Taarifa ya jeshi la polisi kuhusu kumsindikiza Edward Lowassa kuchukua fomu ya Urais

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698
Habari wakuu,
Kamanda Kova asubuhi ya leo akiongea na ITV amekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo whatssap kuwa watu wasiokuwa na shughuli mjini wasiingie kwa sababu mgombea wa CHADEMA atakuwa anachukua fomu na foleni itakuwa kubwa pia itahusisha magari, pikipiki, guta, baiskeli na helikopta, pili taarifa hio imesema maandamano yataanzia makao makuu ya CUF Ilala saa tatu asubuhi lakini njia waliyoandaa jeshi la polisi ya kiusalama itaanzia UFIPA, Kinondoni kupitia Salender Bridge kuelekea ofisi za NEC.

Amewaambia wananchi waje mjini kama kawaida kwa sababu wengine rizki yao inategemea kuamka kwake na kujishughulisha asubuhi mpaka jioni na ukiwaachia tu watu kwa ajili ya kuchukua fomu itakuwa tatizo.

''Tunachukua fursa hii kukanusha haya maelezo sio ya kwetu hata jinsi jinsi tangazo lilivyo sio namna yetu ya kuandika taarifa na watu waache kupotosha watu kupitia mitandao kwa sababu masuala ya kiusalama ni nyeti sana''. Amesema maandamano ni kitu Polisi wanaratibu, hivyo anasema njia ambayo wao polisi wameiandaa ni kuanzia CHADEMA kwenda NEC, njia za kupitiana kila ofisi kidogo ina kasoro ambayo italeta madhara kwa wananchi na kisheria mgombea huyu anatokea CHADEMA, pia amesema kumekuwa na juhudi za kutosha kuwasiliana na viongozi wa chama husika na anadhani hata mwenyekiti wa tume ameshawasiliana na viongozi. Jeshi la polisi liko tayari kuwalinda mgombea pamoja na watu wake lakini ni kwa njia ya Kinondoni maana ndio kazi yake ila hio ya kwenda sehemu mbalimbali inaleta tatizo.


Jeshi la Polisi kanda ya Dar imepiga marufuku maandamano ya mgombea wa UKAWA Mh. Edward Lowassa kwenda kuchukua fomu NEC.

Akiongea na ITV kamanda Kova amesema chanzo cha kupiga marufuku maandamano hayo ni

1.0 Kukosekana kwa kibali cha maandamano,

2.0 Kwa nini maandamano yaanzie Buguruni yalipo makao Makuu ya CUF badala ya Kinondoni UFIPA yalipo makao makuu ya CHADEMA ambaye Lowassa ndiye mgombea wao.

3.0 Taarifa za uwongo zilizoenezwa kuwa yeye kamanda Kova ametoa kibali, kwanza amekanusha na kupiga kupiga marufuku taarifa hiyo.

4.0 Tishio la uvunjifu wa amani.

Chanzo: ITV, RAdio One.

======================
Update

Wakati kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam kamishna Suleiman Kova akitoa taarifa za Polisi kuzuia maandamano ya chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ambayo yalielezwa kuanzia Buguruni ofisi za CUF badala ya Kinondoni makao makuu ya CHADEMA kwa ajili ya kumsindikiza mgombea wao kwenda kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais UKAWA.

Kupitia Mwenyekiti mwenza wake ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ameeleza kuwa hawajapata taarifa za zuio hilo kuanzia ofisi za CUF badala yake wataendelea na ratiba yao kama ilivyopangwa.


=================
Update

Jeshi la Polisi jijini Dar limeafiki maandamano ya kumsindikiza kuchukua fomu mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa kwenda NEC kuanzia ofisi za CUF.
 
kamanda kova anahojiwa na itv anataja hoja nyepesi kua UKAWA wamewapa watu hofu ya kuingia mjini leo kutokana na kutangaza wingi wao HIVYO KAKATAZA RASMI MAANDAMANO.


source ITV.
 
Jeshi la Polisi kanda ya Dar imepiga marufuku maandamano ya mgombea wa UKAWA Mh. Edward Lowassa kwenda kuchukua fomu NEC.

Akiongea na ITV kamanda Kova amesema chanzo cha kupiga marufuku maandamano hayo ni

1.0 Kukosekana kwa kibali cha maandamano,

2.0 Kwa nini maandamano yaanzie Buguruni yalipo makao Makuu ya CUF badala ya Kinondoni UFIPA yalipo makao makuu ya CHADEMA ambaye Lowassa ndiye mgombea wao.

3.0 Taarifa za uwongo zilizoenezwa kuwa yeye kamanda Kova ametoa kibali, kwanza amekanusha na kupiga kupiga marufuku taarifa hiyo.

4.0 Tishio la uvunjifu wa amani.

Chanzo: ITV, RAdio One.
 
Magufuli mbona hakupigwa marufuku? Lowassa anaanza kuonja machungu ya kuwa mpinzani sasa!Sio lelema, tumetoka mbali sana sisi wapinzani!
 
Huyu mzee anaharibu utulivu wa jiji tena Leo siku ya kazi , hongererni polisi kwa kuliona hili
 
Wamewaruhusu kuanzia ofisi za CHADEMA mpaka ofisi ya NEC na kurudi. Mpango wa hawa jamaa ilikuwa ni kupitia ofisi zote za vyama vya UKAWA kitu ambacho kingeathiri shughuli za kiuchumi na kijamii hapa center
 
Back
Top Bottom