Tahadhari: Mlimani city eneo hatari kwa usalama wa raia

Jamani!. Ni leo tuu asubuhi jamaa yangu kaniambia jana wamelizwa lexus yao mpya hapo Mlimani City, wameingia tuu ndani, within no time, wametoka, gari halipo!.Kwenye huu wizi wa hili gari jana, kuna ama good news inakuja, ama bad news inakuja, nitawaupdate ikifika.Sasa wanapaharibu, mimi niliumizwa na kitu kidogo sana, fake na conterfeit perfums kwenye maduka ya hapo!. Nilichoka kabisa, tena duka lenyewe mpaka wana testers kuthibitisha genuinity, kumbe...


nilinunua perfume ya 212 men na ilikuwa feki bora za mtaani na cha kuumiza zaidi nilitoa laki na buku tano...
 
nilinunua perfume ya 212 men na ilikuwa feki bora za mtaani na cha kuumiza zaidi nilitoa laki na buku tano...
tehe tehe pole sana...siku zoote nasemaga vitu vya malls ni fake...sema wabongo wanaona prestige fulani kwenda malls hasa mlimani city kufanya shopping.....

anyways majuzi waliniliza side mirrors mbaya zaidi gari niliazima.....
 
Lakini hapo si kuna ulinzi imara? Hao askari kazi yao nn? Wanauza sura tu?
Kuna kijamaa kama kipemba hivi white hicho balaa kitaalamu cha kupiga vitu vya escudo hapo hapo.
Hii kazi pale ndo mahala pake haswaa.
Kitu kibaya ni kuwa wale walinzi wanashirikiana na jamaa wanaoiba maana mara zote ndio wa kwanza kufanya checking gari inapopark.Kuna rafiki yangu aliibiwa laptop baada ya dirisha la hardtop yake kuvunjwa. Nikajiuliza wale walinzi walikuwa wapi?
This is something of serious concern maana wengine tukipata tu vijisent pale ndo tunapouzia sura.
 
tehe tehe pole sana...siku zoote nasemaga vitu vya malls ni fake...sema wabongo wanaona prestige fulani kwenda malls hasa mlimani city kufanya shopping.....

anyways majuzi waliniliza side mirrors mbaya zaidi gari niliazima.....

Pole sana kamanda!!!!!..Ulikuwa na miadi na shori nini,maana nasikia siku hizi vijana Dar meeting point ni Mlimani City,Samaki Samaki sijui
 
Pole sana kamanda!!!!!..Ulikuwa na miadi na shori nini,maana nasikia siku hizi vijana Dar meeting point ni Mlimani City,Samaki Samaki sijui
yah man pale ndio meeting point ya vitoto visivyojua starehe.....mie pale sio kiwanja changu man.....siwezi nunua kitu buku 2500 wakati kitaa shing 1500...na huduma nyingine bureeee
 
yah man pale ndio meeting point ya vitoto visivyojua starehe.....mie pale sio kiwanja changu man.....siwezi nunua kitu buku 2500 wakati kitaa shing 1500...na huduma nyingine bureeee

Nilitaka kushangaa aisee
 
Ndugu watanzania leo nawaambia hii kitu inatokea lakini sasa hivi is too much,eneo la kibiashara la mlimani city ni hatari sana kwa wizi wa magari,side mirrors na vifaa vingine vya magari…..watu kibao wamelizwa hata sasa hivi ninavyopost kuna mtu analizwa……
Ukiacha mkoba,laptop au kitu kingine ndani umeliwa!!! Wale jamaa ni soo ukifika pale kuna watu wana ku monitor mmoja anakufuatilia kila hatua unapokuwa ndani ya malls akiwasiliana na wengine kwenye parking ambao kazi yao ni kuchukua wanachokitaka……watu wamelizwa mpaka magari…. Afu kuna vijamaa vinasimama jukwaani vinasema Tanzania amani tele…..kudadadeki amani gani watu sasa wakija na magari yao wanang’oa side mirrors na kuingia nazo ndani wakiogopa kulizwa?
Anyway ninachowaambia mkienda Mlimani city na motokaa zenu muwe makini……Hivi nani anahusika na ulinzi Mlimani city?

