Ni kwa sheria ipi serikali inalazimika kusubiri utaratibu wa bunge kuwachukulia hatua wezi na mafisadi waliotajwa na CAG?

Trable

JF-Expert Member
Jan 3, 2023
1,783
3,281
Kwa mjibu wa tamko la kiongozi wa shughuri za bunge letu Sipika Dr Aksoni Tulia kwamba, bunge la kushughurikia wezi waliotajwa kutoka katika wizara mbalimbalu na mkaguzi wa hesabu za serikali CAG kwamba, kwa mjibu wa kanuni na sheria za Bunge, Bunge linaloendelea ni bunge la bajeti peke yake, na hivyo ripoti ya CAG, itajadiliwa katika bunge lijalo!

Sasa Najiuliza hapa kuhusiana na sheria zetu,

1:Kwa sababu hiyo, serikali nayo inabidi ikae kimya ikisubiri kile bunge limeadhimia na kwamba serikali haipaswi kabisa hata kujua pesa zake ni nani amezikwapua na wala haiwezi kushughuulikia ripoti hiyo kwa namna yoyote?

2: Kati ya serikali na Bunge, ni yupi aliyeibiwa pesa? Na kama ndiyo serikali imeibiwa, kwa nini haiwezi kuchunguza wizi huo na kuchukua hatua mpaka kusubiri idhini na ama uchambuzi wa bunge?

3: Kati ya Bunge na serikali ni nani humlipa mwenzake mshahara? Kama ni Serikali, kwani haioni kwamba kutokuchukua hatua sasa inapoteza pesa nyingi na hasara kubwa kusubilia bunge ambalo kila mwezi hutega mikono yake kulipwa posho, mishahara n.k huku likichelewesha uchunguzi wa pesa ambayo serikali imepata hasara?

4: Kati ya serikali na Bunge, ni nani anapaswa kuwa mkali linapokuja suala la wizi na upotevu wa pesa za wananchi?

5: Kati ya Bunge na Serikali, ni nani hasa akiwa legelege atasababisha serikali au bunge na kila kitu kuwa legelege, vile vile ni nani akiwa strong na mwenzake atakuwa strong katika kulinda mali na matumizi ya pesa za Serikali?

7: Lakini katika hali ya kawaida, upotevu na ufisadi uliotajwa na CAG, Ni halali kwa sipika kutangaza hadharani kwamba, Bunge lake linatoa muda wa miezi sita kushughurikia ripoti hiyo?

8:Kama ni kweli, Ya nini sasa kwa ofisi ya CAG kuwa anafanya ukaguzi na kuiwasilisha Bungeni katika kipindi ambacho yeye na serikali pamoja na Bunge wanajua kabisa kwamba haitashughurikiwa kwa sababu ya kanuni na sheria za kibunge?

9: Kama ni kweli serikali, Bunge na ofisi ya CAG wanalijua hilo, kwa nini wanakubali kukaa na sheria mbovu namna hiyo na wao kukubali kupoteza pesa kufanya ukaguzi ambao wanajua haitashughurikiwa?

Au ndiyo kuferi na kuwa na serikali legelege isiyo na meno dhidi ya mafisadi?

Karibuni wajuvi na wabobevu wa sheria zetu ili mtujuze

Tanzania ni yetu sote!

Kisamv....Kwa sasa nipo katika kisiwa cha Mafia!
 
1:Kwa sababu hiyo, serikali nayo inabidi ikae kimya ikisubiri kile bunge limeadhimia na kwamba serikali haipaswi kabisa hata kujua pesa zake ni nani amezikwapua na wala haiwezi kushughuulikia ripoti hiyo kwa namna yoyote
CAG ametumwa na bunge kukagua hesabu za serikali Kuu. Hata bajeti yake inaandaliwa na kamati ya bunge na sio mawaziri/serikali. Maana huwezi pendekeza bajeti ya kukaguliwa!
2: Kati ya serikali na Bunge, ni yupi aliyeibiwa pesa? Na kama ndiyo serikali imeibiwa, kwa nini haiwezi kuchunguza wizi huo na kuchukua hatua mpaka kusubiri idhini na ama uchambuzi wa bunge
Pesa ni za UMMA ila serikali imepewa mamlaka kuzitunza na kuzisimamia ila matumizi yake yanaidhinishwa na bunge, so wakizitapanya wanahojiwa na bunge na kuwajibishwa na bunge. So anayeibiwa ni bunge sio serikali!!

