Taarifa ya smz kuhusu ajali ya meli ya mv. Skagit iliyotolewa jana usiku julai 19,2012

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa taarifa usiku huu ikieleza idadi ya watu waliopatikana wakiwa hai ni 146 na kupata maiti 62.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari usiku leo,Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna alisema taarifa hiyo ndio sahihi na kuwataka wananchi kutoamini taarifa zinazotolewa na watu wengine zaidi ya Serikali.

Waziri Shamuhuna alisema kwamba maiti 62 walipatikana ambao kati ya maiti hizo watoto ni 9 na kuna raia mmoja wa kike wa kigeni ambaye hakuweza kutambulika Uraia wake,lakini umeonekana picha yake moja ndogo ya hati ya kusafiria.

Waziri Shamuhuna alisema meli hiyo ilibeba jumla ya abiria 290 kati ya hao watu wazima 250, watoto wadogo 31 na mabaharia 9.

Waziri huyo aliwataka wananchi katika sehemu mbalimbali hasa katika vijiji vilivyo kandokando ya bahari watakapoona maiti au mtu akiwa hai ambaye wanadhani ni wa ajali ya Meli ya Skagit.

Aidha, Waziri Shamuhuna alisema kwamba kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao watakuwa na wasiwasi wa kutowaona ndugu na jamaa zao amewataka kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kupata taarifa zaidi au kuripoti habari za kupotelewa kwa ndugu au jamaa zao.

Kwa upande wa Zanzibar, Waziri huyo aliwataka wananchi kufika kwa Masheha wao kutoa taarifa kama hizo.

KWA HABARI KAMAILI BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI: TAARIFA YA SMZ KUHUSU AJALI YA MELI YA MV. SKAGIT ILIYOTOLEWA JANA USIKU JULAI 19,2012

 
Back
Top Bottom