Elly B
JF-Expert Member
- Jan 11, 2011
- 1,194
- 906
Umeshindwa kuelezea suala hili chronologically? ... au unataka kuupindisha ukweli na kuhusisha ugomvi wa Kagame na JK kama ndiyo chanzo.
Malalamiko yalianza muda mrefu kutoka kwa wenyeji. Kumyanyasa na kumwibia mali binadamu yeyote ni kosa, tunajua hilo.
Ndugu Kobelo,
Ni kweli malalamiko ya wenyeji yalianza siku nyingi. Lakini kwa nini hatua hizo ziwe sasa? Kwani hiyo siku nyingi Rais na serikali yake walikuwa wapi? Kwani wakati wahamiaji hao wanahamia kienyeji, iwe ni kwa kutoroka makambi ya wakimbizi au kuvuka mpaka kienyeji serikali ilikuwa wapi?
Lina kuja hili la haki za hawa wahamiaji kikatiba. Katiba yetu imetamka wazi binadamu wote, watu wote kuzaliwa HURU na KUWA NA HAKI SAWA MBELE YA SHERIA. Ni kweli Wanapaswa kurejeshwa kwao kama wamekuwa humu kinyume na sheria zetu. Lakini siyo kwa kufukuzwa kienyeji. What is the meaning of diplomacy then? Ni mara ngapi hata wafungwa wanaporejeshwa makwao kunafanyika mawasiliano baina ya nchi husika, utaratibu wa kuwakabidhi na kuwapokea unafanyika kwa murua kabisa? Ni kweli kwamba Wafungwa wana hadhi kuliko hawa wageni?
Halafu kifuate hiki kipengele cha nasaba kati ya nchi jirani na wananchi waishio mipakani. Kwa waliowahi kuishi mipakani watakuwa mashahidi kuwa ni vigumu kuzingatia mpaka wa nchi. Ukienda maeneo hayo ni kawaida kuona mtoto anatoka asubuhi kwenda shule "Kenya" kwa sababu ni karibu na nyumbani kuliko ya "Tanzania" hata kama ni kwa kilomita 1. Kule ni kawaida mtu kukwambia naenda kwa mjomba ikawa anaenda "Kenya" au kukuta mtu anaaga naenda kisimani na ikawa anaenda kuchota maji Burundi. Mwisho wa siku, pamoja na malalamiko yote, siyo halali sana kuwafukuza tu kienyeji kwa sababu wengine ni Wajomba zao na Wahaya flani au ni mama mdogo wa rafiki yako wa pale mpakani na huenda mama mzazi wa Mtanzania flani! Na Kama wamekuwa "Wahamiaji Haramu" ghafla, nataka kukubaliana, kwa mantiki hiyo ya nasaba na kulinda utu, na mwana JF mmoja aliyewatambua hawa wageni kwa mtazamo wa "Wajomba zetu Haramu", "mama zetu haramu" au "Mkeo haramu" (Which is Mbaya)...Na kama wote ni wahalifu basi nasikitika kwani kuna wake za wenzetu siyo "Wananchi kabisa" na wengine wetu ni mapolisi wakuu (Law upholders)! What do you think. In the end hawa ni binadamu wa kawaida! Kuvunjika kwa sheria za uhamiaji hakuwatoi ubinadamu wao!. Jamani hata muhalifu pia ana haki zake.
Vyovyote inavyokuwa kitendo kile kilifanyika kwa jazba za kiongozi na kwa hasira ya matusi ya Rais wa jirani na si kwa kujali sana vilio vya wananchi. Na sitaki kuamini kuwa kwa vilio vya muda huo mrefu ndiyo Rais anavisikia juzi!
Mwisho nahitimisha kwa kusema ni vema tukawa mfano kwa wenzetu kwa vile tunavyotaka watufanyie sisi. Kama wote tungefanya hivyo sidhani kama kungekuwa na mahusiano mazuri na yeyote duniani. Imagine the world where ukipata wageni waliovunja sheria unawakusanya tu unakwenda nao mpakani kwao unawabwaga hapo na kuondoka! Kwamba na China ikusanye wale wauza unga "wetu" wote iwasafirishe mpaka bandarini iwaache kienyeji. Au Afrika ya Kusini ijibebee kina "Masogange wetu" wote ije iwamwage mpakani na kuondoka kimyakimya! Jamani kutakuwa kumebaki thamani ya ubinadamu duniani?......Ile ilikuwa hasira na haikuwa sawa. Siyo kitendo cha mfano wala hakifai kuigwa na si cha kupongezwa kwa namna yoyote hasa kufanywa na kiongozi tena mwenye washauri kibao.
Binafsi naona Mwanakijiji is right. And I do apologize, sincerely, if my understanding is contradictory to yours.