Tahadhari: Kuweni makini sana na wahudumu wa bank

Hata mimi mara mbili nimekwenda kudepost kwa binti mmoja benki moja iko katikati ya jiji wakati nimezihesabu mwenyewe vizuri tu (mimi ni exbanker wa miaka ya 70 na 80 ) lakini yule binti a kaniambia hakuna elfu kumi mara mbili siku wa na jinsi nikatoa.
Mwaka 80 Mmmmh nina mashaka na kichwa chako, Unajua kuhesabu
 
Ni kweli Ndugu.unajua hata kiusalama ni mbaya sana kuhesabu pale kwa kipindi hiki kigumu si wajua wanaweza wakakukibiti!
....ona sasa!.unakubali kosa afu unakuja na excuse ya kijinga;kwahiyo unataka benki wakupe ulinzi?
..kama hukuhakiki hela yako,kiherehere cha kutuhumu watu umekitoa wapi?
..tukuamini tu wewe sababu u mtakatifu sana,ama?
 
Kweli wafanyakazi wa benki hasa NMB, wengi ni wezi, mimi mdogo wangu aliibiwa zaidi ya 2 M, NMB Kenyatta road ,amefuatilia mara ooh mhusika alihamishiwa Bukoba, NMB sio, umakini unatakiwa
 
ubaya wa benki,ukiwahi shtukia basi imekosewa lakini ukienda gundua baada ya kutoka benki imekula kwako!Kuna cashier wetu alishapigwa laki moja kwa kudhani tu benki hawawezi sahau/kosea mahesabu
 
Kuhesabu pale pale ni muhimu sana, lasivyo unapigwa. Kuna siku nilichukua ila machale yakanicheza, kutulia kuhesabu kwenye milioni 2 ikawa inamiss 20elfu. Nikamrudishia naye ahakikishe, kweli akakuta kiasi hicho kinamiss akaongezea. Ukizibeba tu kichwa kichwa inakula kwako.
 
Hilo suala LA kuchomekewa note pungufu liko sana kwenye mabenki hapa nchini , hasa benki ya makabwera inaongoza , ukichukua mzigo mrefu lazima ukute katikati kuna mashimo tu , na huwezi kuhakiki Pesa mfano 5M , unakuwa na haraka cha mhimu wahudumu waone aibu , ni bora waombe kuliko kunyofoa katikati na kubadilisha badara ya elfu kumi unawekewa elfu mbili.
Ni kweli pesa zikiwa nyingi ni ngumu kuhesabu na kuhakiki zote.
 
Nilipewa 20mil cbe zikiwa na yale makamba magumu
Nikaambiwa nipeleke crdb teller alipomaliza hesabu akanidai 20000 kuwa hazipo
Nilimlaani yule mtu hadi leo maana ilibidi mimi ndio niingie hasara kwani aliyenipa hela kapewa hela mapema benki ikiwa imefunguliwa
 
Pole mkuu, mie Barclays niiibiwa 100,000 na mbaba mmoja. NIitamani nimmeze kisha nimtapike. Yaani kuna wengine ni wezi ile mbaya. Usipokuwa makini wanakudonyoa hivi hivi tena na tabasamu usoni . Swines
 
Poleni na kazi,

Naomba nitoe angalizo kama kichwa cha habari hapo juu,

Jana nilikwenda bank moja pale Lumumba kutoa pesa kwa ajili ya biashara zangu. Nilikuta foleni kubwa pale kutokana na umuhimu wa Pesa nilikomaa ktk foleni kama masaa mawili hivi na nikafanikiwa kuchukua Pesa kiasi cha 3.5m.

Tatizo sikuweza kuhakiki pale pesa. Nilipofika tu sehemu yenye utulivu nikahakiki ile Pesa cha kushangaza katika millioni moja nilichomekewa na shillingi elfu mbili.

Je ni wangapi wanapigwa kwa mtindo huu?

Ahsante sana kwa tahadhari.
 
We jamaa nawe....elfu 2 ndo unaifungulia na thread kabisa.!??..Ile mlizoe kusema LAKI SI PESA?
 
