Tahadharini na wafanyakazi wa ndani,H/G!

True story hasa ma-Mercury(Hg) wa Iringa na Morogoro ni wanga sana!

Uchawi hauna kabila. Mimi mwenyewe yamewahi kunikuta. Nilikuwa na bahati mbaya ya ajabu kuwa na ma-HG watatu mfululizo wote wachawi. Wa kwanza alikuwa msukuma, alikaa kidogo na tulipomgundua na kuanza kumpeleka kwenye maombi akatoroka. Wa pili alikuwa Mnyaturu kutoka Singida. Huyu alianza kujieleza mwenyewe kabla hata hatujamgundua. Tulimpeleka kwenye maombi lakini ilipokaribia kufunguliwa naye akatoroka. Huyu alikuwa kila siku usiku anakwenda kwao Singida na kurudi. Alikuwa anachanjwa mwili mzima bila kumuona mchanjaji. Siku nyingine alikuwa anapigwa mihuri ya moto bila kumuona aliyempiga. Tulipomdadisi sana akasema kuwa bibi yake ni mchawi na anataka kumkabidhi vibuyu japo yeye hataki. Naye alipoona maombi yamezidi akatoroka. Wa tatu ndiye alikuwa balaa kabisa. Huyu alikuwa mchaga. Nusura aniulie kijana wangu wa sekondari. Tulipomgundua alikiri na kuweka ushahidi wa maandishi jinsi ambavyo anashirikiana na wachawi akiwemo mama yake mzazi, jinsi wanavyofanya kikao usiku nyumbani kwangu, na hata aliwataja watu wa huko kijijini Moshi ambao wamewala nyama. Pamoja na kumpeleka maombi, ilinitisha nikaamua kumrudisha kwao.
Nimewahi pia kukaa na ma-HG wa Iringa na Morogoro na walikuwa wasichana wazuri tu, wala hawakuwa na mambo ya kichawi. Sasa hivi nina Mgogo and she is okay kwa kweli namshukuru Mungu. Lakini kabla yake nilikaa mwaka mzima bila HG kwa kuwaogopa. Cha muhimu ni kuwa tu waangalifu na kujitahidi kuwachunguza kwa kina na siyo kuwaamini asilimia mia moja.
 
mie kwa sasa sitakikabisa habari ya hg.....
Wa mwisho nilikuwa namlipa mshahara mkubwa...
Matibabu juu yangu...
Kila weekend yupo off.....
Vizawadi....
Likizo nampa n hela ya kuwaachia kwao....

Kaishia kuniibia.....
Pumb*****u kabisa.........
 
Ndugu Liverpool,

Hii taarifa yako inaonekana ina mapungufu makubwa-kama ya kutunga vile!!! Je housegirl zaidi ya kukutwa akiwa uchi sebuleni alikuwa akifanya nini? Nina maana ni kitu gani kilifanya wenye nyumba waseme anawanga? Je, haiwezekani kwamba alikuwa kwenye ndoto? Suala la kuwa uchi inawezekana alilala bila nguo na alioanza kuota akaamka na kutoka kama alivyokutwa. Je ni madhara gani aliyoleta zaidi ya hadithi za milango kukutwa wazi? Je kukutwa kwa huyo Housegirl ambaye mwandishi wa habari hii hautueleza hata hicho alichokuwa akibwabwaja, inatosha kutuambia tujiadhari na wasichana wa kazi za ndani????

Ona hili tutusa nalo!
 
we acha tu......kuna mwingine yeye alikuwa anasafirisha chakula.......utakuta baada ya wiki kila kitu kimeisha wanashangaa hivi vitu vimeishaje kumbe H/G anapeleka kwao kubanwa ndo akasema hivyo.

haya mambo acheni kabisa ni hatari sana.
Kwa kweli ukipata HG mzuri inabidi ushukuru Mungu
 
Iweni makini na HG's au HB's...ni vyema kujua historia na familia zao.
 
Haya mambo yapo sana. Wengine ukiweka Emmanuel TV wanaweweseka
 
Kwa kweli ameng'ang'ana ya kwmb ndiyo kazi yake ktk anga hii anayoishi.

Ameongea mengi sana hasa akisimamia anavyotumika nyakati yote hapo kuzimu na hata anavyosababisha ajali na kuua watu wasio na hatia kwani kule wanapoishi wanakunywaga damu za watu kila siku.

Asubuhi amepumzika ila mtumishi huyu wa Mungu amedamkia naye hapa akimwaga injili balaa na hata huyo H/G ameshatadharisha kitambo ya kwmb hawaogopi chochote zaidi ya wokovu tu!

Ntarudi na mengi aliyoyasema kwani hakika tusipokuwa na Imani tutadidimizwa na mwovu shetani!
Nauliza tu. Watu wanojiita watumishi wa Mungu wako kibao na kila siku wanamwaga NENO na kukemea mapepo, n.k. Mbona basi kwa taarifa zenu hizo nguvu za giza ni kama zinaimarika badala ya kupungua? Au zikipungua ajira za watumishi wa Mungu zitaota mbawa? Nauliza tu.
 
