Taarab ASLI inavyorudi kwa kishindo

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
sie wengine tushachoshwa na haya mambo ya dumbing down of original taarab ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na hizi redia stations mpya zilizojaa watangazaji na waandalizi wasiojua kitu kuhusu Taarab wala miziki yetu ya Asli


Naam na hawa chini ndio IKHWAAN SAFAA au al maarufu kama Malindi

akhwani%20nadi.jpg
Zaidi ya hawa sie wengine husikiliza EGYPTIAN MUSICAL CLUB na zaidi ABBAS MZEE au CULTURE na kwa mbaali si haba kumsikiliza ustaadhi MUKRIM



WAHENGA walisema 'visima vya kale havifukiwi', bali ni hazina muhimu kwa jamii.

Msemo huo unamaanisha kuwa kuwepo kwa kumbukumbu za kale kunasaidia maendeleo katika jamii, hasa kwa wanajamii kujifunza ni wapi walipotoka, walipo na wapi wanaelekea.

Miongoni mwa mambo ya kale ambayo Tanzania haina budi kujivunia ni kundi kongwe la muziki wa taarabu la Malindi... lililoanzishwa mwaka 1905.

Kundi hili lenye maskani yake katika visiwa vya Zanzibar lilianzishwa katika mwaka huo likijulikana kama Nadi ikwaan Safaa.

Nassor Amour (Cholo Ganuor) ni katibu wa kundi hilo ambaye alifanya mahojiano na Nifahamishe jijini Dar es Salaam wakati kundi hilo lilipokuja kufanya onyesho moja lilokuwa limeandaliwa na kampuni ya Abbas Chezntemba Entertaiment.

Cholo alisema kwamba kundi hilo ambalo kwa sasa lina miaka 104 limeweza kuimba taarabu halisi kwa miaka yake yote jambo ambalo wanaliona kama moja ya mafanikio yake.

Cholo alisema kundi la Malindi katika kipindi chote cha uhai wake limeweza kutoa ajira kwa vijana wengi wa visiwani Zanzibar ambao wengine wamezeekea hapo.

Anasema mziki huo wa taarabu asilia umeweza kukubalika pia katika nchi nyingi za Ulaya hali ambayo inachangia wao kufanya maonyesho katika nchi za mbalimbali za Bara hilo.

Katibu huyo alisema kundi hilo limefanikiwa kutawanyika katika maeneo mengi ya Ulaya na Asia lengo likiwa ni kutoa burudani ambayo imekuwa ikikubalika zaidi.

Cholo anasema taarabu asilia imeweza kuendelea kuheshimika hasa katika Visiwa vya Zanzibar ambapo ndipo palipoasisiwa muziki huo.

Anaendelea kuelezea kuwa muziki wa taarabu asilia umefanikiwa katika nchi nyingi za Ulaya kutokana na ukweli kwamba upigaji wake umeweza kugusa nyoyo za wapenzi wake.

Kiongozi huyo wa kundi alisema kundi hilo lina waimbaji nchini Ufaransa zaidi ya 50 ambao wamekuwa wakifanya maonyesho mbalimbali.

Anasema maonyesho katika nchi hiyo yamekuwa na mafanikio kutoka na wingi watu ambao wanajitokeza kuingia bila kuhofia kiingilio.

"Sisi tunaweza kusema kwamba soko letu lipo kubwa katika nchi za Ulaya kwani tunauza na viingilio vya kule ni vikubwa lakini wanaingia," alisema.

Alisema katika miaka ya hivi karibuni kumeibuka taarabu ambazo zinadai kuwa zinaenda na wakati jambo ambalo alilipinga kwa kusema kuwa mziki wa taarabu unaharibiwa na watu ambao amewataja kuwa wenye tamaa.

Cholo alisema watu ambao wanajigamba kuimba taarabu hapa Tanzania kwa sasa wapo katika maslahi ya muda mfupi tofauti waimbaji wa zamani ambao walizingatia vigezo bora vya taarabu.

Katibu huyo alisema katika kipindi cha miaka 104 wamefanikiwa kuanda zaidi ya albamu 200 ambazo zina nyimbo zaidi ya 3,000.
1714958.jpg

Baadhi ya nyimbo ambazo zimeimbwa na kundi la Malindi ni pamoja na Raha ya Moyo wangu, Zabibu, Uwa, Cheo chako, Leo Tena na Usijigambe.