Mweee asante kwa taarifa wengine twapaki vikoko vyetu halafu twasepa mitaani duh ingekuwa Kufa kwa Nyani.....
 
Mie nilishastuka siku nyingi, hakuna parking iliyo safe saaaana Dar kama hujachukua precautions. Nikifika Mlimani City (sitaacha kwenda) napaki gari, namtafuta mlinzi, namkabidhi mia tano. Mchawi mpe mtoto alee ati.Nikirudi namkuta mlinzi yupo palepale na mchuma upo vile vile. Akili kumkichwa Bongo hapa.
 
Hili tatizo ni kubwa sana na linaendelea kukua siku baada ya siku mbaya zaidi ni hakuna effort yoyote inayofanyika kulitatua. Hawa makaburu wasipoangalia hata biashara yao inaweza shuka kwani ni bora mtu akapaki gari yake na kufanya shopping sehemu ndogo lakini safe na una uhakika.

Vigari vyenyewe nya bongo vya mawazo halafu wanakongoloa si aibu kabisa. Ukipita barabarani gari nying sasa hazina sight mirror mtu uko barabarani mara unashangaa wa mbele yako kaingia site yako kisa sight mirror wameramba
 
Kuna wale walinzi sijui ni wa kampuni gani maana kazi yao ni kukusanya na kugawa vijikadi tu badala ya usalama wa raia na mali zao... ni bora tungejua moja kuliko kuwa na kampuni za ulinzi feki kama ile ya mlimani city

Wengi wa vibaka wale ni madeiwaka wa mwenge na ubungo na utawaona wana simu na wana mtandao makini sana kwani wengine huwa kwenye milango ya kuingilia, wengine ndani na wengine kwenye parking... pia kuna wanawake wanahusika kwahiyo utaona watu wamebana kwenye mwisho wa fence ukidhani ni wapenzi kumbe wako kazini

Mlimani city is slowly turning into a crazy unsafe investment
 
Kwani hakuna sehemu nyingine za kupumzika mpaka Mlimani CIty?...

Anyway, kwa wizi pale Mlimani ni mfumo mzima. Nakumbuka yupo kijana alikuwa anafanya kazi katika duka fulani pale Mlimani City na ukienda ana kueleza kuwa anaweza kukuchomolea "kamera, flash disk, na chochcote unachotaka katika duka hilo la Wahindi na kukuuzia kwa bei nafuu (brand new laptop 300,000Tshs unapata).... Baada ya miezi fulani nikaja kumkuta yupo getini kama mlinzi wa kampuni ya fulani, nikamuuliza vipi tena, akasema ameachishwa pale dukani kwa wahindi kwa tuhuma za "kuchomoa" "Laptop,lakini jamaa zake wamemsukia kapata ya ulinzi sasa.

Kudadadeki,...kuna ulinzi hapo?. Ni bora upaki ng'ambo ya pili gari laweza kulala siku nzima.

Kuna machariii (wa kike na kiume) wanashinda pale kwenye vibaa toka asubuhi mpaka sita usiku kila siku, hawana mwelekeo, wakikufahamu stori nyiiingi za kutaka pombe, Baadhi hawa ni watoto ambao walikuwa wakiishi kinyume cha Sheria katika nchi za Ulaya na Marekani wakisema wao "wana kula Bata" lakini baada ya kushindwa maisha au kurejeshwa, wamepoteza kabisa mweleke wa maisha na Mlimani City ndo imekuwa kijiwe chao!...ni haya maisha ya kujifanya upo ulaya muda mrefu wakati kazi unayofanya haileweki, na unaporejea nyumbani wenzio una wakuta wapo mbali unashindwa kujichanganya uishi vizuri na kujenga nchi, unataka kuishi maisha ya kutoonekana hujachoka!, lakini bdo unataka "miteremko" kupitia migongo ya wenzio.

