Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu

assassin eagle

Senior Member
Apr 23, 2022
113
451
Mimi ni kijana nilizaliwa mwaka 88 Mwanza mjini, tuliishi kwenye nyumba ya familia ile nyumba tuliishi familia mbili babu alikuwa na wake watatu hivyo pale walekaa Bibi zangu wawili na watoto wao ambao Kila Bibi alikuwa na watoto Saba Kila mtoto alikuwa na watoto wake pia hivyo waligawana vyumba, Bibi mwingine yeye hakuzaa, japo babu alikuwa na nyumba nyingine tatu.

Kila Bibi alikuwa amepewa nyumba moja na nyumba hizi zilikuwa zimejengea mitaa tofauti, kwa kifupi maisha hayakuwa mazuri pale tuliishi kigumu gumu, uwezo wangu darasani pia haukuwa mzuri japo nilikuwa siwi wa mwisho mwaka 2000 walielewana wauze ile nyumba sisi tulienda kuishi na Bibi yetu ambae alikuwa ameacha chumba kimoja katika ile nyumba waliogawiwa, vyumba vingine walikuwa wamepangisha Kodi watoto ndio waliokuwa wanachukua yeye hakupewa kitu.

Bibi yangu alikuwa mpole sana, watoto wa kiume ndio walipanga pembeni watoto wa kike walikaa na mama yao pamoja na wajukuu wale wa kiume pia kula walikuwa wanakula pale kwa bibi ,Bibi yangu alikuwa anajishughulisha na biashara ndogo ndogo aliweza kutulisha wote na matumizi madogo madogo alikuwa anatupatia ,kwakweli maisha Yale yalikuwa yananiumiza sana yaani kulala ni tabu wajukuu wengi mna lala mpaka uvunguni nilijaribu kwenda kwa mzee wangu kukaa sababu yeye alikuwa na nyumba kubwa tu ,lakin yule mke wake akakataa Mimi kukaa pale yule mwanamke alisusia Kila kitu akasema kama Mimi nakaa pale basi yeye ataondoka.

Baba ikabidi anifukuze ila niligoma kuondoka baadae baba akaniita pembeni kwa upole akanieleza nirudi tu kwa mama yangu akaniambia hanichukii ila Sasa hivi ni ngumu kumuelewa ila nikiwa mkubwa nitakuja kumuelewa basi bwana ikabidi niondoke zangu niende kwa Bibi tuliishi hivyo hivyo kwa tabu aise ,mwaka 2002 nilimaliza darasa la Saba sikufanikiwa kufaulu Bibi nae alikuwa ameshachoka Kila siku anaumwa baadae Bibi alishindwa kabisa kuendelea kufanya biashara ikabidi apumzike huwezi amini watoto walishindwa kumtunza kabisa yule mzee.

Itaendelea
===
Muendelezo soma Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu
 
Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -2

Baada ya Bibi kushindwa kufanya biashara maisha yalikuwa magumu sana, baadae mama yangu alienda visiwani kufanya shughuli za upishi kwa wavuvi, alikaa kule kama miezi 4 akaniita na Mimi ili nikafanye shughuli ndogo ndogo, basi tulipambana na kusaka maisha na mama, baadae mama aliweza kununu mtego wa kuvulia dagaa na taa za karabai, mtumbwi alikodi akawa analipa kwa Giza (mwezi ) tulienda kupambana baadae nakaanza shughuli ya kuuza dagaa, nachukua kule visiwani napeleka mwaloni kuuza mtaji wangu ulikuwa mdogo hivyo nilikuwa nasubiri dagaa zilizokosa wateja ndio nachukua Mimi, baadae wajomba zangu nao walianza kufanya hiyo kazi ya kuuza dagaa lakini hawa jamaa Kuna muda wanakuomba pesa yako kwamba wakiuza mzigo watakurudishia lakini ukiwapa ndio mazima pesa hairudi kwa kweli roho ilikuwa inaniuma sana .

Itaendelea

===
Muendelezo soma Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu
 
Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -3

Niliendelea kukomaa hivyo hivyo baadae mama alianza kuugua kwa muda mrefu, pale kwenye kazi ilibidi Mimi ndio niwe nasimamia, pesa niliyokuwa naipata nyingine nilikuwa natuma kwa mama nyingine nilikuwa natunza nilikuwa najiwekea akiba kwa matumizi ya baadae.

Sasa baadae mama akarudi nikamuuliza walikukuta na shida gani huko hospital, mama akasema walimpima VVU na kukuta na maambukizi ila wameshamuanzishia dawa pia Kila mwezi anatakiwa kwenda cliniki kwa ajili ya kuongeza dawa, kwakweeli roho iliniuma sana.