Aidha aliwataja baadhi ya waimbaji wa kundi la Malindi kuwa Rukia Ramadhani Haji Mohamed, Yussuf Mohamed na Mwanahawa Ally.

Alisema nyimbo hizo na albamu zimeweza kukubalika kwa kiwango cha hali ya juu hivyo kuwapa moyo wa kujiamini na kujituma zaidi.

Akizungumzia changamoto ambazo wanakabiliana nazo ni katika kuhakikisha kuwa mziki huo wa taarabu asilia unakubalika hasa katika nchi za Afrika ambapo kunaonyesha kutawaliwa na mitindo ya kisasa.

Cholo anasema taarabu ambayo inaimbwa kundi hilo inazingatia kuburudisha na kuelimisha jamii ambayo imewazunguka.

Amour alisema kutokana na hali hiyo jamii ya watu wa pwani wanaposikia muziki wa taarabu asilia wanapata ujumbe ambao una manufaa kwao.

Pia alibainisha kuwa katika nchi hii ya Tanzania yapo makundi mawili pekee ambayo yanajihusisha katika uimbaji wa taarabu asilia ambayo ni Malindi na Culture Music Club yote ya Zanzibar.

Alisema ni vema Watanzania wakajaribu kubadilika ili kuendana na muziki ambao una ujumbe wa kutosha na kuachana na ushabiki kutoka kwa makundi mengine ambayo yanaonekana kupotosha kwa makusudi muziki huo taarabu kwa kigezo cha maslahi.

Hilo ndilo kundi la Malindi Innardwan Safaa ambalo maskani yake yapo Zanzibar ambapo lengo lake ni kuhakikisha kuwa taarabu asilia inarudi Tanzania.

Kundi hilo limeonyesha mfano wa kukuza na kuendeleza historia, kwani wameweza kupiga hatua kwa kujifunza na kuyaendeleza yale yote mazuri waliyoachiwa.

Ukweli utaendelea kubakia kwamba watanzania wengi siku hizi wamekuwa wakikumbatia tamaduni za kigeni wakipuuzia utamaduni wetu.

Hapa Tanzania suala la mambo ya kale huonekana kama ujinga na wengi wetu tunaelekeza nguvu zetu katika kuukumbatia utamaduni wa mataifa ya magharibi tukiamini huo ndio muafaka.

Umefika wakati wa kuanza kuenzi tamaduni zetu na kuendeleza yale mazuri tuliyoachiwa.
 
Yaani umenipa mambo ya kinyumbani mambo ya halisi ya kipwani, ya mziki nyororo wa sauti za vinanda na ghani tamu za akina Rukia Ramadhan, Sihaba Juma. Umenikumbusha wimbo mmoja wa Malindi alioimba Mohd Maulid Machapralla uitwao" mtajirusha wenyewe"
Ngoja nikube ubeti mmoja uonje ladha ya marashi ya karafuu:

Mtajirusha wenyewe, roho na akili zenu.
Kisemeni msizuwe, kilichomtoa kwenu.
Na huku kaja mwenyewe, kajua hamna lenu.
Ya bure yenu mayowe, huyu sasa siye wenu.

kiitikio:
Mtajirusha wenyewe, roho na akili zenu x2
Na mseme, x2 msizuweee kilicho mtowa kwenu.

Yaani raha hizi tunazikosa siku hizi kwa hizi vurugu mechi na matusi wanayoita "modern taarab'.
 
Hapo sijakupa kipande kimoja kitamu cha shairi kilichowahi kuimbwa na kundi hilo na Al marhum ,gwiji, ustadh, Seif Salim katika wimbo wa "kheri Pendo la NdoNdoNdo"

Kheri pendo la Ndo! ndo! la chururu linadhara.
Wacha pupa na vishindo, Mapenzi siyo papara.

shairi:
kusabilia mahaba, siyo kwangu masikhara.
Ukishindwa kuyabeba, itakufika idhara.
Nitakupa habahaba, usije kula khasara.

