosi anapasha moto,
anakaa na kula,
hali yupo usingizini.

Ukimshitua unaweza kumpeleka katika shock,
na brain ikashindwa kufanya kazi vizuri kwa muda.

Kitaalamu ugonjwa upo.

Hata hivyo sipingi madai kwamba,
ana nguvu nyingine kutoka katika dunia ya roho.


Kabla ya kuingia kwangu ktk mparangano wa hapa town nimeenda tena nyumba ile lengwa na kukuta maombi ya Imani ikifanyika haswa na mpk sasa yule H/G hajazinduka,na kila akipata kusema neno ni kwmb anasema "ACHENI KUNIUNGUZA,NINATOKA NISAMEHENI" ndiyo lugha yake kubwa mara akitaka kusema neno.

Kazi kweli kweli!
 
Hapo kwenye red mpaka mwili wangu umetetemeka.Unaweza kusifia nyama ya leo tamu sana, kumbe bonge la maiti ya ajali.Eeeh Mungu tusaidie!
kama ulikuwepo na wao walikuwa wanasifia nyama tamu kweli kumbe za watu.
 
Uuuuwi jamani haya mambo mhhhh
Mie binafsi yalinikuta lakini sijui kama nilikuwa nawangiwa ama la.
Msichana mwenyewe aliniambia historia yake ya huko alikotokea, kuwa aliwahi kupotea for a year katika mazingira ya kutatanisha, wazazi wakajua amefariki! kumbe anaishi na bibi yake aliyefariki huko mapangoni!!!! uuuwi vinatisha nyie...nakumbuka mwili ulipata ganzi nikawa siwezi kuinuka nlipokaa kwa kama saa nzima hivi,,,,ukizingatia kuwa ndiye ninayemuacha na mtoto mimi nikienda kazini!!!aliniambia pia ana majini kibao mpaka makata lkn kwa sasa eti yamefungwa mpk atakapofikisha umri flani!!!
Nilinywea!!!
Kumfukuza nikawa naogopa maana sikuwa na sababu ya wazi!
Nashukuru Mungu hakukaa sana sababu ya kuondoka ikapataikana!!!

Tuliachana kwa wema na hakuna chochote kibaya kilotokea!

Ila bi dada nadhani sasa hivi atakuwa sangoma maana alinipigia kunijulia hali akasema ameanza kufundishwa hiyo fani!
That was last year!!!

"Nadhani itafikia wakati itabidi kuacha kazi ili kulea......................" (mhhh just thinking louder hapa)
 
Uuuuwi jamani haya mambo mhhhh
Mie binafsi yalinikuta lakini sijui kama nilikuwa nawangiwa ama la.
Msichana mwenyewe aliniambia historia yake ya huko alikotokea, kuwa aliwahi kupotea for a year katika mazingira ya kutatanisha, wazazi wakajua amefariki! kumbe anaishi na bibi yake aliyefariki huko mapangoni!!!! uuuwi vinatisha nyie...nakumbuka mwili ulipata ganzi nikawa siwezi kuinuka nlipokaa kwa kama saa nzima hivi,,,,ukizingatia kuwa ndiye ninayemuacha na mtoto mimi nikienda kazini!!!aliniambia pia ana majini kibao mpaka makata lkn kwa sasa eti yamefungwa mpk atakapofikisha umri flani!!!
Nilinywea!!!
Kumfukuza nikawa naogopa maana sikuwa na sababu ya wazi!
Nashukuru Mungu hakukaa sana sababu ya kuondoka ikapataikana!!!

Tuliachana kwa wema na hakuna chochote kibaya kilotokea!

Ila bi dada nadhani sasa hivi atakuwa sangoma maana alinipigia kunijulia hali akasema ameanza kufundishwa hiyo fani!
That was last year!!!

"Nadhani itafikia wakati itabidi kuacha kazi ili kulea......................" (mhhh just thinking louder hapa)


Kuna habari nyingine true nimepata muda si mrefu hapa ktkt ya mji na inafanana na hii ya kwako haswa!

Pole Mpendwa wetu!
 
