Kuongezeka kwa Ujenzi wa Vituo vya Mafuta kwenye makazi ya watu Serikali inasubiri ya Morogoro yatokee ndio ichukue hatua?

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Vituo vya Mafuta vinajengwa kila sehemu hadi kwenye makazi ya watu. Kwanini Serikali inatoa vibali kwa sehemu hatarishi?

Kuna vituo vingi sana vya mafuta vinajengwa katika maeneo hatarishi kwa jamii na Serikali sijui inaridhia ujenzi huu kwa namna gani? Sijui kwanini haifikirii?

Nakumbuka Septemba 2022, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula aliagiza kusimamishwa kwa ujenzi wa majengo yanayojengwa kinyume cha sheria na kuondolewa vituo vya mafuta vilivyojengwa kinyume cha sheria ikiwa ni pamoja na kutozingatia umbali. Alitaka wabadilishe umbali wa kutoka mita 200 hadi mita 500 wa kituo kimoja kwenda kingine.

Aidha, Novemba 10, 2022, Waziri Mabula alisema Serikali imesitisha ujenzi wa vituo vya mafuta ili kutoa nafasi ya kufanya tathimini ya ujenzi wa vituo hivyo kufuatia ongezeko la ujenzi holela wa vituo hivyo

Lakini pia, mnamo Aprili 2023, Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango aliagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kushirikiana na Wizara ya Ardhi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kufanya ukaguzi wa kina juu ya vituo vya mafuta vinavyojengwa kwa wingi kwenye makazi ya watu mkoani Dar es Salaam ili kunusuru kusitokee majanga ya moto.

Pamoja na matamko yote hayo, Serikali imedhiirisha kuwa ya matamko kwani hakuna kilichoendelea wala kufanyika

Mfano Kituo cha mafuta cha Lake Oil kilichopo Kawe pale Tanganyika Packers ni hatarishi kweli kweli iwapo kutatokea mlipuko au madhara ni makubwa sana

Bado kuna Kituo kingine kimejengwa Mikochenk karibu na makazi ya Watu ambacho kimelamikiwa hadi na Mwanasiasa nguli, Prof. Anna Tibaijuka ila bado Serikali hii ipo kimya.

Huenda inangoja yatokee yale ya ajali ya moto wa mafuta na idadi ya vifo vile kama kule Morogoro ndio wanashughulikia na kuweka sana pale ambapo Watanzania watakuwa na huzuni kubwa ya kupoteza Ndugu, Jamaa na Marafiki.

IMG_8602.png

Ramani kuonesha Kituo cha Mafuta cha Lake Oil kilichopo Kawe

Je, Serikali inasubiri hadi majanga yatokee na tupate maafa kama ya Morogoro kwenye ajali ya mafuta ili kuchukua hatua?

Natambua Waziri wa Ardhi wa sasa, Jerry Silaa amechukua hatua ya kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa maendeleo ya makazi, Deogratius Kaliminze ila hiyo haitoshi kabisa, mara nyingi sana hii hutokea na hakuna cha maana kinafanyika. Inadaiwa huyu mtu vituo kadhaa ni vyake kupitia syndicate aliyoitengeneza.

Soma: Pongezi Waziri Silaa kumsimamisha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi vituo vya Mafuta vinajengwa katikati ya Makazi

Pia soma: Waziri Silaa apiga marufuku ujenzj holela wa Vituo vya Mafuta na kusimamisha matumizi ya Kituo cha mafuta cha Barrel cha Mikocheni
 
Hivi vituo vilitakiwa vijengwe nje ya mji vijitenge na makazi ya watu. Kuna mji mmoja barabara kuu vituo vya mafuta vimejengwa vinakaribiana mita chachache kutoka kimoja hadi kingina na vyote vipo kwenye makazi ya watu
 
Vituo vya Mafuta vinajengwa kila sehemu hadi kwenye makazi ya watu. Kwanini Serikali inatoa vibali kwa sehemu hatarishi?

Kuna vituo vingi sana vya mafuta vinajengwa katika maeneo hatarishi kwa jamii na Serikali sijui inaridhia ujenzi huu kwa namna gani?
Hilo la Moro ulishuhudia au ulihadithiwa mbona hatujawahi kulisikia, usiwe umechanganya tukio la lori la mafuta lililopata ajali na moto ukasababishwa na bodaboda wezi wa mafuta, na ajali kama hiyo ilitokea Mbeya pia.
 
Acha wivu mzee utakufa masikini. Ile ya Msamvu ilikua ajali ya gari sio kituo cha mafuta. Alafu usitukumbushe machungu😟😟😟😟😟
 
Huo mfano wa Morogoro hauna mantiki kwenye hoja yako ile ajali ilitokea barabarani na hakikua kituo cha mafuta.