3: Kati ya Bunge na serikali ni nani humlipa mwenzake mshahara? Kama ni Serikali, kwani haioni kwamba kutokuchukua hatua sasa inapoteza pesa nyingi na hasara kubwa kusubilia bunge ambalo kila mwezi hutega mikono yake kulipwa posho, mishahara n.k huku likichelewesha uchunguzi wa pesa ambayo serikali imepata hasara?
Serikali inajichunguzaje na kujichukulia hatua? Lazima kuwepo na oversight body/Kiranja kama Bunge ndio ichukue hatua kupitia maazimio ya bunge baada ya ripoti kujadiliwa.

Ucheleweshaji ni udhaifu wa kanuni za bunge kwamba lazima PAC ipitie upya ripoti ya CAG na iite taasisi Moja Moja itoe maelezo then wafikie hitimisho Sasa hayo yote ndio yanafanyika kwa miezi kadhaai!! Na mwishowe ndio ripoti ya PAC inapelekwa bungeni kwa majidiliano zaidi.
4: Kati ya serikali na Bunge, ni nani anapaswa kuwa mkali linapokuja suala la wizi na upotevu wa pesa za wananchi
Bunge ndio wanapaswa kuwa wakali maana ndio wanawakilisha UMMA ambao ndio Kodi zao zinatunzwa na serikali kwa niaba Yao.

5: Kati ya Bunge na Serikali, ni nani hasa akiwa legelege atasababisha serikali au bunge na kila kitu kuwa legelege, vile vile ni nani akiwa strong na mwenzake atakuwa strong katika kulinda mali na matumizi ya pesa za Serikali?
Bunge wakiwa wakali serikali haiwezi kuwa ya kifisadi. Unakumbuka bunge la 9 mbona serikali ilijaa ufisadi ila bunge liliwanyoosha sana.
7: Lakini katika hali ya kawaida, upotevu na ufisadi uliotajwa na CAG, Ni halali kwa sipika kutangaza hadharani kwamba, Bunge lake linatoa muda wa miezi sita kushughurikia ripoti hiyo?
Udhaifu wa kikanuni huu kumbuka ripoti ni ya 2021-22 ilihali tupo 2023. Nadhani inabidi CAG awe anatoa ripoti January Ili zijadiliwe mapema kuliko kuzichelewesha zinatoka wakati wa bunge la bajeti.
9: Kama ni kweli serikali, Bunge na ofisi ya CAG wanalijua hilo, kwa nini wanakubali kukaa na sheria mbovu namna hiyo na wao kukubali kupoteza pesa kufanya ukaguzi ambao wanajua haitashughurikiwa?
Kanuni hizo zilitungwa na CCM Ili kulinda mafisadi. Maana mpaka PAC ijadili unakuta watu walishahama vitengo so hatua inakua ngumu kuchukuliwa na hata ushahidi kufunikwa.
 
Bunge lililopatikana kwa wizi wa kura litapata wapi nguvu ya kukemea wezi wengine?
Pepo akimtoa pepo huo utawala umefitinika.
Wanacho weza kufanya wakiwa ktk vikao vyao vya kahawa ni kusema tuu ila wenzetu mmepiga pesa nyingi jamani tuchoteeni na wenzenu.
Kama walivyo fanya ktk ujambazi wao wa Tegeta escrow mipesa lizolewa Bank na haya majizi kama ifuatavyo

Mwenye sandarusi hayaa
Mwenye kiroba hayaa
Mwenye gunia hayaa
Mwenye kikapu hayaa
Mwenye tolori hayaa
Mwenye mabegi hayaa
Menye sufuria hayaa
Nchi imechezewa hii na haya ma ccm kupita kiasi haya lazima kufurumushwa kwa lazima.
 
Bunge lililopatikana kwa wizi wa kura litapata wapi nguvu ya kukemea wezi wengine?
Pepo akimtoa pepo huo utawala umefitinika.
Wanacho weza kufanya wakiwa ktk vikao vyao vya kahawa ni kusema tuu ila wenzetu mmepiga pesa nyingi jamani tuchoteeni na wenzenu.
Kama walivyo fanya ktk ujambazi wao wa Tegeta escrow mipesa lizolewa Bank na haya majizi kama if unavyo

Mwenye sandarusi hayaa
Mwenye kiroba hayaa
Mwenye gunia hayaa
Mwenye kikapu hayaa
Mwenye tolori hayaa
Mwenye mabagi hayaa
Nchi imechezewa hii na haya ma ccm kupita kiasi haya lazima kufurumushwa kwa lazima.
Doh!
 
