kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,318
- 12,622
Kuna Kwaresima na Ramadhan miezi ambayo waumini wa Kikristo na Kiislam wanafunga kama sehemu ya imani zao kwa lengo la kumpendeza Mungu wao ili awasamehe dhambi au awape kibali cha kuingia peponi. Kwenye upande huu wa dini sintakuongelea zaidi kwakuwa imani ya mtu ni package ambayo haiko wazi kujadiliwa wa kukosolewa na mtu mwingine. Hata hivyo ikumbukwe kuwa Ukristo na Uisilam ni dini ambazo chimbuko lao ni Asia ya Kati, watu ambao wana mazingira, tabia, vyakula, utamaduni na bila shaka na magonjwa yanayofanana. Kufunga ilikuwa ni njia yao ya kuzuia (primary prevention) na kutibu (secondary prevention) magonjwa fulani fulani kwenye jamii zao. Njia hii ya kufunga kuacha kula chakula haifanyi kazi ya kukinga na kutibu magonjwa kwa wayahudi na waarabu tu bali hata kwa viumbe vyote vya mwenyezimungu ili vipate maisha marefu na afya tele.
Kufunga kula chakula kunasaidiaje kukinga na kutibu magonjwa kwa binadamu?
1. Kwa kukausha/kuchoma/kutumia mafuta mabaya yaliyozidi mwilini: Miili yetu ina tabia ya kuhifadhi vyakula vya ziada tunavyokula ili mwili wako ivitumie vyakula hivyo siku utakapokosa chakula.
Ugali, ubwabwa, viazi, majimbi, ngano, mihogo, soda, chai na vyakula vyote vya kutia mwili nguvu vinapoliwa kwa wingi kuliko mahitaji ya siku ya mwili huwa ziada inahifadhiwa ndani ya mwili kama sukari (glucose, fructose na galactose) kwa matumizi ya mwili ya sasa hivi na baadae kidogo kama masaa 4 kama utakuwa hujakula chakula kingine, lakini kama baada ya masaa 4 utaendelea kula chakula kingine na kupata glucose mpya mwili utageuza ile glucose/fructose/galactose ya kwanza kuwa glycogen, aina ya sukari ambayo ni ngumu kidogo mwili kuitumia kuliko glucose; glycogen inatakiwa itumike kutia nguvu mwili kama glucose iliyopo imekwisha mwilini. Lakini, Kama mtu ataendelea na kula kula kula chakula kuliko mahitaji ya mwili, mwili wake utaigeuza ile glycogen inayohifadhiwa kuwa mafuta (lipids).
Hivyo mafuta yanayopatikana kwa kula ziada ya Ugali, ubwabwa, viazi, majimbi, ngano, mihogo, soda, artificial juices na vyakula vyote vya kutia mwili nguvu yanaungana mwilini na mafuta mengine unayoongeza kwenye chakula kama vile mafuta ya mbegu za mimea (nazi, kweme, ufuta, alizeti, mahindi, mawese, pamba, korie, nk) pamoja na mafuta uliyokula yenye asili ya wanyama (jibini, siagi, nyama zilizonona, senene, kumbikumbi, nk) kutengeneza tabaka kubwa la mafuta (adipose tissue) mwilini, hivyo kusababisha mwili kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta kuliko mahitaji ya mafuta yanayohitajika kwa kazi za mwili.
Changamoto za kuwa tabaka kubwa la mafuta mwilini:
Mafuta haya mwili unayahifadhi kwenye vioungo na sehemu mbalimbali za mwili kama vile tumbuni (vitambi), matakoni (wowowo), mapajani, shingoni, mikononi, misuli na kwenye ngozi. Kama sehemu zote hizi zikijaa mwili utayatafutia mafuta yako sehemu nyingine za kuyahifadhi kama vile kwenye utumbo, moyo, ndani ya mishipa ya damu, via vya uzazi, mafigo, ini na kila sehemu yenye nafasi, haiyatupi maana mwili hautupi chakula.
Kusudi kubwa la mwili wako kugeuza chakula chako cha ziada ulichokula kuwa mafuta na kuyahifadhi ni ili mwili wako uweze kuyatumia mafuta hayo kutoa nishati ya kusukuma mwili KAMA mwili wako utakosa chakula kwa muda mrefu (starvation), hivyo mtu mwenye mafuta mengi mwilini anaweza kuishi hata siku 30 bila kula chakula bila kufa. Katika kipindi hicho mwili utayaunguza/unayafagia/unayapakua/unayatumia mafuta yote ili kupata chakula.