Halafu hapo unafuata mziki lainiiiiiiiiiii wa vinanda ghani kali kutoka kwa gwiji hilo lililotamba katika enzi za uhai wake kwa tunzi, kuimba na kuweka muzeka.Yaani raha kwenda mbele
 
Naam hapa namsikiliza ABBAS MZEE wa kile kikkundi cha EGYPTIAN anakwambia

Harusi Furaha yaaake....
haina mwanzo wala Mwisho...

Harusi Furaha yakeee
Haina mwanzo wala mwisho...


akh...

halafu ntawasahau vipi CULTURE na usaadhi MUKRIM?
Wazazi wa pande zoote
Huwapamoja kwenye chereko cheroko
 
KAMA UKO dAR BASI KUNA DUKA MOJA LIKO iLALA BOMA naweza kukupa contact lakini pale unakwenda kwa appointment kwa sababu ya msululu wa watu wanaotaka hizi OLDIES
 
Mkuu nimekupata. Mie naona umenifikisha nilipokuwa napataka. Sasa hakuna taarab bali dansi la gambusi. Huyu kijana Mzee Yusuf angejua alifanyalo katika kuua muziki huu nadhani angejuta kuingia katika uga huu. Siku ya kuporomoka kwake kwa umaarufu zinahesabika. Namshauri asikate tamaa kujifunza ni kwa nini wakongwe kama Maulid Machaprala, Chimbeni Kheri na wengineo bado wanavuma? Game nitumie mawasiliano yao
 
mimi mkenya tena mbara lakini napenda raha z pwani
Aidha napenda nyimbo za taarab sana

Nawaomba mashabiki mnipe namna nitaweza kuipata rekodi moja kali sana ya TANGA KUNA RAHA

Hii huniamsha ari ya mahaba na raha

Iwapo mna mmoja wetu atakayenitumia rekodi hii, mie niko tayari kumstiri kiuchumi na gharama \\

Kwa kheri
 
Ukiwaacha malindi kuna wakongwe kama Matano Juma **** Juma bhalo na pete ilo kidoleni iliyomsababishia tifu Zenj akatolewa mkuku yaani ni raha tupu.Mambo ya mod kina bwabwa na welawela vijiwe vyao basi tabu tupu kama si karaha kabisa.HISHIMA ZIRO AIBU TUPU.lakini hata muziki wa dansa kote ni lahaula tupu na ubongo fever.
 
Ukiwaweka kando hao malindi pana majina ambayo ni aghalabu kuyasahau.MATANO JUMA, JUMA BHALO na pete yake iliyomtoa kamasi ZENJ Yaani ni raha tupu. Sio leo mod taarabu za kina bwabwa na kina WELAWELA upuzi kama sio wehu mtupu.hakuna heshima .Taarabu imeenda upogo raha hakuna:mad:
 
Mbona mnafanya vichekesho? swahili music from Tanzania and kenya from the 1920s to the 1950 , Hivi Tanzania wakati huo ilikuwa au ilijulikana kuwa inakuja ? tuwe wakweli baadhi ya wakati uongo mwingi humletea mtu kufa kifo cha kuhudhunisha.
 
Kuna mtu analoshairi la nyimbo ya ISSA MATONA sina jina lakini kibwagizo chanke ni AJE AHAYA...NA BIBI YAKE HARUUSI NAYE AJE HAPA

Nahitaji mashairi ya nyimbo nzima kama kuna mtu anayo tafadhali hebu nimwagie humu kuna kipande nataka nimtumie mtu ana nisumbua sana
 
Naam hapa namsikiliza ABBAS MZEE wa kile kikkundi cha EGYPTIAN anakwambia

Harusi Furaha yaaake....
haina mwanzo wala Mwisho...

Harusi Furaha yakeee
Haina mwanzo wala mwisho...


akh...

halafu ntawasahau vipi CULTURE na usaadhi MUKRIM?
Wazazi wa pande zoote
Huwapamoja kwenye chereko cheroko

EEEEEEE h unanifanza mate yanitoke hio nyimbo leo ni mwaka wa tatu nnaitafuta kwa hamu sijaipata, naomba kama inawezekana ukatutumbukizia humu takarahika pamoja
 
Back
Top Bottom