Suala ya Pensheni laibuka Bungeni, Lissu na Zitto watoa hoja, Mhagama ataka lijadiliwe kikamati

Hii sheria kipengere kimechomekwa

Ndiyo maana mimi napenda Dr.slaa awe the next president kwani ni yeye tu ndiyo makini anayeweza kufanya tracing on issues za kibunge.Mtakumbuka mwaka 2009 sheria aliyyosaini JK kwa mbwembwe lakini siku hiyo hiyo dr slaa alifanya reference kweny original bill iliyopelekwa bungeni na kugundua kipengere kilichomekwa.ZITTO UPO??????? wewe drslaa siyo saizi yako yule mzee ni planet nyingine kama MESSI wa Algentina.

Ninachoweza kusema ni kwamba HATUNA WABUNGE MAKINI baada ya DR.SLAA kuondoka bungeni.Hata wale wanaotaka kugombea urais ni wala posho tu. Mtu kuitwa makini lazima uonekane kweli wewe makini.Mimi namwamini Dr.slaa ndiyo pekee anayeweza kutuvusha salama.wengine porojo tu
 
wameona hali tete hawana njia nyingine at last itabidi waibadilishe tu. madhara ya kulala wakistuka ndioooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo. shame shame shame.
 
Mkuu asante kwa ufafanuzi, lakini kama hapo saa saba Bunge itaagiza kama ulivyosema tayari haitakuwa kama nilivyosema hapo juu kuwa iwapo itabaki kama walivyoamua hapo awali. Lakini bunge likiona ni sawa mswada uliopitishwa awali uendelee kama sheria halali ndiyo nilichopendekeza hapo juu tukishikie bango!.

kyaiyembe nadhani upepo wameuona wananchi hususani wafanyakazi wamechachamaa watataka kuicheza hii karata vizuri! Si wanajiita wasikivu watu wanataka kuona huo usikivu!
 
Kwa Bunge lilivyosasa si sheria zote zinazopitishwa Bungeni wabunge walikubaliana nazo bali wanatimiza wanachotaka watawala. Kwa hii sheria ya mifuko ya jamii tutahitaji HANSARD ili kila mwanajimbo ajiu mbunge wake alichangia nini. Mlioko mjengoni tunaomba HANSARD za mjadala wa sheria ya mifuko ya jamii
 
Mh. Lugola leo amewasuta na kuwaonyesha wabunge kuwa ni wanafiki kwa kitendo chao cha kupitisha sheria ya mpya ya mifuko ya jamii na leo kuonekana kuunga mkono hoja ya mh. Lusinde alietaka bunge lijadili kwa dharura kanuni hiyo ili ibadilishwe.

Baada ya mh. Lusinde kutoa hoja hiyo wabunge wengi waliiunga mkono kanakwamba sio wao waliipitisha sheria hiyo inayozuia mafao ya kujitoa mpaka mtu afikishe angalau miaka 55. Kweli hatuna bunge makini ila tuna bunge la ndio hata kwa mambo ambayo ni wazi si ya kupitisha kabisa.

Hivi sheria hii inatofauti gani na zile za kikoloni? Hivi kweli hawa ni wabunge kwa ajili ya kutete mwananchi au ni wabunge kwa ajili ya kutetea serikali? Hili bunge bora livunjwe kwani ni mzigo na ni janga la kitaifa.

Mh. Lugola aliomba muongozo na alipopewa nafasi aliwasuta wabunge na kusema bunge haliko makini. Mimi naungana na huyu mh. kwani ni wabunge hawahawa ndio walipitisha sheria hii mwezi Aprill mwaka huu ila baada ya kuona umma umekuja juu sasa wanajidai kutetea wananchi.

Mtu mnafiki ni hatari kuliko hata ukoma.

salary slip jina lako laonesha nawe ni mmoja wa wahanga wa hii sheria. Nilitaka nikukumbushe kuwa hoja hii ilitolewa na Mbunge wa kisarawe Mh Seleman Jaffo sio Mh Lusinde.
 
