Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,322
- 219,639
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mbunge ajaye wa Mbeya Mjini , Bilionea Joseph Mbilinyi, amemuonya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Bwana Benno Mallissa kuacha kuhujumu Chadema , na kwamba akiendelea na jambo hilo Watu wa Mbeya watampiga Marufuku kuhudhuria Club za Starehe za Mji huo ( Inadaiwa Mallisa ni Mpenda Bata )
Taarifa zinaeleza kwamba Mallisa alijaribu kuhujumu Maandamano ya Chadema kwa kukusanya Madereva wote wa Bajaji Mbeya Mjini na kuwahonga pesa ili wasihudhurie Maandamano ya Chadema , Hata hivyo amechemsha .
labda Kwa wasiomjua Benno Mallisa ni hivi, Huyu alifukuzwa UVCCM haraka sana , katika ile kampeni ya wanaccm ya kuzuia kiongozi kuwa na Kofia Mbili, Kampeni iliyolenga kumvua Uenyekiti wa ccm Kikwete ili abaki na Urais pekee na kumvunja nguvu kwenye vikao vya chama, kampeni hiyo ikidaiwa kuendeshwa na Team Lowassa , huku Mallisa akiwa kwenye timu hiyo , akapigwa chini na kupotezwa kabisa kwa miaka mingi , hata huu UDC aliopewa ulichagizwa na ushawishi wa Lowassa baada ya Kikwete kuondoka Madarakani .