Kama watu hawataki kukaa karibu na vituo vya mafuta basi walipwe fidia wahame

By the way sijawahi kusikia kituo cha mafuta kimeleta madhara kwenye makaz ya watu
 
Huo mfano wa morogoro hauna mantiki kwenye hoja yako ile ajali ilitokea barabarani na hakikua kituo cha mafuta.

Kama watu hawataki kukaa karibu na vituo vya mafuta basi walipwe fidia wahame

By the way sijawahi kusikia kituo cha mafuta kimeleta madhara kwenye makaz ya watu
Usisubiro usikie ndio uelewe madhara yake.
 
Kuna kituo kingine jina sikumbuki, kimejengwa katikati ya makazi barabara ya kwenda UDSM kupitia Ubungo Msewe, ile ni hatari.
1. Barabara ni finyu sana.
2. Kituo kimebanana na makazi
 
Utitiri wa Vituo vya Mafuta ni hoja ya KIBIASHARA zaidi kuliko ya KIUSALAMA.
Haiingii akilini kuwa uhitaji wa Petroli na Dizeli umekuwa mkubwa sana kiasi cha kutakiwa uongezekaji wa Vituo, tena karibu karibu kama tunavyoona jijini Dar es Salaam.

Tatizo la usalama kuhofia KULIPUKA MOTO kwenye Vituo vya Mafuta ni dogo sana kwa sababu Mafuta yaliyohifadhiwa chini ardhini ndani ya Matenki ni salama zaidi kuliko Galoni ya Mafuta ya Taa iliyohifadhiwa ndani ya Nyumba zetu.
Chupa ya Mafuta ya Taa nyumbani ni hatari zaidi KIUSALAMA maana Mafuta yanakutana na hewa ya Oksijeni kiurahisi zaidi.

Kama ilivyo kwenye "Sheli za Pikipiki" ambazo zimesambaa sana kwenye maeneo yetu ya Makazi kuhudumia Bodaboda.

Ni vema kufahamu kwamba Petroli na Dizeli, vyenyewe, HAIWAKI/HAILIPUKI mpaka ikutane na hewa ya OXYGEN.
Kama Bomba za Chuma zinazoleta Mafuta kutoka kwenye Matanki chini ya Ardhi kupeleka kwenye Pampu za kujazia Mafuta kwenye Magari HAZIVUJI, uwezekano wa MLIPUKO wa Moto unakuwa haupo.

Lakini kitu muhimu cha kujiuliza ni iwapo kuna umuhimu wa kuwa na Vituo vingi vya Mafuta kwa kiasi tunachoona.

Ni sawa na kujenga Soko kila Mtaa.
Watu wa Mipango Miji wanaoruhusu hali hii wameonyesha UDHAIFU mkubwa wa KITAALUMA.

Na UDHAIFU huo unachochowa na RUSHWA.

Biashara ya Mafuta ni biashara ya pesa nyingi.
 
Vituo vya Mafuta vinajengwa kila sehemu hadi kwenye makazi ya watu. Kwanini Serikali inatoa vibali kwa sehemu hatarishi?

Kuna vituo vingi sana vya mafuta vinajengwa katika maeneo hatarishi kwa jamii na Serikali sijui inaridhia ujenzi huu kwa namna gani? Sijui kwanini haifikirii?

Nakumbuka Septemba 2022, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula aliagiza kusimamishwa kwa ujenzi wa majengo yanayojengwa kinyume cha sheria na kuondolewa vituo vya mafuta vilivyojengwa kinyume cha sheria ikiwa ni pamoja na kutozingatia umbali. Alitaka wabadilishe umbali wa kutoka mita 200 hadi mita 500 wa kituo kimoja kwenda kingine.

Aidha, Novemba 10, 2022, Waziri Mabula alisema Serikali imesitisha ujenzi wa vituo vya mafuta ili kutoa nafasi ya kufanya tathimini ya ujenzi wa vituo hivyo kufuatia ongezeko la ujenzi holela wa vituo hivyo

Lakini pia, mnamo Aprili 2023, Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango aliagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kushirikiana na Wizara ya Ardhi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kufanya ukaguzi wa kina juu ya vituo vya mafuta vinavyojengwa kwa wingi kwenye makazi ya watu mkoani Dar es Salaam ili kunusuru kusitokee majanga ya moto.

Pamoja na matamko yote hayo, Serikali imedhiirisha kuwa ya matamko kwani hakuna kilichoendelea wala kufanyika

Mfano Kituo cha mafuta cha Lake Oil kilichopo Kawe pale Tanganyika Packers ni hatarishi kweli kweli iwapo kutatokea mlipuko au madhara ni makubwa sana

Bado kuna Kituo kingine kimejengwa Mikochenk karibu na makazi ya Watu ambacho kimelamikiwa hadi na Mwanasiasa nguli, Prof. Anna Tibaijuka ila bado Serikali hii ipo kimya.

