Eeh! M/Mungu naomba uwezo wa kubadili yanayowezekana na kukubaliana na hali kwa yasiyowezekana

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
424
1,044
Kuna siku nilikuwa nimekaa kwenye Gari ya mizigo naelekea sehemu dereva alikuwa mzee mmoja wa makamo. Kwa haraka haraka mzee anamiaka 50s ni dereva wa magari. Story ilianza kimasihara tuu. Kwani tukiwa tumetulia eneo changamfu sana pale Ushirombo maemeo tulipokuwa tumekaa kwa wenyeji wa huko watapajua panachangamka sana usiku hata mchana siyo sana kivile kuliko usiku. Na pale tulipokuwa ni barabara kuu kamanunaelekea Kigoma, Bukoba, Rwanda na Uganda ni njia maarufu sana pale magari yakiwa yametoka masafa kama anataka kupata chochote atapaki barabarani na kupata chakula kwa ajili ya kuendelea na safari yake. Tukiwa tumekaa na mzee huyo mara zikapita gari za kifahari Lilipita gari aina ya Toyota Hilux nafikiri ni gari kama milion 95s au zaidi. Akaniambia "Kijana wangu"

Unaweza kuamini na mimi nilikuwaga na ndoto za kumiliko hiyo chuma? Nilijisikia vibaya lakini nikamwambia mbona bado sana mzee endelea kuwa na subra! akaniambia hapana kijana wangu ukifikisha miaka 50 kama mimi hujaweza kutengeza ndo umepotea hapo.

Lakini aliendelea kuongea maneno ambayo yalinitesa kwa kiasi kwamba niliona hata ile story imekuja vibaya kwani niliona kama ananiongelea mimi.

Nikaendelea kusikiliza story hii ni kweli au mzee ananipanga ngoja nimsikilize. Akacheka baadae akajisemea kwa umri wangu mimi hapa sasa napambana tuu ili nile nife. Hata wazo la Hilux sina tena yaani mimi nikitoboa sana labda nijinunulie simu ya "Touch" yaani hapo ndo nimekomaa sana au nijenge walau nyumba ya room 3 za tofali hapo kweli nitaona nimefika mbali.


Aliendelea kuongea akasema "Kijana wangu zamani watu walikuwa wanasema siijui kesho yangu sijui itakuwaje lakini siku hizi maisha yamebadilika kiasi kwamba huwezi fikiria kesho tena unafikiria leo nitatoboa?. Akaniambia kwa mfano mimi ni dereva. Napambana nisomeshe, watoto wale


Lakini unashangaa napambana ikifika jioni napigwa faini ya elfu 60 hapo boss hataki kujua hivyo kama nilikuwa na akiba kidogo inabidi nikaichukue nilipe faini... Kama sina napunguza kidogo kidogo mpaka wiki iishe ile namaliza wakati mwingine unapigwa faini nyingine. Kutokana na

maelezo yake sikuweza kumuuliza ni aina gani ya makosa anafanya zaidi lakini aliongea kwa uchungu akisema

"Mdogo wangu tunakusanya kwa shida sana lakini kuna watu wanamishahara yao karibu lakini 7 kila mwezi lakini wanataka hata kile kidogo chetu"

Kwa akili yangu nilielewa tuu anamaanisha nini sitaki kuingia ndani zaidi. Niliendelea kumsikiliza akasema sasa hivi unaona vijana wanaamka asubuhi wanaondoka home usifikiri wanaenda popote? hakuna, ni kwamba wanahisi wakikaa hapo ndani watachanganyikiwa kwa mawazo wanasema heri wasogee mbali na home labda watakutana na riziki huko mbele ya safari.

Ila ukifuatilia mambo yamekuwa magumu sana. Akaniambia mfano mimi sasa nikapata mtu hata kama atanilipa laki 7 kwa mwezi sitokaa nikafanikiwa kununua hiyo Hilux lazima nikubali uhalisia. Mimi ninapokubali uhalisia haimaanishi kwamba

nimekata tamaa hapana bali inanipa amani ya moyo kwamba nisitamani mambo ambayo siwezi kuyafikia. Ile inanisaidia mimi kupunguza stress walau.

Nakumbuka mwaka 1992 niliwaza sana sijui niwe jambazi? ukicheki mwili pia na nguvu ninazo na akili ya kuwa jambazi ninayo na ningeweza kuwa jambazi.

Lakini nikafikiria kwamba nikiwa jambazi ninaweza kufa kifo kibaya sana ama nikaishi maisha ya wasiwasi kama ndege. Akanigeukia akaniambia hata wewe nakwambia hapa. Umependeza hivi sijui ukoje lakini je upo kwenye mfumo?

"Badala ya kujibu nikacheka" akaniambia wala usicheke ila kama haupo kwenye mfumo na wewe ile Hilux utaisikia tuu kwa washkaji na wazee wa TRA kama mimi yaani watu wa kwenye mfumo ndo wanafanikiwa hasa kwa sisi ambao tumetoka familia duni.

Yaani unakuta baba hakuwa na kitu chochote cha kukupa kuanzia elimu na uhuru wa kujipambania wala kianzio hupewi hapo kutoboa ni kazi. Alafu mbaya zaidi unakuja kupambana lakini mazingira yanakukatili. Yaani inakuwa kama umepambana kupata walau tone la maji jangwani lakini tone lile lina kaushwa na jua tena, ila kijana wangu wewe endelea kupambana sana ila uwe na adabu ya maisha pata muda na watu wa hali ya chini sana kaa nao hata Mungu akikusaidia ukawa mtu fulani mara moja mora njoo huku kwenye dala dala usikae kwenye V8 ukala viyoyozi maana hutojua tunapitia nini wengine

Ningeomba niishie hapa kwa leo. Ila niliondoka kwa yule mzee nikiwa nimeshika kichwa maana ni kama alikuwa ananifundisha maisha yakoje.

MWISHO NIKASEMA.
Eeh! M/Mungu naomba uwezo wa kubadili yanayowezekana na kukubaliana na hali kwa yasiyowezekana na pia naomba busara ya kujua tofauti kati ya hayo mawili.

Alionyesha kuwa mafanikio hayapatikani kwa urahisi na kwamba ni muhimu kutambua na kuthamini kile unachopata katika maisha.

Ushauri wake wa kujenga uhusiano na watu wa hali ya chini na kutambua changamoto zao ilikuwa njia ya kuelewa tofauti za maisha na kusaidia kuwa na mtazamo wa upendo na huruma kwa wengine. Alionyesha pia umuhimu wa kukubaliana na hali yako na kutambua mipaka yako ili kuepuka kutamani mambo ambayo huenda usiyaweze kufikia.

Mwisho wa mazungumzo yenu, uliomba uwezo wa kukubaliana na yale yanayowezekana na yasiyowezekana na busara ya kutofautisha kati ya hayo mawili. Hii inaonyesha kutambua umuhimu wa kuelewa hali na kujua jinsi ya kubadilika na kukabiliana na mazingira mbalimbali.

Ni muhimu kuchukua mafundisho haya na kuyatumia katika maisha yako kwa njia inayofaa kwako. Kumbuka kuwa kila mtu ana hadithi yake na changamoto zake, na kila mmoja wetu anaweza kujifunza kutoka kwa wengine na kuimarisha njia yetu ya kuelewa na kukabiliana na maisha.
 
Back
Top Bottom