Hao ndo wezi mashuhuri pale Mlimani City na kwingineko, wanaishi kwa "vichanjo" (wizi wa kutumia Debit/Credit cards)"....ukiwaona unawajua tu, ni malimbukeni fulani, ana nguo tatu alizotoka nazo nje na manukato (prefumes) kibao mwilini, kuongea kwiiiingi habari za ulaya au Marekani kumbe hakuwa hata na issue huko!....
 
bongo kuna vituko!mwanzo walikuwa wanavunja nyumba kuiba music systems,then wakaanza kuiba TV sets,baada ya hapo wakaanza kukwapua simu,wakahamia laptop,sasa hadi side mirrors na locks!duh
 
bongo kuna vituko!mwanzo walikuwa wanavunja nyumba kuiba music systems,then wakaanza kuiba TV sets,baada ya hapo wakaanza kukwapua simu,wakahamia laptop,sasa hadi side mirrors na locks!duh

Haya mambo yapo dunia nzima na wewe sio tunadramatize bongo kila kitu mazee.... Paris mpaka sandwich wanaikomba ukiwa kwenye pikipiki
 
Jamani mbona kila mtu anaita mlimani city ni Makaburu!! ninavyojua mimi pale kuna maduka mengi sana pamoja na sinema ni za watanzania, sasa hili la makaburu limetoka wapi? labda shoprite, Mr Price na...
Kuhusu tatizo la wizi ni linatokana na njaa, watu sasa hivi wana njaa sana, hawajui watakula nini? kwa hiyo hakuna jinsi lazima tu wataiba wapate ku survive, na tujiandae na wimbi kubwa la wizi katika maeneo yote, chanzo cha yote haya ni mgawanyo mbovu wa rasilimali za nchi yetu,uongozi wa juu wote ni wasanii
 
Huu ni mfano tuu wa maisha ambayo watanzania tunayaendea kwa kuimarisha ubepari na kuwatuuza mabepari kama mlimani city mnowaita kwa jina la kuwapamba eti wawekekezaji. Hili ni eneo la matumizi kwa wenye nazo wasio stahili kuchagnyikana na sisi kwani sisi ni masikini na maisha yetu ni ya kishenzi. Bahati mbaya , masikini ni wengi na ukiwaita au kuwafan ya washenzi hatima yake ni hayo yanayo tokea. Keki ya taifa ni lazimaau vema iliwe au kugaiwa kwa watanzania wote bila ubaguzi. Kinachotokea ni kwamba wachache ambao ni matajiri(mabepari) wana faidi vyote nchini na wengi ambao ni masikni wanashuhudia tu ingawa wakishindwa hulazimika kujichukulia kwa nguvu zao(wanaiba). Tukumbuke hawa wawekezaji tuliwaita wanyonyaji ambao hutumia nguvu za masikini(vibarua/wafanyakazi wa bei poa),ardhi yetu (kamamlimani city),na rasilimali zetu nyingi na kodi sijui kama wanalipa. Eti utaratibu wa jenga, endesha na rudisha lini? Hatuja chagua maendeleo ila tumechagua kushuhudia maendeleo ya wenyewe mabepari(wanyonyaji) mnao waita wawekezaji. Nakumbuka marehemu J.K.Nyerere, Chachage,Lenin, Karl Marx na sasa Obama wanao sisitiza maendele lazima yawe ni ya watu (watu wengi/majority). Tanzania tutaendelea kushuhudia maendeleo na zaidi kufanikisha maendeleo ya watu hasa wage na wasomi wachache wakiwemo wafanyabiashara/mabepari waTZ lakini tukiendelea kuumia kwa umaskini wetu. We need change.
 
Back
Top Bottom