Dar: Polisi yazima maandamano, yakiri kumshikiliwa Sheikh Ponda kwa mahojiano

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP. Muliro amepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika leo Novemba 10, 2023 Dar es Salaam, pia amewatahadharisha wananchi kutoshiriki maandamano hayo.

=====

Polisi Dar wazima maandamano, Sheikh Ponda akamatwa
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezima maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kuanzia viwanja vya Mnazi Mmoja hadi Manzese, huku likikamata baadhi ya viongozi wanaodaiwa kuyandaa akiwemo Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Taarifa za maandamano hayo inayoandikwa kuwa imetolewa na Shura ya Maimamu Tanzania, zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii leo Novemba 10, zikieleza kuwa ni maandamano ya kutetea Mamlaka ya Palestina ambayo yalipangwa kufanyika leo saa 7:30 mchana kuanzia Mnazimmoja hadi Manzese.

Kufuatia taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Jumanne Muliro alitoa taarifa kupitia video kwenye mitandao ya jamii akipiga marufuku maandamano hayo.

Mwananchi Digital ilifika Mnazimmoja na kukuta umati wa watu, huku askari Polisi wenye sare wakiwa wameimarisha ulinzi kuzunguka viwanja hivyo.
Chanzo: Mwananchi

===========

UPDATES: TAARIFA YA JESHI LA POLISI

Akizungumza na JamiiForums kuhusu taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Jumanne Muliro amesema:

"Tulimueleza taarifa zinazohusiana na mikutano au makusanyiko, taarifa zake anatakiwa kupeleka kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya kwa mujibu wa Katiba na Sheria, na Mkuu wa Polisi wa Wilaya anatakiwa kutoa mwongozo wa kiusalama, yeye (Ponda) hakufanya hivyo.

"Baada ya kuelezwa hivyo, hakufanya chochote, akawa anahamasisha kwenye mitandao kuhusu, akaanza kukusanya watu, hakufuata utaratibu kama anakubaliwa au la.

"Kinachofanyika anahojiwa, tunataka kujua kuna nini kinachoendelea kuhusu mipango iliyopo.

"Baadaye tutaangalia mazingira, tutaangalia hiki kinachochunguzwa kama kinadhaminika au tofauti, baada ya mahojiano tutaangalia dhamana kwa mujibu wa Sheria na anatoa ushirikiano mzuri katika mahojiano."
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP. Muliro amepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika leo Novemba 10, 2023 Dar es Salaam, pia amewatahadharisha wananchi kutoshiriki maandamano hayo.

Kwa nini wananchi wawe wanapnywa kutekeleza entitlements za kisheria? Katiba na sheria vinaruhusu maandamano. Polisi wanazuia. Nani wa kumpuuza?
 
Poleni sana Wapalestina wa Bongo.

Walioandaa Maandamano hawana weledi,wangetumia kigezo Cha Kuandamana Ili Hamas Wawaachie Wale Watoto Wetu ,harafu mbele huko inageuka kuwa Takbiir na kulaani Mazayuni.

Bure kabisa 😁😁
---
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezima maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kuanzia viwanja vya Mnazi Mmoja hadi Manzese, huku likikamata baadhi ya viongozi wanaodaiwa kuyandaa akiwemo Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Taarifa za maandamano hayo inayoandikwa kuwa imetolewa na Shura ya Maimamu Tanzania, zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii leo Novemba 10, zikieleza kuwa ni maandamano ya kutetea Mamlaka ya Palestina ambayo yalipangwa kufanyika leo saa 7:30 mchana kuanzia Mnazimmoja hadi Manzese.

Kufuatia taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Jumanne Muliro alitoa taarifa kupitia video kwenye mitandao ya jamii akipiga marufuku maandamano hayo.

Mwananchi Digital ilifika Mnazimmoja na kukuta umati wa watu, huku askari Polisi wenye sare wakiwa wameimarisha ulinzi kuzunguka viwanja hivyo.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom