Taasisi ya Regia Mtema Foundation & Biography ya Regia

Jul 14, 2008
1,820
1,031
Wanajamii

Taasisi ya Regia Mtema Foundation (RMF) iliyosajiliwa BRELA Tarehe 27-04-2012 na kupewa Cheti Cha Usajili No: 90580 imeshaanza rasmi kazi zake na pia kazi ya kuandika "Biography ya Regia Mtema" na pia kuandika "Kitabu Cha Kero Za Wananchi" ambazo Marehemu Regia alikuwa amezikusanya ili hatimaye ziwakilishwe kwa wahusika. Tayari RMF imeshaingia Mkataba wa Kuandika Vitabu hivyo na Kampuni (Biography) na Mwandishi wa Kujitegemea (Kero za Wananchi).

Vitabu vyote viwili vinatarajiwa kukamilika katika muda wa Siku 60 zijazo na hivyo kuweza kuzinduliwa rasmi.

Jumla ya TZS 20.3 Millioni zinatakiwa ili kukamilisha kazi ya kuchapisha Nakala 1000 za awali kwa kila kitabu.

Kwa niamba ya RMF naomba kutoa wito kwa Marafiki wote wa marehemu Regia; Ndugu, Jamaa na Marafiki ambao Walithamini Michango na Kazi Zake na sasa wangependa kuchangia Kifedha katika kufanikisha kazi hii wanakaribishwa sana kuweza kuchangia.

Michango iwakilishwe kwa:

Michaeli Dalali - Katibu wa RMF: +255 +255 783 222 217; +255 717 011 112
Maxence Mello - Mjumbe wa Bodi: +255 784 526 444
Sanctus Mtsimbe - Mwenyekiti RMF: +255 782 820 820

Unaweza pia kutoa Ahadi yako kwa kunitumia PM hapa JF na kutoa Contacts zako ili tuweze kufuatilia kama utapenda.

Kwa wale waliopo Dar Es Salaam tunaweza kutuma mjumbe kuja kuchukua mchango wako popote ulipo na hivyo kurahisisha upatikanaji wa mchango wako.

Waliopo Mjini Dar Es Salaam, mnaweza kutoa Michango yenu kwenye Ofisi za Muda za RMF zilizopo:

Sokoine Drive/Pamba Road
Opposite Luther House or Life House/Standard Chartered Bank
Tancot House;
2[SUP]nd[/SUP] Floor; Left Wing (3rd Floor including Mezanine)

Kwa yeyote anayependa kuwa Mwanachama wa Taasisi hii ya RMF anaweza kutuandikia na tutamtumia nyaraka zote muhimu zinazohusiana na Taasisi.

Wasalaam

Sanctus Mtsimbe
Mwenyekiti wa Muda
Regia Mtema Foundation

sam@danimex.com
+255 782 820 820
 
Along with this message is my applause and gratitude for the wonderful job you have done today and days beforehand. May today's success be the beginning of tomorrow's achievements
 
Pamoja na hizi jitihada, si vibaya kuangalia wale ambao hupenda kutoa support kama vile kulipia printing, etc. some people waoga kuadvance cash kutokana na previous experiences zao
 
Along with this message is my applause and gratitude for the wonderful job you have done today and days beforehand. May today's success be the beginning of tomorrow's achievements

Mkuu The Finest tuko pamoja Mkuu. Asante kwa kazi kubwa uliyoifanya pale BC bado nakumbuka.

Tuendeleaa kuyafanyia kazi. This time kwa vitendo.
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na hizi jitihada, si vibaya kuangalia wale ambao hupenda kutoa support kama vile kulipia printing, etc. some people waoga kuadvance cash kutokana na previous experiences zao

Mkuu TIMING, tuko pamoja. Wenye uwezo wa kufanya hivyo wanakaribishwa pia. At the end of the day kinachotakiwa ni output.

Je, unapenda kutoa ahadi kuchangia chochote?
 
Last edited by a moderator:
Amina chifupa foundation imekwenda wapi?????????????? Nchi inatakiwa kuwa na foundation ngapi? Nyerere foundation, Mkapa foundation.

kwa nini wasipanue majukumu ya Nyerere foundation na kuichangia fedha zaidi kama ilivyo kwa Mandela foundation?
 
MAMA POROJO tafadhali kama una hoja kuhusu Amina Chifupa Foundation anzisha thread kuhusu hilo. Kuhusu nchi inatakiwa kuwa na foundations ngapi nakushauri ukaulize kwenye taasisi zinazohusika na usajili wa hizi taasisi. Btw, mbona mlipoanzisha Benjamin Mkapa Foundation haukusema msifanye hivyo ila mpanue majukumu ya Nyerere Foundation?
Kama huna mchango si lazima ku-comment.
 
Asante Mama Porojo. Kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni anayotaka ili mradi havunji sheria.

Nimeona wadau wameshakujibu.
 
Dili hilo wadau,

Bilauri iliyo na maji nusu ujazo unaweza ikaangaliwa kwa mitazamo miwili tofauti juu ya ujazo wake:

Glass is Half Full
or
Glass is Half Empty

Whatever the case is is the matter of someone's attitude of looking into things. And the choice is completely his/hers.
 
MAMA POROJO tafadhali kama una hoja kuhusu Amina Chifupa Foundation anzisha thread kuhusu hilo. Kuhusu nchi inatakiwa kuwa na foundations ngapi nakushauri ukaulize kwenye taasisi zinazohusika na usajili wa hizi taasisi. Btw, mbona mlipoanzisha Benjamin Mkapa Foundation haukusema msifanye hivyo ila mpanue majukumu ya Nyerere Foundation?

Kama huna mchango si lazima ku-comment.

Well written.

Thank you.
 
Napongeza kwa kazi nzuri nitajitahidi kuchangia kuanzia wk ijayo tupo pamoja.
Huwa naamini katika kutoa zaidi kuliko kupokea Mungu awabariki.

Mkuu tuko pamoja sana.

Kwa ajili ya kutusaidia, unaweza kunitumia PM nikajua ahadi yako ni kiasi gani na umepanga kuzitoa namna gani?
 
Back
Top Bottom