Swali: CCM ni Chama Cha 'Mapinduzi' Yepi?

unashangaa nini matokeo kupinduliwa?Mosi, Chama chenyewe ni cha MAPINDUZI, kwa hiyo kupindua matokeo si jambo la ajabu.Pili, Viongozi wake wote wa juu ni WanajeshiMwenyekiti: Luteni Kanali Jakaya KikweteKatibu Mkuu: Luteni Yusuf MakambaNaibu Katibu Mkuu: Kapteni George MkuchikaKatibu wa Itikadi/Uenezi: Kapteni john ChiligatiMeneja Kampeni: Kanali Abdulrahaman KinanaTatu, Gazeti la Serikali, Daily News ambalo editor in Chief ni Rais, limeshasema: Dk. Slaa hatakuwa rais wa tano wa TanzaniaNne: Tamko la Luteni Jenerali Shimbo linajieleza: "Wagombea wakubali matokeo, la sivyo..."Tano: Katiba ya nchi/ sheria ya uchaguzi iko wazi: Matokeo ya urais yakishatangazwa, hakuna chombo chochote kinachoweza kuyapinga.
*
Sasa mnashangaa nini eti mnajidanganya bila kujua kuwa nchi hii ni ya utawala wa kijeshi.
*
Haya nendeni mkapige kura kutimiza haki yenu ya kikatiba, narudia tena kutimiza haki yenu ya kikatiba.Nawasilisha
 
Message za aina hii mimi sizifagilii kabisa. Wakati mwingine wafuasi wa CHADEMA mnasambaza message ambazo mnadhani ni za kuwasaidia, kumbe ni za kuwamaliza. Ukishasambaza message ya kwamba CCM ni chama cha kijeshi na kwamba kura zitaibiwa, huoni kwamba unawakatisha tamaa baadhi ya wanamageuzi ambao wataona hakuna sababu ya kupiga kura kwakuwa hata wakipiga zitaibiwa? Tutiane moyo na tuhamasishane kwenda kupiga kura kwa maana ya kuchagua Rais ambaye ana uchungu na nchi yetu na yupo kwa maslahi ya taifa na si kupiga kura kwa ajili ya kutimiza haki yetu.
Tuwe waangalifu na aina ya ujumbe ambao tunausambaza jamani.
 
mkuu hutakiwi kukata tamaa kiasi hicho kwani wewe kama great thinker unatakiwa kutoa matumaini kwa watanzania ili kwa kupitia kwako waweze kujipa moyo na kwenda kutekeleza haki hiyo ya kikatiba.
 
unashangaa nini matokeo kupinduliwa?Mosi, Chama chenyewe ni cha MAPINDUZI, kwa hiyo kupindua matokeo si jambo la ajabu.Pili, Viongozi wake wote wa juu ni WanajeshiMwenyekiti: Luteni Kanali Jakaya KikweteKatibu Mkuu: Luteni Yusuf MakambaNaibu Katibu Mkuu: Kapteni George MkuchikaKatibu wa Itikadi/Uenezi: Kapteni john ChiligatiMeneja Kampeni: Kanali Abdulrahaman KinanaTatu, Gazeti la Serikali, Daily News ambalo editor in Chief ni Rais, limeshasema: Dk. Slaa hatakuwa rais wa tano wa TanzaniaNne: Tamko la Luteni Jenerali Shimbo linajieleza: "Wagombea wakubali matokeo, la sivyo..."Tano: Katiba ya nchi/ sheria ya uchaguzi iko wazi: Matokeo ya urais yakishatangazwa, hakuna chombo chochote kinachoweza kuyapinga.

*
Sasa mnashangaa nini eti mnajidanganya bila kujua kuwa nchi hii ni ya utawala wa kijeshi.
*
Haya nendeni mkapige kura kutimiza haki yenu ya kikatiba, narudia tena kutimiza haki yenu ya kikatiba.Nawasilisha

Sijajua kama watu wenye sifa za kijeshi kuwemo katika utumishi ama utawala wa nchi kunafanya utawala huo kuitwa wa kijeshi ama kuwa wa kijeshi. Ninapata walakini na namna ujumbe huu ulivyoumbwa na unachokusudia kukileta.

Hata hivyo, si dhani kama tulipofikia kwa sasa panaonesha kweli kwamba kupiga kura ni haki ya Kikatiba, mbona wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma wamepokwa haki hiyo kama ni ya kikatiba kweli?
 
kunjygroup au Kinjegroup?

Unaogopa kivuli chako mwenyewe? Kumbe tatizo unaliona kabisa kwa macho yako na akili yako inatambua hilo.. unafikiri hakuna njia nyingine ya kuweza kurekebisha hayo? NJIA NI KUPIGA KURA, NA MATOKEO YAWE YA UWAZI NA UKWELI KWA KUSIMAMIWA NA WEWE MWENYEWE NA MUHIMU ZAIDI NI KUHAKIKISHA KILICHOHESABIWA NDO KINATANGAZWA!! KINYUME NA HAPO INABIDI UHOJI KWA NGUVU.

kunjygroup, acha woga na kukata tamaa - jiamini na utashinda. Kampigie kura Dr. Slaa uepukane na ujima huu.
 