Hii sheria kipengere kimechomekwa

Ndiyo maana mimi napenda Dr.slaa awe the next president kwani ni yeye tu ndiyo makini anayeweza kufanya tracing on issues za kibunge.Mtakumbuka mwaka 2009 sheria aliyyosaini JK kwa mbwembwe lakini siku hiyo hiyo dr slaa alifanya reference kweny original bill iliyopelekwa bungeni na kugundua kipengere kilichomekwa.ZITTO UPO??????? wewe drslaa siyo saizi yako yule mzee ni planet nyingine kama MESSI wa Algentina.

Ninachoweza kusema ni kwamba HATUNA WABUNGE MAKINI baada ya DR.SLAA kuondoka bungeni.Hata wale wanaotaka kugombea urais ni wala posho tu. Mtu kuitwa makini lazima uonekane kweli wewe makini.Mimi namwamini Dr.slaa ndiyo pekee anayeweza kutuvusha salama.wengine porojo tu
Ndiyo maana wanatumia hela nyingi za kodi yako kupanga kumuondoa duniani kabla ya 2015.
 
Amini usiamini hiki kipengere kimemekwa baada ya sheria kupita mimi nilifuatilia kusikiliza bunge hii hoja ilipopelekwa bungeni april 2012 hakikuwepo wala wabunge hawakujadili.Kinachogomba hapa hawa wabunge wetu hajajua wajibu wao.Wanatakiwa kufuatilia kila sheria zinaposainiwa na mkulu kuona kama inafanana na ya mwanzo.Inabidi wabunge wafuatilie ili kama ikionekana kilichopmekwa wai-task serikali kwa forgery
 
Hivi hawa wabunge wa ccm wanapopitisha miswaada ya kifisadi kama hii, wanakuwa wanafikiria nini? lakini pia Hawa wafanyakazi ni vipi wanaendelea kuikumbatia ccm na JK alisema hata wasipo mpa kura zao hajali, Hivi bado ccm itakuwa na mshabiki na mwanachama mfanyakazi?
 
Ndiyoooooo! Haya sasa ndugu zako wasubiri wafikishe miaka55/60. Wewe mbunge NDIYO Unalipwa, una mafao kibao utawasaidia ndugu jamaa na marafiki mpaka 55itimie au ndiyo utakuja na hoja ya posho haitoshi iongezwe kwa sababu wewe NDIYOOO ndiye uliyepitisha sheria hii ya mafao ktk mifuko ya jamii iwe mpaka ufikishe 55yrs
 
salary slip jina lako laonesha nawe ni mmoja wa wahanga wa hii sheria. Nilitaka nikukumbushe kuwa hoja hii ilitolewa na Mbunge wa kisarawe Mh Seleman Jaffo sio Mh Lusinde.

Mkuu Wabunge wote wa CCM hawatofautiani wote kama Lusinde tuu Salary Slip hajakosea
 
CCM ni matapeli, inawezekana mswaada uliokuwa umepelekwa Bungeni ni mwingine na alio saini rais na kuwa sheria ni kitu kingine, Haiwezekani mswaada kama ule upite ukiidhinisha dhuluma kwa wafanyakazi wake
Kwa Bunge lilivyosasa si sheria zote zinazopitishwa Bungeni wabunge walikubaliana nazo bali wanatimiza wanachotaka watawala. Kwa hii sheria ya mifuko ya jamii tutahitaji HANSARD ili kila mwanajimbo ajiu mbunge wake alichangia nini. Mlioko mjengoni tunaomba HANSARD za mjadala wa sheria ya mifuko ya jamii
 
Wengi wanashangaa ilikuwae wabunge wa so called upinzani hawakuliona hili kabisa!!!!! Ukweli ni kuwa, Serikali inawajua vizuri hawawabunge na inaelewa jinsi ya kuwa tune, waliporushiwa fupa la tume ya katiba wakasahau kila linaloletwa bungeni.
 
