Jaluo_Nyeupe
JF-Expert Member
- Dec 21, 2010
- 2,697
- 1,962
Polisi hawajishughulishi na kesi za wanandoa au wapenzi kwa sababu mara nyingi zimekaa kutishiana tishiana zaidi na hakuna dhamira ya dhati ya kushitakiana. Kama kweli umedhamiria kwa dhati kupata haki yako mahakamani waeleze hilo polisi na hawawezi kukupuuzia kwani hawana mamlaka kisheria kuzuia makosa ya jinai yasifike mahakamani.