Watu wengi huwa nyanyapaa watumishi hawa,
na kuwafanya second class citizen.
Kuna wenye nyumba ambao huwageuza nyumba ndogo,
tena kwa kuwabaka.
Huwafanyisha kazi masaa 24.
Hakuna mikataba,
siku zote hupunjwa ujira.
Ndiyo. Kuna upande wa pili wa sarafu. Akina dada wengine hata kulea watoto wao hawajui wanawaachia ma HouseGirl. Haiwezekani huyo binti kutokana na uchovu au mkanganyiko wa mawazo (baadhi wananyanyaswa kweli kweli) alikuwa anatembea usingizini (sleep walking). Hizi conclusions walizofikia zina kasoro kwa maana binti anaweza kuwa mgonjwa anahitaji msaada badala yake anazushiwa uchawi. Je, mmempeleka kwa mtaalamu wa saikolojia ili amfanyie uchungzi wake kiakili? Mimi nasema 'Watumishi wa Mungu' wanaeneza ushirikina na siyo imani kwa Mungu wa kweli. Yesu hakutembelea Prado au kusaka utajiri.
 
Update:

Baada ya mzunguko wangu wa kutwa!
Nilirudi na nikatamani nipate kujue kilichojiri baada ya ile songombingo ya yule H/G.

Habari nilizozipokea toka kwa mama mwenye nyumba ni kwamba baada ya ile tukio mama mzazi wa yule H/G amepiga simu toka Mkoani Dodoma na kwamba anamwomba mtoto wake mara moja.

Na ndipo jioni ya leo msichana yule amelala kwenye basi la Arusha - Dodoma na tayari kuelekea kwao.

Nikasema ngoja niwajuze ndg zanguni nanyi mjue yaliojiri tangu muda ule mpaka sasa!

Huyo ndio H/G! Kazi kweli kweli!

Muwe na wakati mzuri pale popote mlipo!
 
yaani hivi vichwa mnavichosha mno, mbona shida ni nyingi mno kuanza kufikiria HG anawanga?

Awange tu, mie hanihusu
 
Naomba waTZ tuache kuwa watu wa kulaumu na kuwasimanga watu wengine kwa kukosa maarifa. Tunahitaji kubadili mtazamo pale ambapo tunaona eneo fulani kuna udhaifu basi ni vyema kutafuta jinsi ya kuboresha. Hawa wasichana wakutusaidia nyumbani hatuna jinsi tunawahitaji, yule anayesema kwamba hahitaji msaidizi basi atakuwa bado hajawa na familia (watoto). Nafikiri jambo la msingi kwetu sote ni kuliona jambo hili kuwa ni changamoto na kutafuta njia mbadala ya kutatua tatizo hili; mimi nikiwa kama mjasiriamali nimeona hii ni fursa ya biashara kwa kuanzisha chuo cha mafunzo ya mhudumu wa ndani (Housemaid Training School) na vile vile unaweza kuwa wakala wa hawa wahitimu kwa kuwatafutia kazi. Tunahitaji kuboresha maisha yetu sote, tutakapofanikiwa kuwapa maarifa hawa watumishi basi tutakuwa tumeboresha maisha ya familia zetu.

Ni kweli itawasaidia sana. Kuna watu ambao walikuwa ma-HG lakn wameweza kuwa na nafasi zao. Kwa mfano TV presenter Irene Kiwia, and shez proud to tell her bacground and the achievements she has. Wapo wengi ambao waajiri wao waliwapa nafasi za kujiendeleza.
Yote kwa yote adha za wasichana wa kazi najizua. Lakn yote tisa kumi HG kumleta mvulana ndani kila unapoenda kazini halafu kijamaa kinanjunja na kupikiwa ugali kama yy ndo baba mwenye numba. Gghhh(hasira manake)
 
sorry kwa kupindisha mada hivi ni lazima tuwe tuna ajiri house girls mbona wenzetu wa nchi zilizoendelea huwa hawana house girl wanawajibika wao kama wao? na kama unaenda night shift ndio unamlipa mtu kuna watu special wa kufanya hiyo kazi tena unamlipa kwa masaa sasa huku unakuta mke ni golikipa ila bado anahitaji house girls ebu niambieni hapa pamekaaje wakuu? ina maana sisi tuna kazi nyingi sana au,
 
Nauliza tu. Watu wanojiita watumishi wa Mungu wako kibao na kila siku wanamwaga NENO na kukemea mapepo, n.k. Mbona basi kwa taarifa zenu hizo nguvu za giza ni kama zinaimarika badala ya kupungua? Au zikipungua ajira za watumishi wa Mungu zitaota mbawa? Nauliza tu.

Zinahamia kwa watu wengine nguvu hizo za shetani (mapepo) haziwezi kuelea hewani.
 
Huyo mchungaji naona amepata sehemu ya kujichukulia maujiko. muda si mrefu watz watamfungia safari kwenda kutolewa mapepo. Kikombe cha babu kilianza hivi hivi.
 
Back
Top Bottom