Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,573
- 19,456
Tarehe 5 mwezi februari mwaka 1977 nikiwa mwanafunzi wa Form 3, nilikuwa mmojawapo wa waliochukuliwa kutoka shuleni kwetu kuunda gadi moja ya kucheza halaiki tukishirikiana na wanafunzi wa shule za msingi.
Katika hotuba yake Mwalimu Nyerere aliyoitoa kutokea uwanja wa Aman kule Zanzibar alituahidi kuwa waliamua kuunganisha vyama vya TANU na ASP ili kuunda chama kiomoja chenye nguvu kitakacholeta mapinduzi ya haraka kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa watanzania wote. Wakati huo TANU ilikuwa imefikisha umri wa miaka 23 wakati ASP ilikuwa na umri wa miaka 20 tu. Katika kipindi cha uhai wa vyama hivyo vya TANU na ASP vilikuwa vimeshaleta mafanikio makubwa sana nchini. Vyote viliondoa ukoloni nchini na vilikuwa vimeshaanza kuboresha maisha ya mtanzania. Vilijenga mazingira ambamo wanachi walikuwa wanajivunia nchi yao na viongozi walikuwa wanajua kuwa wao ni watumishi wa wananchi; malalamiko ya wananchi yalikuwa yakichukuliwa kwa uzito sana na ule msingi wa CHEO NI DHAMANA ulikuwa na uzito sana.
Leo hii ni miaka 31 tangu CCM izaliwe; huo ni umri mkubwa sana zaidi ya ule wa vyama vilivyoizaa. Mazingira yaliyojengwa na chama hiki ni yale ambamo wananchi hawana imani na utawala, na vile vile watawala wamekuwa hawaogopi malalamiko ya wananchi. Yote hayo kwa pamoja yameondoa uzalendo kabisa miongoni mwa watu wetu ambapo, viongozi wetu bila woga wanaweza kusaini mkataba wa kukodisha yetu kwa mtu mwingine milele!! !!. na mtu akiuliza kulikoni, basi anapewa vitisho vikali.
Mfano mzuiri ni hili tishio lililotolewa na Katibu Mkuu wa CCM dhidi ya kijana Nape Nnauye kufuatia tamko lake kuhusu ufisadi ndani ya UVCCM. Tihio hilo linaonyesha jinsi gani chama hicho kinavyoheshimu mafisadi na kuwapuuza wananchi tofauti na ilivyokuwa wakati wa TANU na ASP. Kwa nini Makamba amtishie kijana yule badala ya kumtaka alete ushahidi ili yeye (Makamba) aweze kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watuhumiwa hao badala ya kutoa onyo kabla ya kuangalia ushahidi unasemaje. Huko siyo kujenga mazingira ya mapinduzi.
Ndiyo maana najiuliza, je kweli chama hiki bado ni chama cha Mapinduzi yale tuliyoahidiwa mwaka 1977?