Hatari sana sister
we acha tu......kuna mwingine yeye alikuwa anasafirisha chakula.......utakuta baada ya wiki kila kitu kimeisha wanashangaa hivi vitu vimeishaje kumbe H/G anapeleka kwao kubanwa ndo akasema hivyo.

haya mambo acheni kabisa ni hatari sana.
 
ndugu liverpool,

hii taarifa yako inaonekana ina mapungufu makubwa-kama ya kutunga vile!!! Je housegirl zaidi ya kukutwa akiwa uchi sebuleni alikuwa akifanya nini? Nina maana ni kitu gani kilifanya wenye nyumba waseme anawanga? Je, haiwezekani kwamba alikuwa kwenye ndoto? Suala la kuwa uchi inawezekana alilala bila nguo na alioanza kuota akaamka na kutoka kama alivyokutwa. Je ni madhara gani aliyoleta zaidi ya hadithi za milango kukutwa wazi? Je kukutwa kwa huyo housegirl ambaye mwandishi wa habari hii hautueleza hata hicho alichokuwa akibwabwaja, inatosha kutuambia tujiadhari na wasichana wa kazi za ndani????
hulazimishwi kuamini we potezea yakikukuta nawe utakuja huku mbona inaeleweka vizuri au hujawahi ishi uswaz???????????? Tunamuelewa mtoa mada vizuriiii
 
Yuko MH mmoja aliwahi kuwa waziri enzi za Mwalimu,
Ma HG wake wote ambao ni 5 amewasomesha mpaka kidato cha 6

Si hivyo,
Enzi hizo miaka ya 90 alikuwa akiwapa Tsh25,000 wakati wengine wakilipa 2000.
Zaidi ya hapo alihakikisha kila mwezi anaweka 10,000 ili akifanya kazi miaka 3 mfululizo anaanza shule kama binti yake.

Watu wengi walimwona falla mkubwa.

Leo hii wale Ma HG wana kazi zao nzuri kabisa,
huenda kwake wakati wa likizo,
Ni bint zake nao wanamwona ni baba yao.

Mabinti 4 ni Wahehe 1 ni mrangi

inataka moyo lakini.

Kodi zetu hizo, ha ha ha haah! Nasikia wanapewa hadi posho za wakata majani ya ng'ombe hata kama hawafugi!
 
kuna nyumba fulani walikuwa wanalishwa nyama za watu bila kujua..........siku moja yule mama akamleta mchungaji nyumbani kwake H/G wacha apandishe na kuanza kutoa siri.

mimi nadhani ukimpata tu H/G unamwitia mchungaji au unampeleka kanisani akaombewe mana ni hatari................na tuwe na utaratibu wa kusali usiku majumbani kwetu na kama unaweza mwagia nyumba yako kwa maji ya baraka kabla ya kulala unapita kila chumba unamwagia maji ya baraka na kusali.

Wewe mwenyewe hapo ulipo huna idea na maombi, ila unacreat maombi kwa HG. You must be kidding. Swali kabla ya kuswaliwa.
 
Wewe mwenyewe hapo ulipo huna idea na maombi, ila unacreat maombi kwa HG. You must be kidding. Swali kabla ya kuswaliwa.
ulivyoongea as if unanijua kiundani sana.........embu isome vizuri hiyo post uliyoni quote mana ndivyo uwa nafanyaga.
 
Ndugu Liverpool,

Hii taarifa yako inaonekana ina mapungufu makubwa-kama ya kutunga vile!!! Je housegirl zaidi ya kukutwa akiwa uchi sebuleni alikuwa akifanya nini? Nina maana ni kitu gani kilifanya wenye nyumba waseme anawanga? Je, haiwezekani kwamba alikuwa kwenye ndoto? Suala la kuwa uchi inawezekana alilala bila nguo na alioanza kuota akaamka na kutoka kama alivyokutwa. Je ni madhara gani aliyoleta zaidi ya hadithi za milango kukutwa wazi? Je kukutwa kwa huyo Housegirl ambaye mwandishi wa habari hii hautueleza hata hicho alichokuwa akibwabwaja, inatosha kutuambia tujiadhari na wasichana wa kazi za ndani????

Je hakuna uwezekano kwamba hapo sebuleni alikuwa na baba mwenye nyumba au kijana mwingine; vile vile tukumbuke kwamba hawa wasichana wa kazi katika baadhi ya nyumba hutendewa vibaya na wanaume (baba au watoto).
 