Well. Thanx 4 yo contributions great thinkers.
Sijakata tamaa kabisa. Mie ni great activist wa vijana kudai mabadiliko na kuwahamasisha kupiga kura. The msg i posted came in my email inbox so i put it so that i get your reaction.
Mapambano daima. Slaa rais wetu 2010. Naenda Mbeya kuangalia Sugu anavyoutikisa mji
 
kupiga kura ni lazima kwa kila mwananchi acha woga nenda kapige kura ushindi unakuja hata kama wataiba zikiwa nyingi sana hawataweza kuiba zote
 
unashangaa nini matokeo kupinduliwa?Mosi, Chama chenyewe ni cha MAPINDUZI, kwa hiyo kupindua matokeo si jambo la ajabu.Pili, Viongozi wake wote wa juu ni WanajeshiMwenyekiti: Luteni Kanali Jakaya KikweteKatibu Mkuu: Luteni Yusuf MakambaNaibu Katibu Mkuu: Kapteni George MkuchikaKatibu wa Itikadi/Uenezi: Kapteni john ChiligatiMeneja Kampeni: Kanali Abdulrahaman KinanaTatu, Gazeti la Serikali, Daily News ambalo editor in Chief ni Rais, limeshasema: Dk. Slaa hatakuwa rais wa tano wa TanzaniaNne: Tamko la Luteni Jenerali Shimbo linajieleza: "Wagombea wakubali matokeo, la sivyo..."Tano: Katiba ya nchi/ sheria ya uchaguzi iko wazi: Matokeo ya urais yakishatangazwa, hakuna chombo chochote kinachoweza kuyapinga.
*
Sasa mnashangaa nini eti mnajidanganya bila kujua kuwa nchi hii ni ya utawala wa kijeshi.
*
Haya nendeni mkapige kura kutimiza haki yenu ya kikatiba, narudia tena kutimiza haki yenu ya kikatiba.Nawasilisha
.

Dr Slaa ni raisi wa 31 oct.

Waulize Karatu wamipateje ukombozi kwa kumchagua Dr Slaa, haikuwa rahisi na kama kuiba waliiba yeye mwenyewe ana ushahidi wa mahakama. Ila Kupiga Kura na kusimamia ndio jibu.

usikate tamaa saa ya ukombozi imeshafika, Katiba inabadilishwa, hakuna nguvu nyingine zaidi za People power.
 
ni kweli...lakini kumbuka tukiungana kwa pamoja...hao wote watakuwa ni kama tone la maji kayika bahari!!
 
Haki ya mtu haiombwi,ondoa woga piga kura chagua kiongozi unayemuona anamwelekeo wa kuwa kiongozi bora si bora kiongozi.Woga hautusaidii bali unatudumaza.
 
Kuna kitu kinaitwa status quo....na kuitetea status quo!? CCM ilianzishwa kufanya mapinduzi si kwa watanzania tu bali Afrika nzima. Kipindi icho ilikua mapinduzi ya kuondoa wanyanyasaji ambao ni watawala wa kigeni. Sasa "utawala huo haupo tena", bali tunatawala wenyewe. Na utawala wenyewe wa sasa ivi afrika nzimo uko katika context ya UBEPARI, na Afrika nzima inahimiza kipaumbele kwa sekta binafsi kuendesha uchumi, hasa uwekezaji. SWALI LANGU, JE INACHOFANYA CCM NI SAHIHI KWA MANTIKI YA MAPINDUZI? Kwamba inaongoza mapinduzi kwa context iyo, ya kibepari ambapo wachache wanajilimbikizia kwa kuangamia kwa wengi? KAMA NDIYO, BASI WAKO SAHIHI KUCHAKACHUKA NA KULINDA STATUS QUO---in line with development context!????? AU mi ndo skuelmika murua?
 
Leo mchana kuna mdau mmoja wa cuf alimuuliza mwana-ccm kwa nini chama chenu mlikiita chama cha mapinduzi?

Ni mapinduzi gani mnayozungumzia wakati hakukuwa na mapinduzi yoyote kwa sababu kilianzishwa wakati tayari tanganyika na zanzibar zilikuwa huru, tena tanganyika ilipata uhuru wake kwa amani?

Jamaa wa ccm alibaki anajing'ata ng'ata, na yeye akamuuliza mwana-cuf, kwa nini mmekipa chama chenu jina la kiingereza wakati asilimia kubwa ya watanzania hawakijui? Kwanza nitafsirie hiyo "civic united front" kwa kiswahili safi, tuone, jamaa wa cuf nae hakuweza kumjibu.

Mwishoni nikagundua kuwa chadema pekee ndio chama ambacho kipo safi, kuanzia jina lake, sera, mpaka dk wa ukweli.

I am proud being member of chadema.

Peoplezzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz...
 
..wajumbe wa Afro-Shiraz Party waliokuwepo ktk kamati ya kuunganisha vyama[asp & tanu] ndiyo waliolazimisha neno Mapinduzi liwepo ktk jina la chama kipya.

..hivi Afro-Shiraz ilianzishwa tarehe 5 mwezi wa 2 kama CCM? hilo nawaachia great thinkers mfanye uchunguzi wenu.
 
Kwa maoni yangu neno la Mapinduzi kwenye jina la CCM sio kwa ajili ya kupindua nchi au authority fulani kama ilivyo kwenye "coups d'état". Nafikiri wakati kiswahili kilikuwa hakijakua sana lakini walichotaka kumaanisha ilikuwa ni "REVOLUTION" kama kwenye cultural revolution ya wachina au Bolsheviks ya Warusi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom