Taarifa ya Polisi Dar kuhusu wanaojihusisha na ‘UKUTA’

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573



jjj.jpg

Licha ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutangaza kufanya maandamano ya nchi nzima Septembe 1 2016, Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam limemkamata mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Yoram Mbyellah kwa kupatikana na kuuza sare aina ya fulana zenye maneno ya kichochezi zikiwa na alama ya CHADEMA huku nyingine zikiwa na maneno ‘UKUTA’

Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema…>>>’August 20 2016 Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya Kinondoni kuna duka linauza flana zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ , ‘UKUTA’

‘Aidha Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara na mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake’

‘Ili tuishi kwa amani ni lazima tutii sheria na kama hutaki kutii sheria tutashughulika naye, Kama kuna mtu anataka kuvunja amani katika mkoa wetu ajue kabisa hatoweza na niseme tu kwamba kama wanataka kujenga ukuta wajenge ukuta mwingine maana huu umeshadondoka‘

‘Na wapo watu wanasema kwanini tunafanya mazoezi, nikwamba Jeshi la Polisi ni kawaida kufanya hivyo na muhimu watu wajue hiyo September 1 hakutakuwa na maandamano ya aina yoyote kwahiyo watu wasiwe na hofu bali wachape kazi’
 
Safi sana
Ila hata ikiwa ni lengo la kuzuia wanywa viroba kuivuruga nchi ni mahala pake,
Kiukweli natoa pongezi sana kwa police
Vijana wengi wame ghairi UKTA
Kwa mazoezi yale,
Wengi wamesema kutumika tena no
 
Safi sana
Ila hata ikiwa ni lengo la kuzuia wanywa viroba kuivuruga nchi ni mahala pake,
Kiukweli natoa pongezi sana kwa police
Vijana wengi wame ghairi UKTA
Kwa mazoezi yale,
Wengi wamesema kutumika tena no
Kumbuka vita havina macho.
Mtego wa panya kuingia waliomo na wasiokuwemo.
 
Tumeishawazoea kwa kutoa taarifa za uongo, kwani pale bavicha waliposema wanaenda dodoma kuzuia mkutano wa ccm si tuliona mambo kama haya, sasa wanamdanganya nani, tukutane tarehe 1 September
 
Hivi itakuwaje kama jamaa atatoa maana tofauti ya neno ukuta kwe hilo kaptura lake walilomkamata nalo....au watamlazimisha maana yao wao?
 
Back
Top Bottom