CCM ni matapeli, inawezekana mswaada uliokuwa umepelekwa Bungeni ni mwingine na alio saini rais na kuwa sheria ni kitu kingine, Haiwezekani mswaada kama ule upite ukiidhinisha dhuluma kwa wafanyakazi wake

Kuna fupa la tume ya katiba walirushiwa wabunge, ndio huu muswada ukajadiliwa pia.
 
Ndiyo maana umakini unahitajika.Mimi bado nauliza yule mbunge anayetaka kuwa rais wetu 2015 alikuwepo??? wakati wa mjadala, ila huyu asingepinga maana ni mshikaji na CEO wa NSSF.Ndiyo maana nasema ONLY FOR dr.SLAAAAAAAAAAAAAAA
 
This is ridiculous! Vijana wa sasa tunaishi leo siyo kesho. Wengi hutuna mpango wa kufanya kazi za kuajiriwa hadi kustaafu bali tunatafuta mitaji tujiajiri. Hivi serikali inapopiga kelele watu wajiajiri bila kuwapa mitaji wanategemea nini?Sisi wengine tunategemea michango yetu iwe mitaji mambo ya kufikisha miaka 60 ni mawazo mufilisi kabisa na haikubaliki! Kama serikali inajali wastaafu ingeonesha mfano kwa wazee wa Africa masharika wanaopuliziwa maji ya kuwasha kila siku. Kwa hili serikali ya CCM iwe makini kama inataka kuendelea kututawala. Hivi inawezekana kukopeshwa nyumba ya m.60 au 80 wakati umechangia m. 10 au 15 tu? Kwa wale wanaocha kazi na kujiunga na mashirika ya kimataifa yenye mifumo yao ya pension kama UN, AfDB,WB na mengineyo na wale wanakwenda kufanya kazi nje ya nchi inakuwaje? Hii SSRA naona inajitahidi kuiondoa CCM madarakani!!! Kwa hili wafanyakazi tupo pamoja!!!!!
Hiki ni kipimo kwa wabunge wote!Ngoja tuone hiyo saa saba yatajiri mambo gani.
 
Kwa Bunge lilivyosasa si sheria zote zinazopitishwa Bungeni wabunge walikubaliana nazo bali wanatimiza wanachotaka watawala. Kwa hii sheria ya mifuko ya jamii tutahitaji HANSARD ili kila mwanajimbo ajiu mbunge wake alichangia nini. Mlioko mjengoni tunaomba HANSARD za mjadala wa sheria ya mifuko ya jamii
Ipo humuhumu. Tafuta thread inayosomeka: "Kilichojili bungeni april 13, 2012".
 
Amini usiamini hiki kipengere kimemekwa baada ya sheria kupita mimi nilifuatilia kusikiliza bunge hii hoja ilipopelekwa bungeni april 2012 hakikuwepo wala wabunge hawakujadili.Kinachogomba hapa hawa wabunge wetu hajajua wajibu wao.Wanatakiwa kufuatilia kila sheria zinaposainiwa na mkulu kuona kama inafanana na ya mwanzo.Inabidi wabunge wafuatilie ili kama ikionekana kilichopmekwa wai-task serikali kwa forgery

Hivi baada ya kujadili si walitakiwa kupitia kopi ambayo imekuwa Approved kuona kama walilichokijadili ndicho???
wasilete usingizi hapa..
 
Kuitwa mtunga sheria lazima uonekane kuwa ni kweli mtunga sheria.Sheria za kutungwa na kina lusinde na Komba na KINA MWIGULLU matokeo ndiyo hayo.Watu wakome kukimbilia ubunge.Wabunge wetu hawasomi vipiengere wanapitisha kwa wingi wao na si kwa hoja.Matokeo ya sheria ni kwamba hata wao wabunge sheria hii itawakumba kama walimekuwa wakichangia wamejikuta wamepitisha sheria ya kuwamaliza wao wenyewe.

Ndiyo maana kila siku tunasema ccm wanendelea kupitisha sheria gandamizi wakijifanya sheria zile hazitawadhuru wao.Hii ni hatari sana
 
Back
Top Bottom