Supu is overrated

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,572
44,797
Supu ya nyama ina nini cha ziada Mimi naona kama ni maji tu,unakuta mtu anakunywa mapombe too much akiamini supu yenye kakipande kamoja cha nyama inasaidia kutibu madhara ya pombe alizokunywa.

At least Ki dogo iwe supu nzito yenye viazi, karotihohonyama pc 5 ila sio supu hizi za uswahilini za chapati 2 ni michongo tu.
E3C3C68D-0B7C-431D-8C8A-83E3272A0ADA.jpeg
 
Supu ni mlo unaoweza kutumia kwa breakfast ama kama chakula cha jioni haswa kwa watu wanaozingatia uzito na ufanisi wa chakula mwilini.

Supu standard inatakiwa kuwa ni mlo uliokamilika, inaweza kuwa supu ya mbogamboga, sea food, ama nyama za kawaida Ila uwepo wa mbogamboga hâta kama ni supu ya nyama, mifupa kuku au samaki itamuwezesha mlaji kupata starehe ya harufu na ladha, virutubisho vinavyohitajika mwilini pamoja na île hali ya kukinai hivyo huta-crave mavyakula mengine mazito Ili uweze kujaza tumbo kama ambavyo wengi tunaona ni kawaida.


Hizi supu tunazokunywa uswazi maji yanaongezwa Mara tatu tatu kisa tuu tunakamulia ndimu ni mazoea tunayotakiwa kuyaacha kama kweli tunamini katika nafasi ya chakula kwenye ubora wa afya.
 
Yaani mi nikipiga vyombo nikifika home lazima waniandalie mchanganyiko wa parachichi,tango, malimao hata matatu, carrot, hoho na mazagazaga mengine..... Hio ni kama sheria
 
Kwasababu ya uharaka na husasa ndiyo maana siku hizi hakuna supu bali tunakunywa michuzi ya nyama!

Supu sikuzote hutokana na Utumbo wa Ng'ombe au Mbuzi,hiyo ndiyo inaitwa Supu!.

Haya mamichuzi ya ng'ombe na finyango mbili za nyama kwenye bakuli siyo supu hiyo!.

Dar es salaam hakuna supu bali kuna michuzi tu kwenye mabakuli na finyango kadhaa za nyama!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom