Tumeshuhudia mateso makali na ya kinyama aliyofanyiwa Dr Ulimboka, alitekwa akapigwa kwanza ndani ya gari na baadaye katika Msitu wa Pande, ambako ndiko alikokutwa asubuhi akiwa hoi bin taaban. Madaktari wenzake wanasema kavunjwa mbavu, mikono na taya. Pia kangolewa meno mawili ya mbele na kunyofolewa kucha.
Sasa viongozi wanasema hawahusiki na tukio hilo lakini waathirika wanasema wanamjua mhusika. Hakuna anayemtaja mbele za watu mhusika huyo ni nani, lakini kwenye vijiwe, kila mtu anataja kuwa serikali inahusika na kwamba wahusika ni Kijitonyama.
Ukiuliza Kijitonyama ni nani, wanasema ni wenyewe hao hao serikali. Kiongozi wa nchi kasema serikali haihusiki lakini yaelekea raia hawamwamini na hawaiamini serikali kuwa haihusiki. Lakini mngoaji meno, mvunjaji mbavu, mikono na mataya atakuwa nani na kwa nini?
Na kwa nini mtu mwenyewe anayevunjwa mikono, mbavu na taya ni yule tu mwenye ugomvi na serikali? Kama ni kweli waliompiga Dk. Ulimboka, wakamvunja taya, mikono, mbavu na wakamnyofoa kucha walikuwa wakimhoji eti nani wanakutumia kuongoza migomo, je, ni nani hao wapigaji?
Source: ************************** wavuti - wavuti