Nikasema Sasa mama yangu anaondoka wadogo zangu bado wadogo sana wapo 3 ,ila Kuna Dada yetu mmoja alibahatika kuwa mwalimu sengerema vijijini, baadae ile pesa niliyokuwa naitunza nilitaka niende shule ya private nijiandikishe nisome hivyo hivyo hata kama nisipo maliza fresh tu ili mradi nimeingia secondari. Basi bana nikaenda kuchukua fomu ya kujiunga Sasa zile gharama za kuanza kulipia masomo zilikuwa hazitoshi nikamshirikisha Bibi yangu baadae Bibi akamwambia mjomba mjomba akasema twende tukafate dagaa mjomba alikuwa na laki 7 Mimi ya kwangu ilikuwa laki 3 na nusu tukaenda kuchukua mzigo kurudi kuuza dah pesa niliyoambuluia ni kama elfu 70 tu .

Itaendelea

===
Muendelezo soma Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu
 
Mimi ni kijana nilizaliwa mwaka 88 Mwanza mjini, tuliishi kwenye nyumba ya familia ile nyumba tuliishi familia mbili babu alikuwa na wake watatu hivyo pale walekaa Bibi zangu wawili na watoto wao ambao Kila Bibi alikuwa na watoto Saba Kila mtoto alikuwa na watoto wake pia hivyo waligawana vyumba, Bibi mwingine yeye hakuzaa, japo babu alikuwa na nyumba nyingine tatu.

I
Hi nayo Ni stori za kuendlea embu acha upumbavu
 
Mimi ni kijana nilizaliwa mwaka 88 Mwanza mjini, tuliishi kwenye nyumba ya familia ile nyumba tuliishi familia mbili babu alikuwa na wake watatu hivyo pale walekaa Bibi zangu wawili na watoto wao ambao Kila Bibi alikuwa na watoto Saba Kila mtoto alikuwa na watoto wake pia hivyo waligawana vyumba, Bibi mwingine yeye hakuzaa, japo babu alikuwa na nyumba nyingine tatu.

Kila Bibi alikuwa amepewa nyumba moja na nyumba hizi zilikuwa zimejengea mitaa tofauti, kwa kifupi maisha hayakuwa mazuri pale tuliishi kigumu gumu, uwezo wangu darasani pia haukuwa mzuri japo nilikuwa siwi wa mwisho mwaka 2000 walielewana wauze ile nyumba sisi tulienda kuishi na Bibi yetu ambae alikuwa ameacha chumba kimoja katika ile nyumba waliogawiwa, vyumba vingine walikuwa wamepangisha Kodi watoto ndio waliokuwa wanachukua yeye hakupewa kitu.

Bibi yangu alikuwa mpole sana, watoto wa kiume ndio walipanga pembeni watoto wa kike walikaa na mama yao pamoja na wajukuu wale wa kiume pia kula walikuwa wanakula pale kwa bibi ,Bibi yangu alikuwa anajishughulisha na biashara ndogo ndogo aliweza kutulisha wote na matumizi madogo madogo alikuwa anatupatia ,kwakweli maisha Yale yalikuwa yananiumiza sana yaani kulala ni tabu wajukuu wengi mna lala mpaka uvunguni nilijaribu kwenda kwa mzee wangu kukaa sababu yeye alikuwa na nyumba kubwa tu ,lakin yule mke wake akakataa Mimi kukaa pale yule mwanamke alisusia Kila kitu akasema kama Mimi nakaa pale basi yeye ataondoka.

Baba ikabidi anifukuze ila niligoma kuondoka baadae baba akaniita pembeni kwa upole akanieleza nirudi tu kwa mama yangu akaniambia hanichukii ila Sasa hivi ni ngumu kumuelewa ila nikiwa mkubwa nitakuja kumuelewa basi bwana ikabidi niondoke zangu niende kwa Bibi tuliishi hivyo hivyo kwa tabu aise ,mwaka 2002 nilimaliza darasa la Saba sikufanikiwa kufaulu Bibi nae alikuwa ameshachoka Kila siku anaumwa baadae Bibi alishindwa kabisa kuendelea kufanya biashara ikabidi apumzike huwezi amini watoto walishindwa kumtunza kabisa yule mzee.

Itaendelea
I
kuzaa sio kupata chunguza utagundua wanaume walio wengi wanapo oa wake wengi inakuwa sababu ya watoto kuteseka hata muoaji awe na hela yakutosha tatizo wanaweke baadhi yao wanakuwa na roho mbaya inayo ambatana na uchawi
 
Back
Top Bottom