Tahadhari ya Polisi na RC Morogoro kuhusu Hukumu Kesi ya Uchaguzi kesho

Wanaintelegensia Kali sana hawa polisi watakuwa wamepata taarifa za kiintelejensia kuhusu hukumu ya jaji itakavyokuwa hiyo kesho! Tehe only in Tanzania
 
Hakuna tofauti na vjarida vya bongo wenyewe tunaita magazeti! hakuna hata mmoja anayesema kama ushindi unapokwa nini kifanyike! Wote mnalalama kwa kutoa sifa tu! Eti huenda imeshajulikana so what?
 
1469736988255.jpg
 
Amani iwe kwenu wakuu,ile kesi ya ubunge iliyofunguliwa Morogoro dhidi ya wabunge wa CHADEMA inatarajiwa kutolewa hukumu kesho.Lakini cha kusikitisha ni kwamba kesi hizo ni kama zishaamuliwa kwa sababu mkuu wa jeshi polisi mkoa wa Morogoro amemwaga askari hali ambayo sio ya kawada sio kwamba kuna kitu kimejificha.

Mkuu wa mkoa ambaye pia ni kada wa CCM ametoa amri kuwa wananchi wasifike mahakamani kusikiliza kesi kinyume na taratibu zilizowekwa.

Swali la kujiuliza kwanini wanamwagwa askari wengi namna hii?

Kwanini mkuu wa mkoa ametoa onyo wananchi wasijitokeze kusikiliza hukumu hiyo?? Kuna kitu ambacho kinaendelea kuna uwezekano kabisa refa ashapanga matokeo kabla timu hazijaiingia uwanjani,hivyo wapenda demokrasia hili jaribio lingine la ubakwaji wa demokrasia.

Kwa hiyo uchaguzi unarudiwa?
 
Magufuli alisema hapendi siasa

Mbna anaetembea kwenye viatu vya Kikwete tu

Hizi kes zimekaa kisiasa sana, nyuma ya pazia kuna mengi yanaendelea
 
Wew jinga kabisa mahakam ndo itoe tahadhari....ivi umeandika mwenyew au umeandikiwa unatia kinyaaa
 
Hii kesi inavutia hisia za wananchi,ni uamuzi kuhusu kura walizopiga kuchagua wabunge wao. Kisutu mbona watu wanajaa lakini haijawahi kutolewa tahadhari kama hii? Kazi ya polisi ni nini?
 
Yawezekana jamaa wanajua mwenendo wa kesi,kinadharia tuiache Mahakama iamue kwakuwa ni jukumu lake kutoa Haki.Japo kwa kauli za viongozi zilizotolewa ni tata.
 
Sasa tukio linalotokea morogoro,linamfanya mghana adharauliwe kwanini?
Hao wa Ghana unaowasema mpaka baada ya kunukishana kwanza ndipo akili za viongozi zilipokuwa sawa na kujiwekea mfumo mzuri wa kuongozana. Africa walio ktk uongozi hujiona Miungu watu na watawala. (Hii ndio shida ya Africa )
 
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro leo limetoa tahadhari kuwa halitasita kuchukua hatua kali kwa vikundi vya wanasiasa vitakavyokusanyika kesho kwenye mahakama ya Morogoro kusikiliza hukumu ya keshi ya uchaguzi kwenye majimbo ya Kilombero pamoja na Mrimba ambapo hukumu zote mbili zinatolewa Ijumaa wiki hii.

Wakati Polisi ikisema hivyo, RC nae amesema yoyote ambaye kesho hatakubaliana na uamuzi wa mahakama kuu akakate rufaa na asilete manung'uniko yasiyotarajiwa na wala asifanye mkusanyiko wowote ule kesho Ijumaa .

Kauli za wote hawa wawili binafsi zinanipa shaka kuwa kulikoni waanze na tahadhari za aina hii na kujipanga mapema kuonya wanasiasa kwa hukumu ambayo haijatoka. Je wanajua hukumu ina nini ndani yake hadi wameamua kutoa tahadhari hii?

Kwanini Mahakama isitoe tahadhari badalala yake Polisi na RC ndio watoe tahadhari hii? Kwanini itokee Morogoro tu na haijawahi kutokea mahala pengine popote tahadhari za aina hii?

Nimejiuliza sana na kesho nategemea bao la mkono Mahakamani.
Ni jukumu la vyombo vya usalama kutoa tahadhari hasa pale ambapo kuna mazingira ya uvunjifu wa amani
 
Back
Top Bottom