Kwa hili nililoliona, Wazazi kuweni makini sana kuweka uangalizi kwa watoto wadogo wa kiume

Von_Lufuta

JF-Expert Member
Mar 19, 2023
1,530
3,607
Habari zenu wakuu.. Hope mpo vizuri.

Bila kupoteza muda, Wiki 3 zilizopita nikiwa Mkoa X, nilikutana na tukio la kusikitisha sana. Sio mimi tu, hata watu wa mtaa ule wanawake kwa wanaume waliishia kushika vichwa na wengine kumwaga machozi kabisa.

Ilikuwa hivi..

Kuna nyumba fulani ambayo imejengwa nyumba kuu pamoja na vyumba vya pembeni kwa ajili ya wapangaji. Mwenye nyumba huishi pale pamoja na wapangaji wake. Mwenye nyumba ana watoto wakubwa tu ambao wa mwisho ndio wanaingia kidato cha sita. Huyohuyo mwenye nyumba huwa ana kakijana kadogo tu ka kiume miaka kama 8 au 7 hivi ambako ni katoto ka ndugu yake amekachukua kwa ajili ya kukaa nako.

Katika wale wapangaji kuna mmoja ana watoto wanne, na mtoto wake wa kwanza ni kijana ana umri kati ya miaka 18 au 19 hivi.

Sasa kwenye nyumba hiyo kuna chumba kimoja kimetengwa kwa ajili ya vijana wa yule mwenye nyumba ambao nimeeleza kuwa wapo shule kwa sasa. Kutokana na kutokuwepo, kile chumba akawa analala yule mtoto wa miaka saba pamoja na yule kijana wa mpangaji.

Huyo kijana wa mpangaji ni aina ya vijana ambao wana ule uhuni wa kuiga na kuigiza, bangi za kufata mkumbo pamoja na marafiki wasioeleweka. Unaweza kusema ni balehe lakini naweza kumuweka kundi la wapumbavu sababu mara kadhaa baba yake kamtafutia kazi za kufanya ili kumnusuru lakini hataki kazi kabisa..

Siku ya kuumbuka kwake, Asubuhi alifanya tukio la ubakaji huko mtaani baada ya kumrubuni binti muuza vitumbua kuwa anampeleka walipo wateja wengi anapoweza kumaliza biashara mapema. Kwa umri huyu dogo ni mkubwa kuliko hako kabinti. Alichokifanya akakapeleka maporini huko kisha akatekeleza uovu wake kwa kutumia nguvu na kumsababishia majeraha ya mikwaruzo usoni na sehemu mbalimbali yule binti alipojaribu kujinusuru. Akaendelea na mambo yake akasahau kabisa akarudi kwa wahuni wenzake.

Kale kabinti kumbe kalienda kushtaki ikabidi muda wote ule wazunguke na bibi yake kutafuta wapi anakaa kijana yule ili wapeleke mashtaka. Ilipofika mida ya jioni kweny saa moja kasoro, wakawa wamefanikiwa kupapata kwao na huyo dogo. Wakatoa malalamiko yao, watu kwa hasira wakaanza harakati za kumtafuta kijana kwenye mazingira ambayo mara nyingi huwa anakuwepo bila mafanikio. Kwenye saa mbili na nusu ndio dogo anajirudisha akiwa hana wazo kama uovu wake umefika nyumbani.

Kafikia mikononi kwa watu, alipigwa sana na baba yake. Sasa hapo ndio yakaibuka mapya, kale katoto anakolala nako ikabidi kaseme kuwa huwa anakafanyia ujinga wa kukaingilia.. ikabidi mjadala uhame wakaulize kwa undani. Kweli katoto kakakiri kuwa karibuni kila siku lazima akafanyie huo upuuzi.. watu wakakauliza kwanini muda wote hakajawahi kushtaki? Kakasema huwa anakatishia kukachoma kisu endapo katashtaki.. wakakaagiza kakalete hicho kisu. Kweli kakaingia ndani kanapolala na kutoka na kisu.

Watu walilia, baba yake alimpiga hadi kutaka kumuua wakina mama walilaani sana mtaa ule hadi kuita polisi usiku uleule na yule dogo muovu akaja kubebwa.

Hiki kisa nimekileta ili wazazi tuongeze umakini sana, tena sana kwa watoto wetu wote. Haya mambo ya sijui mjomba au nani kaja halafu unamlaza na watoto kuweni nayo makini sana. Dunia imefikia pabaya mno ndugu zangu.

Ni hayo tu
 
Back
Top Bottom