Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
"Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."
Wafuasi wa Simba walilipuka kama gas iliyoshika moto kwa kutaka atolewe nje ya ukumbi. Mwenyekiti wa uchaguzi Profesa Tibaijuka alitumia mamlaka yake kumlinda Shyrose Bhanji asitolewe njie kwa vile ni haki yake kumwuliza swali mgombea.
Jibu la Sofia Simba kwa swali la Shyrose lilikuwa jepesi kama ifuatavyo:
"Inaonekana aliyeuliza swali hajakomaa katika siasa za nchi, ndio maana ameambulia kuzomewa na wajumbe wa mkutano huu. Habwatuki bungeni au majukwaani kwa vile yeye ni serikali, na hata mbunge wa CCM hapaswi kukikosoa chama chake. Mimi si mithili ya upinzania kukaa na kukiosoa chama napaswa kukitetea. Anayesema Sofia Simba hajafanya kitu anajidanganya kwani wapiga kura wako kwenye matawi, kata, wilaya na mikoa, hao ndio wapiga kura wa chama na mimi kama mwenyekiti wa UWT nilijiimarisha katika ngazi za chini."
Note:
Note:
Shyrose alielekeza swali gumu pia kwa Anne Kilango Malecela kabla ya kumwuliza Simba. Swali lilikuwa kama ifuatavyo:
"Nini kimekusukuma kugombea uenyekiti UWT."
Swali hilo lilikingiwa kifua na Mwenyekiti wa Uchaguzi profesa Tibaijuka kwa kulikataa. Shyrose alipopata tena nafasi ya kumwuliza Simba ndipo yakajilia haya tunayojadili.