Sugu akamate CDM Mbeya

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Baada ya Shitambala kujitosa mwenyewe baharini, ninaanza rasmi kumpigia chapuo JM (Sugu) ashike hatamu za CHADEMA mkoani Mbeya. Ni wakati wa vijana sasa, na anaweza.
 
Yes; Agree ila vema tujue watu wanaoweza kazi; kuwa mbunge sio lazima uwe mwenyekiti wa mkoa wa chama
 
Sijatumia ubunge kama kigezo cha kumpigia debe. Hata kama asingekuwa MP angeweza ku-mobilise vijana, na ndio wanaohitajika kujenga chama chenu.
 
Kuna watu wengi sana wanaoweza kuongoza chama mbeya,sugu hawezi sioni kigezo hata kimoja cha yeye kuweza kuongoza chama
 
Baada ya Shitambala kujitosa mwenyewe baharini, ninaanza rasmi kumpigia chapuo JM (Sugu) ashike hatamu za CHADEMA mkoani Mbeya. Ni wakati wa vijana sasa, na anaweza.
inaonekana hauishi mbeya na wala c mwanachama wa Cdm,CDM MBY tuna hazina kubwa ya viongozi,mwache Sugu aendelee na ubunge,wapo wengine watakaosukuma gurudum
 
Wazo la mtoa mada sio baya,lakini ingekuwa vema zaidi Mbunge wetu Sugu akajikita zaidi kwenye kushughulikia kero za wananchi ili tuendelee kushikilia jimbo hilo.Mimi kama mwanachama wa CDM,na mwana Mbeya pindi uchaguzi utakapotangazwa nitakuwa miongoni mwa watakaochukua fomu ya kugombea.Ukiondoa Mbeya mjini na Mji wa Mji wa Mbalizi na Tunduma,chama bado hakijakita mizizi mkoani Mbeya,mf sehemu za Tukuyu,Chunya,Mbarali n.k.Tunahitaji nguvu mpya na kukijenga chama kwa wananchi kuliko kumjenga mtu mmoja mmoja.Naomba kuwasilisha.
 
Jitambulishe rasmi tuanze kukupigia debe.
 
Back
Top Bottom