Kukosekana kwa dollar hapa Tanzania ni kwa sababu moja kuu na isije tokea gazeti likakudanganya huu ndiyo ukweli wizi alioibua CAG umetishia uchumi wa nchi. Kwasababu viongozi croocks wamefungua account za benki dubai na qatar.

Hizo fedha walizoiba wezibadilisha kuwa dollar ili waweze kudeposit kwenye mabenki ya nje ya bara la Afrika. Ukweli ni kwamba namba moja tumuombee sana. Raisi anapitia kipindi kigumu sana kuchagua kati ya kulipa wema au kufata majukumu yake kikatiba. Imagine mtu anaiba billion 1 akibadilisha kuwa dollar ni kama 250,000 milioni dollars hivi kirahisi hivo? Mtu kupata hela nyingi hivyo kwa mara moja?

Mimi nina declare maishani kwangu siwezi kuiba bilioni moja au zaidi kwakuwa nitakuwa nimedhulumu mamilioni ya watanzania wenzangu. Sio haki kuiba pesa ambazo umeaminiwa kuzilinda.
 
Kwa mjibu wa tamko la kiongozi wa shughuri za bunge letu Sipika Dr Aksoni Tulia kwamba, bunge la kushughurikia wezi waliotajwa kutoka katika wizara mbalimbalu na mkaguzi wa hesabu za serikali CAG kwamba, kwa mjibu wa kanuni na sheria za Bunge, Bunge linaloendelea ni bunge la bajeti peke yake, na hivyo ripoti ya CAG, itajadiliwa katika bunge lijalo!

Sasa Najiuliza hapa kuhusiana na sheria zetu,

1:Kwa sababu hiyo, serikali nayo inabidi ikae kimya ikisubiri kile bunge limeadhimia na kwamba serikali haipaswi kabisa hata kujua pesa zake ni nani amezikwapua na wala haiwezi kushughuulikia ripoti hiyo kwa namna yoyote?

2: Kati ya serikali na Bunge, ni yupi aliyeibiwa pesa? Na kama ndiyo serikali imeibiwa, kwa nini haiwezi kuchunguza wizi huo na kuchukua hatua mpaka kusubiri idhini na ama uchambuzi wa bunge?

3: Kati ya Bunge na serikali ni nani humlipa mwenzake mshahara? Kama ni Serikali, kwani haioni kwamba kutokuchukua hatua sasa inapoteza pesa nyingi na hasara kubwa kusubilia bunge ambalo kila mwezi hutega mikono yake kulipwa posho, mishahara n.k huku likichelewesha uchunguzi wa pesa ambayo serikali imepata hasara?

4: Kati ya serikali na Bunge, ni nani anapaswa kuwa mkali linapokuja suala la wizi na upotevu wa pesa za wananchi?

5: Kati ya Bunge na Serikali, ni nani hasa akiwa legelege atasababisha serikali au bunge na kila kitu kuwa legelege, vile vile ni nani akiwa strong na mwenzake atakuwa strong katika kulinda mali na matumizi ya pesa za Serikali?

7: Lakini katika hali ya kawaida, upotevu na ufisadi uliotajwa na CAG, Ni halali kwa sipika kutangaza hadharani kwamba, Bunge lake linatoa muda wa miezi sita kushughurikia ripoti hiyo?

8:Kama ni kweli, Ya nini sasa kwa ofisi ya CAG kuwa anafanya ukaguzi na kuiwasilisha Bungeni katika kipindi ambacho yeye na serikali pamoja na Bunge wanajua kabisa kwamba haitashughurikiwa kwa sababu ya kanuni na sheria za kibunge?

9: Kama ni kweli serikali, Bunge na ofisi ya CAG wanalijua hilo, kwa nini wanakubali kukaa na sheria mbovu namna hiyo na wao kukubali kupoteza pesa kufanya ukaguzi ambao wanajua haitashughurikiwa?

Au ndiyo kuferi na kuwa na serikali legelege isiyo na meno dhidi ya mafisadi?

Karibuni wajuvi na wabobevu wa sheria zetu ili mtujuze

Tanzania ni yetu sote!

Kisamv....Kwa sasa nipo katika kisiwa cha Mafia!
Kisamvu
Nenda hapo halmashauri ukawaulize internal auditor kazi zake ninini? Hoja za mkaguzi zikija tu mezani kwa DED wakuu wa idara wanafukuzwa kazi bila kuzijibu kwanza? Kama upo serikalini basi wewe ni njuka na hujui namna serikali inavyofanya kazi.
Hoja za CAG Ni tuhuma mpaka zijibiwe ndo unakuwa ubadhirifu mkuu.
 
Back
Top Bottom