Taarifa kwa Wanafunzi wote waliochaguliwa UDSM 2015/2016

Ahsante kwa taarifa. Mimi nimechagulia provisionally kupitia NACTE na list za UDSM sijaona jina langu. Can u plz help in this?
 
hata mie nimechaguliwa kupitia nacte lakini jina sijaona na kwenye profile nasubiri confermation kutoka chuoni na mda ndo unakaribia wa kuripoti chuon bro utatusaidiaje hpo
 
naomba kuuliza hapo kwenye kuchukua admission letter je hata cheti cha kuzaliwa kinaweza tumika ??
 
TAARIFA KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE MAIN CAMPUS.

Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) inapenda kuwataarifu wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa tayari wanaweza kufuata kufuata admission letter chuoni.
Hii ni kwa wale waliopo katika mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa. Wanafunzi wote waliochaguliwa na wapo mikoani watachukua admission letter kuanzia tarehe 31 October 2015, tarehe ambayo ndio wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza watafika chuoni rasmi.

Hivyo, ikiwa umechaguliwa kuanza masomo yako ya chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mlimani campus, na Upo Dar es salaam, unaweza kufika chuoni kuanzia kesho tarehe 13 October 2015 na kupata admission letter Jengo Utawala, Room namba 105.

Kuhusu form nyingine Kama form ya uchunguzi Wa Afya, malipo yote ya chuoni n.k zinapatikana mtandao kupitia website ya chuo www.udsm.ac.tz
Ingia kwenye kipengele cha undergraduate na utaona form zote hapo.

Ni vyema kwa wanafunzi wa mikoani kufika tarehe 31 October ili kuanza orientation week.

Ili uweze kupata Admission Letter unalazimika kuja na Kitambulisho chochote kinachoweza kukutambulisha kama Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha mpiga, passport na aina nyingine ya vitambulisho vinavyokubalika.

Imetolewa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Mambo ya nje-DARUSO

Waziri; Yahaya Jalia- 0719 120 001
N. Waziri: Kennedy Mmari-0719579733

this is so useful. .. thnx brothers. me goin to contact u soon..
 
TAARIFA KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE MAIN CAMPUS.

Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) inapenda kuwataarifu wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa tayari wanaweza kufuata kufuata admission letter chuoni.

Imetolewa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Mambo ya nje-DARUSO

Waziri; Yahaya Jalia- 0719 120 001
N. Waziri: Kennedy Mmari-0719579733

@Kennedy Daima Mmari Vipi kuhusu upigaji Kura Oct.25.2015!
Wizara ya habari na Mawasialiano inajibu lolote toka Kwa Jaji Lubuva na NEC yake?.

Je Vyuo vitakuwa vimefunguliwa ?
Je Kama bado wanachuo watapataje haki yao ya kupiga kura?

Kwa faida ya wanachuo over 50.000 TZ nzima naamini mtatoa taarifa.

Back
Top Bottom