Hivyo, changamoto za kutunza mafuta hayo mwilini ni mapoja na:
1. Kuongezeka uzito kuliko uwezo wa misuli yako (mifupa, tendons, muscles) inavyoweza kubeba.
2. Kuminya mishipa ya damu na fahamu, hii inasababisha presha na ganzi kwenye mikuu, mikono au kwenye makalio.
3. Kupunguza kiwango cha maji mwilini, Mtu mwenye mafuta mengi (mnene) ana kiwango kidogo cha maji.
4. Kupunguza tundu (lumen) la mishipa ya damu na kusababisha kupata ugonjwa wa pressha (high blood pressure, kiharusi)
5. Kupunguza kiwango cha dawa kutibu magonjwa (lazima dose yako iwe kubwa kuliko kawaida)
6. Kupunguza uwezo wa kongosho (pancrease) kutoa insulin na insulin kushindwa kuchakata chakula unachokula na kusababisha kupata ugonjwa wa Kisukari (diabetes)
7. Kupunguza nguvu za kiume
8. Kupumua kwa shida na kukoroma sana usingizini
9. Kupata ugumba na utasa
10. Kutembea kwa shida na miguu kupata maumivu
11. Kinga ya mwili kushuka
12. Kuongeza uwezekano wa kupata kansa (cancer) ya matiti, utumbo, ngozi, mfumo wa uzazi na viungo vingine.
13. Siku mafuta yaliyoko ndani ya mishipa ya damu yakimeguka na kuzunguuka pamoja na damu ndani ya mishipa yanaweza kwenda kuziba mishipa midogo midogo mwilini na kusababisha kiharusi au moyo kusimama kutegemea bonge la mafuta limeenda kukwamia wapi na kwenye kiungo gani.
Faida za kufanga ni zipi?
Kufunga kula chakula ni muhimu sana kwa kila mtu, sio kwaajili ya kwenda mbinguni tu, lakini kwa
1. kuzuia na kuponya magonjwa yote hayo niliyoyasema hapo juu kwa mwili kuyafagia mafuta mwilini kwa kiasi kikubwa.
2. Ini, tumbo, utumbo, kongosho na nyongo (bile) ndivyo vinavyofanya kazi kubwa ya kuchakata chakula na mafuta, hivyo kufunga kula chakula kutasaidia viungo hivyo kurudisha afya yake (kupunzika na kupona majeraha na uchovu)
3. Mafuta yakipungua magonjwa yote hayo yatapotea ghafla bin vuu.
4. Kufunga kunaongeza uwezo wako wa kufikiri, kutafakari na kuzingatia (focus). Hii inasaidia kwenye kutatua shida na migogoro na mahusiano yako na watu wengine kwa kumaanisha.
Hivyo kufunga sio tu ni ibada lakini ni tiba kamili kwa viumbe, usisubiri mpaka Ramadhan na Kwaresma ndipo ufunge, unakosa mengi sana,
Namna ya kufunga:
Hakikisha kuwa unafunga kula chakula na vinywaji vyenye sukari, sio kama wengine wanavyosema kuwa wamefunga kusema uongo, sijui kuseng'enya na nini, Kufunga ni kuacha kula chakula kwa masaa 12. Unaweza kunywa maji tu kwa wanaofunga kwajili ya afya ya magonjwa haya.
1.Wakati wa kufungua jioni hakikisha kuwa huli vyakula viiiingi na vyenye mafuta mengi kama wengine wanavyofanya wakati wa kufungua. Kunywa maji mengi na matunda zaidi ukishafungua jioni na baada ya nusu saa ndio ule vyakula vingine vya kawaida.
2. Usile daku alfajiri ili kupunguza ukali wa njaa, hapo utakuwa umejidanganya mwenyewe, kula kama kawaida yako.
3. Anza kufungua kwa kula vitu vyepesi kama maji, matunda, juice isiyokuwa na sukari, au uji usiokuwa na sukari. Epuka soda na vitu vitamu sana kama halua.
4. Usichanganye nyama na carbohydrates kwenye mlo mmoja, usichanganye matunda na chakula pamoja, usichanganye maziwa na chakula kwenye mlo.
5. Fanya mazoezi, fanya kazi, usilale wakati umefunga ili kupata ubora wa kufunga.
6. Wakati umefunga jaribu tena kuTatua migogoro iliyokushinda huko nyuma utaona maajabu makubwa.
Hawa Wayahudi na Waarabu nina uhakika elimu hii ya kufunga kwa afya walikuwa nayo tangu siku nyingi ndio maana ukawa utamadini wao ukaingizwa kwenye dini, tuwapigie makofi mengi.
Kama una swali niulize, nimejikita kwenye sayansi za afya sio kwenye dini ya huyu wala yule, samahani, msinipige mawe.