Huenda inangoja yatokee yale ya ajali ya moto wa mafuta kama kule Morogoro ndio wanashughulikia na kuweka sana pale ambapo Watanzania watakuwa na huzuni kubwa ya kupoteza Ndugu, Jamaa na Marafiki.

View attachment 2850297
Ramani kuonesha Kituo cha Mafuta cha Lake Oil kilichopo Kawe

Je, Serikali inasubiri hadi majanga yatokee na tupate maafa kama ya Morogoro kwenye ajali ya mafuta ili kuchukua hatua?

Natambua Waziri wa Ardhi wa sasa, Jerry Silaa amechukua hatua ya kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa maendeleo ya makazi, Deogratius Kaliminze ila hiyo haitoshi kabisa, mara nyingi sana hii hutokea na hakuna cha maana kinafanyika. Inadaiwa huyu mtu vituo kadhaa ni vyake kupitia syndicate aliyoitengeneza.

Soma: Pongezi Waziri Silaa kumsimamisha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi vituo vya Mafuta vinajengwa katikati ya Makazi
WIZARA ya ARDHI ina WASOMI lakini MICHANGO ya WASOMI wao ni KUHARIBU MIJI NA KUONGEZA MIGOGORO isiyo na ULAZIMA

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Utitiri wa Vituo vya Mafuta ni hoja ya KIBIASHARA zaidi kuliko ya KIUSALAMA.
Haiingii akilini kuwa uhitaji wa Petroli na Dizeli umekuwa mkubwa sana kiasi cha kutakiwa uongezekaji wa Vituo, tena karibu karibu kama tunavyoona jijini Dar es Salaam.
Tatizo la usalama kuhofia KULIPUKA MOTO kwenye Vituo vya Mafuta ni dogo sana kwa sababu Mafuta yaliyohifadhiwa chini ardhini ndani ya Matenki ni salama zaidi kuliko Galoni ya Mafuta ya Taa iliyohifadhiwa ndani ya Nyumba zetu.
Chupa ya Mafuta ya Taa nyumbani ni hatari zaidi KIUSALAMA maana Mafuta yanakutana na hewa ya Oksijeni kiurahisi zaidi.
Kama ilivyo kwenye "Sheli za Pikipiki" ambazo zimesambaa sana kwenye maeneo yetu ya Makazi kuhudumia Bodaboda.
Ni vema kufahamu kwamba Petroli na Dizeli, vyenyewe, HAIWAKI/HAILIPUKI mpaka ikutane na hewa ya OXYGEN.
Kama Bomba za Chuma zinazoleta Mafuta kutoka kwenye Matanki chini ya Ardhi kupeleka kwenye Pampu za kujazia Mafuta kwenye Magari HAZIVUJI, uwezekano wa MLIPUKO wa Moto unakuwa haupo.
Lakini kitu muhimu cha kujiuliza ni iwapo kuna umuhimu wa kuwa na Vituo vingi vya Mafuta kwa kiasi tunachoona.
Ni sawa na kujenga Soko kila Mtaa.
Watu wa Mipango Miji wanaoruhusu hali hii wameonyesha UDHAIFU mkubwa wa KITAALUMA.
Na UDHAIFU huo unachochowa na RUSHWA.
Biashara ya Mafuta ni biashara ya pesa nyingi.
Kama sababu ni za kibiashara then inatakiwa waachwe soko litaamua. Huwezi kumzuia mtu kuanzisha biashara eti kwa kigezi kuwa tayari kuna biashara kama hiyo pembeni yake. Acha wapambani kibiashara soko litaamua nani atasurvive.
Hoja ya kupinga nafikiri iwe ya kiusalama zaidi kuliko kibiashara.
Kama vile ukitaka kufingua hotel mtaa fulani, manispaa haipaswi kukuzuia kwa kigezo kuwa tayari kuna hotel nyingine ipo mtaa huo. Soko huria.
 
Kuna mixenge itakuja kukupinga na umeongea ukweli mtupu..

juzi Kuna sehemu nimepita Barabara ya mtaani,nikakuta foleni iliyosababishwa na gari la mafuta kumbe Kuna kituo Cha mafuta humo humo mtaani,Cha ajabu ile Barabara nyaya za nguzo pande moja kwenda nyingine zilikuwa zimelala Hadi Lori limeshindwa kupita..Kuna siku balaa likitokea tutarudi kwenye hii nyuzi
 
Sijui ni nn mm mwenyewe mpaka nimejiuliza mfano ni mdogo tu kutoka kigamboni ferry pale mpaka kigamboni darajani kuna vituo vya mafuta hata kumi na usheee sehem ambayo si zaid ya km 8 lakini ina vituo kumi na ushee na eneo hilo ndio kuna makazi ya watu pia matank ya reserv ila ndo kuna vituo vya mafuta km vyote.
 
Back
Top Bottom