TAESA imekuwa ni janga kubwa la kukata ndoto za vijana. KwaniniSerikali (PSRS) isianze na vijana wa TAESA kwanza kwa uzoefu walio nao?

Mleta mada pole kwa unayopitia lakini unavyosema PSRS waanze na interns wa TAESA unaonesha kiasi gani ulivyo mchoyo.

TAESA wanatoa internship opportunities ili upate uzoefu ili uongeze employability yako. Na kwa kuwa mnaopitia TAESA mna uzoefu, tunategemea mko vizuri kucompete kwenye interviews.

PSRS wana recruit on behalf of the government ila hawaangalii uzoefu pekee. Wanaangalia MAARIFA, UJUZI, UWEZO, UMAHIRI etc. Sasa sio kila anaepata TAESA ana hivyo vitu

Mkuu, kama unaona hapo TAESA unateseka, njoo mtaani tuungane kupambana kutafuta ajira. Hiyo nafasi waachie wanaotaka kupata experience itakayowasaidia kwenye kutafuta ajira au kujiajiri, vyovyote.

Unasema wanakutumikisha mkuu, hapana, you are being exposed to the tasks ili upate huo uzoefu husika.

Salaam
 
Mtalia sana, mtaomba sana lakini hakutakuwa na matokeo yoyote. Vijana wa Tanzania mnatakiwa mchukuwe action. Haki huja kwa kupiganiwa na siyo kulialia. Mwaka 1951, mwandishi maarufu, Shaaban Robert aliandika kwenye kitabu chake cha Adili na ndugu zake: ''kula uhondo kwataka matendo. Asiye matendo hula uvundo''. Tafakarini!
Tafadhali tuna timia matendo ingawa hatujui huenda tunatumia isivyo sahihi ama kwa watu fake
 
Tena kiko chini ya ofisi ya Mhe. Waziri mkuu. Ni shida kwa kweli. Kwanini wanawatesa vijana wa Kitanzania kiasi hicho? Bora wewe umejipata humo kwenye kutumikishwa kuna wengine tangu wamemaliza kujaza yo profile yao miezi sita imepita hamna lolote.

Bora wangekuwa na hata private kulipia baadhi ya huduma zao maana mambo ya bure bure yanawafanya watu wote kama wajinga wasio na maana.
 
Habari wana JF,

Mimi ni kijana ambaye kwa sasa nipo chini ya Taesa, kwa msiojua utaratibu wao ni kuwa wanakutafutia sehemu ya kufanya internship kwa mkataba wa mwaka mmoja halafu wanakulila 150k per month (Ambayo ni kipengele kwa kweli kuipata) na then mkataba ukiisha wanakuacha.

Hii kitu haimake sense kabisa kwani Taesa wanafanyia vijana interview kama vile utumishi na isitoshe Taesa ipo chini ya serikali najiuliza kwanini hawa vijana wasipewe kipaumbele na PSRS kwenye ajira, mwishowe wanawatumikisha na kuwapotezea tu muda.

Siwafichi jamani sisi vijana wa Taesa tunateseka huku maofisin tunatumikishwa na hela pia zinachelewa lkn serikali hii inakaa kimya kabisa ni as if hii taasisi haina vision, sabb mtu ana experience na bado anatelekezwa this is not right.

MAMA SAMIA NA WIZARA YA UTUMISHI NA KAZI KAMA MNASOMA HILI NAOMBA MLIFANYIE KAZI, kamwee kijana aliotoka internship chini ya Taesa kwa interview juu huwez kumtelekeza kirahisi na kumuacha apotee mtaani na wakat tayar anajua system ya kazi na isitoshe ni kama serikali imemu overuse.

NB: AMBAE HAUPO TAESA NA HUPITII HILI USICOMENT UJINGA SABB HUJUI TUNACHOPITIA.
Mkuu hivi Kuna probability yeyote ya taasisi unayifanya intern
pia kukulipa
 
Kama kawaida yetu dunia ya sasa....

Tunatibu Symptoms badala ya Ugonjwa; Tatizo kubwa ulimwengu huu wa Teknolojia Manpower Haiitajiki kama zamani; Hivyo basi tatizo sio vijana hawa wala vijana wale kupewa..; Bali issue ni Kama taifa kuongeza vitu vya kufanya ili vijana wote na wananchi wote wapate ujira....

Dunia imebadilika; we are at a cross roads; Kwa Ushauri; Vijana au kada yoyote ile usitegemee Serikali hii au mtu yoyote kukusaidia au kuwasaidia ni nyie wenyewe kwa umoja wenu ndio mnaweza kujikomboa..., Ni either mta-survive wote kwa pamoja au kufa mmoja mmoja; Hakuna njia nyingine
 
Hivi kumbe inawezekana, ikiwa bahati ukapewa mkataba wa kudumu kwenye baadhi ya hizi taasisi
Mkataba wa kudumu sidhani

Mm mwenyewe nipo njia panda nawaza ntawezaje kuishi na 150k maana Kodi ya chumba ,nauli pamoja na kula haitoshi hapo Bado sijaumwa ,,halafu pia ndio wanasema huipati kwa wakati😭😭
 
Mkataba wa kudumu sidhani

Mm mwenyewe nipo njia panda nawaza ntawezaje kuishi na 150k maana Kodi ya chumba ,nauli pamoja na kula haitoshi hapo Bado sijaumwa ,,halafu pia ndio wanasema huipati kwa wakati
Kama huna ishu ya kukuingizia hicho kiasi na upo karibu nenda tu
 
Mkataba wa kudumu sidhani

Mm mwenyewe nipo njia panda nawaza ntawezaje kuishi na 150k maana Kodi ya chumba ,nauli pamoja na kula haitoshi hapo Bado sijaumwa ,,halafu pia ndio wanasema huipati kwa wakati
Mkuu usiache kwenda acha sababu trust me hautojutia kama mm nmeweza kikubwa usiifkirie sana hyo hela if kwenu au kama una ndugu wanaweza kukupa back up ata kwa miezi 2 yq mwanzo itakua njema sabb utapata experience ya kutosha na tanga uwasa kuna hela hela huwez toka patupu niamin
 
Lakini toka mwanzo si mlikubaliana na wewe ukakubali.
Sometimes tuache lawama sizizo na msingi. Upo hapo kujifunza ilipaswa wewe ndo uwalipe kabisa.
 
Mkuu usiache kwenda acha sababu trust me hautojutia kama mm nmeweza kikubwa usiifkirie sana hyo hela if kwenu au kama una ndugu wanaweza kukupa back up ata kwa miezi 2 yq mwanzo itakua njema sabb utapata experience ya kutosha na tanga uwasa kuna hela hela huwez toka patupu niamin
Hizo hela hela mkuu zinatokea wapi. Ni bora ukamueleza ukweli tu ili kama ni mbinu azijue badala ya kumpa matumaini hewa
 
Back
Top Bottom