Hilo suala LA kuchomekewa note pungufu liko sana kwenye mabenki hapa nchini , hasa benki ya makabwera inaongoza , ukichukua mzigo mrefu lazima ukute katikati kuna mashimo tu , na huwezi kuhakiki Pesa mfano 5M , unakuwa na haraka cha mhimu wahudumu waone aibu , ni bora waombe kuliko kunyofoa katikati na kubadilisha badara ya elfu kumi unawekewa elfu mbili.
anajua akiomba huwezi kumpa
 
habari zenu ndugu zangu.nampa pole sana ndugu yetu aliye ibiwa na bank teller hiyo 8000,ila naomba usimhukumu moja kwa moja huyo teller kwaani ina wezekana alifanya kosa la kiufundi kwenye kuset counting machine,yaani pesa zake alikuwa anahesabia kwenye "count mode"badala ya kuweka "cf mode" kwahiyo kama ailiweka count mode maana yake aliiruhusu machine ipitishe kila kitu bila kupembua chochote(yaani fake,iliyonusu,karatasi,of different denomination n.k) kwahiyo hapa inawezekana amepokea pesa toka kwa mteja,akapitisha kwenye mashine idadi ikasoma ziko 100 basi yeye akaamini kwamba zote ziko sawa kumbe haiko hivyo,na mwisho wa siku akitokeamteja anatoa(withdrawal) na akalipwa pesa zilezile alizopokea kutoka kwa mteja mwingine aliyekuwa anaweka(deposit) ndo kinatokea kama hicho kilichotokea kwa ndugu yetu.ikumbukwe mteja anajua yeye pesa ametoa benki kwahiyo shida yeyote ile atakayokutana nayo kwenye hizo pesa,moja kwa moja atamshuku teller, kumbe masikini ya mungu,hata yeye hakujua kama kuna note fake,au za denomination tofauti amebambikiwa.
nb ikumbukwe kwamba kama teller angetumia CF mode kuhesabu pesa zote anazopokea na kulipa basi hili suala lisingejitokeza.
swali:ni kwanini basi tellers wasitumie CF mode kuhesabia pesa?
jibu ni kwamba pesa zetu nyingi zinawahi kuchoka au kuchakaa,sasa ukiweka hii setting inawezakana kabisa kwenye note 100 za elfu kumi kumi zikapita note 20 the rest 80 zinakuwa rejected,sasa inabidi azirudie kwa mkono.fikiria una milion 3,kwenye hizo tatu,elfu kumi kumi ziko laki nane tuu,elfu tano tano ziko 600000,zilizobaki zote ni elfu 1000 na elfu mbili mbili na kila akipitisha kwenye mashine zinakwama au mashine ina stack pia ikumbukwe maximum time ya mteja kuhudumiwa na cashier ni 2-3 mins,hapo ndipo anapoamua kujiripua kwa kuiset mashine kwenye "COUNT mode " ili aweze kuhudumia wateja wengi zaidi.
ANGALIZO:kama una chukua kiasi kikubwa na wewe unaenda kulipa watu ni bora ukaomba upewe pesa ambazo zimefungwa na mikanda,pia hizi zilizofungwa na mikanda huwa zinakuwa na lebo juu yake,ile lebo inaonesha ni nani alizihesabu na kuhakiki,kwahiyo ukienda ukakuta kuna upungufu wa note kwenye hizo bundles unachukua ile lebo husika unarudi nayo bank kuwaambia kuhusu tatizo lako.ikumbukwe unaweza lipwa dirisha kwa cashier no 1 lakini kumbe hizo bundles zilihesabia siku 8 nyuma na cashier no 3.
NB:tunajua kwamba ukichukua 10m+ huwezi kuhakiki au comply na sheria ya count your money before leaving the counter"basi atleast hesabu hata migongo ili usije ukarudi kesho yake ukasema kuna upungufu wa milioni moja.
ni hayo tuu kutoka kwa ndugu yenu ex banker
 
Nimekuelewa mkuu
 
....ona sasa!.unakubali kosa afu unakuja na excuse ya kijinga;kwahiyo unataka benki wakupe ulinzi?
..kama hukuhakiki hela yako,kiherehere cha kutuhumu watu umekitoa wapi?
..tukuamini tu wewe sababu u mtakatifu sana,ama?
Naheshimu na wazo na mtazamo wako pia.sipendi wengine wapate tatizo
 
We jamaa nawe....elfu 2 ndo unaifungulia na thread kabisa.!??..Ile mlizoe kusema LAKI SI PESA?
Hapo kumbuka imepungua elfu8, mtu anayejua thamani ya pesa huwa anathamini hata shilingi 100, na ukifuatilia ndio huwa wanafanikiwa sana.
 
Back
Top Bottom