sie huwa tuna utaratibu HG siku ya kuja anakaguliwa vitu alivyo navyo na siku ya kuondoka pia.na huwa tunapenda kujua kama ana ugonjwa wowote wa kudumu au ana mambo ya kimila.sasa kuna huyo binti alitokea Tanga.kwa kweli aikua anafanya kazi yake vizuri.na kwetu huwa mambo mengi yanafanyika kifamilia zaidi.muda wa kula tunakula wote pamoja isipokua mchana kwani yeye anabaki peke yake na watoto nyumbani.tukitoka matembezi tunatoka wote.sasa kuna siku wife alikua anatafuta nguo za mtoto,katika pekua pekua kwenye chumba chao,mara akakuta Bonge ya hirizi,mara kakuta simu,kumbuka wakati anafika hakuwa na simu na wala hakuwahi kutumia simu sisi tukiwepo hata siku moja.Simu haikua issue sana ila ilitujuza kwamba kuna mtu huwa nakuja pale nyumbani sisi tukiondoka.maana kwa mazingirayalivyo huwa hawezi pata muda wa kutoka labda tukiwa mapumzikoni week end.
sasa alipohojiwa kuhusiana na ile hirizi akawa speechless.hatukumaliza ile siku tukapigiwa simu na shangazi mtu akimtaka binti arudi kwao haraka sana kwani baba yake anamuhitaji."What a coincidence"Tukawaomba watupe muda ili tutafute mwingine,hakikueleweka.Keshao yake tukabeba watoto kupeleka kwa bibi yao na yule binti tukamrudisha.
Kwakweli ile kitu ilinikatisha tamaa sana ya kuwa na mabinti wa kazi.
 
Watu wengi huwa nyanyapaa watumishi hawa,
na kuwafanya second class citizen.
Kuna wenye nyumba ambao huwageuza nyumba ndogo,
tena kwa kuwabaka.
Huwafanyisha kazi masaa 24.
Hakuna mikataba,
siku zote hupunjwa ujira.

Wakati mwingine hutaka kuondoka kwa sababu ya unyanyasaji na kukataliwa kuondoka au kurudishwa na hatimaye huamua kufanya visa ili waweze kurudishwa kwao. Eneo ninaloishi kuna jirani yangu kamtoa binti kwao Kigoma na binti baada ya kufika hajaridhishwa na jinsi anavyotumikishwa na sasa anataka kurudi kwao, lakini huyo aliyemleta anakataa kumrudisha. Bahati mbaya kwamba hajui hata stesheni ya reli ilipo. Katika hali ya namna hii binti anaweza kuleta kituko chochote kwa ajili ya ukombozi wake.
 
Mi nimeshaamua mahousegirl no kwa sasa. Kila ukirudi nyumbani ni kelele weee hakuna hata zuri wanalofanya, wanajua kupika na kudeki, kuosha vyombo basi tena ili mradi. Ukikagua nyumba chafuuu, vyombo vyenyewe vichafuu, chakula yenyewe basi tu, hafu namlipa. Nimeona ni ujinga tu. Bora kuwa mwenyewe, maisha yanaenda.
Likija suala la watoto nitatafuta namna ya kuwahudumia. Hawa wasichana wana matatizo mengi.
 
cheichei2010 Yani kuna tukio lingine nimeambiwa kuhusiana na hawa H/G ila hakika kama nilivyoelezwa kwa kweli wanakatisha tamaa kama hauna Imani vizuri!
 
Last edited by a moderator:
Yuko MH mmoja aliwahi kuwa waziri enzi za Mwalimu,
Ma HG wake wote ambao ni 5 amewasomesha mpaka kidato cha 6

Si hivyo,
Enzi hizo miaka ya 90 alikuwa akiwapa Tsh25,000 wakati wengine wakilipa 2000.
Zaidi ya hapo alihakikisha kila mwezi anaweka 10,000 ili akifanya kazi miaka 3 mfululizo anaanza shule kama binti yake.

Watu wengi walimwona falla mkubwa.

Leo hii wale Ma HG wana kazi zao nzuri kabisa,
huenda kwake wakati wa likizo,
Ni bint zake nao wanamwona ni baba yao.

Mabinti 4 ni Wahehe 1 ni mrangi

inataka moyo lakini.



Mungu amjalie sana! Hakika thawabu amepewa.
 
Naomba waTZ tuache kuwa watu wa kulaumu na kuwasimanga watu wengine kwa kukosa maarifa. Tunahitaji kubadili mtazamo pale ambapo tunaona eneo fulani kuna udhaifu basi ni vyema kutafuta jinsi ya kuboresha. Hawa wasichana wakutusaidia nyumbani hatuna jinsi tunawahitaji, yule anayesema kwamba hahitaji msaidizi basi atakuwa bado hajawa na familia (watoto). Nafikiri jambo la msingi kwetu sote ni kuliona jambo hili kuwa ni changamoto na kutafuta njia mbadala ya kutatua tatizo hili; mimi nikiwa kama mjasiriamali nimeona hii ni fursa ya biashara kwa kuanzisha chuo cha mafunzo ya mhudumu wa ndani (Housemaid Training School) na vile vile unaweza kuwa wakala wa hawa wahitimu kwa kuwatafutia kazi. Tunahitaji kuboresha maisha yetu sote, tutakapofanikiwa kuwapa maarifa hawa watumishi basi tutakuwa tumeboresha maisha ya familia zetu.
 
Back
Top Bottom