dosama
JF-Expert Member
- Dec 25, 2010
- 912
- 957
Lapigwa dana dana na mwenyekiti wa Bunge hadi saa saba mchana wakutane kikamati na watoa hoja waje na data za kueleweka juu ya kipi wananchi wanakilalamikia.
Wabunge wa CCM wamzomea Lissu kwa hoja ilipitishwa tayari na bunge
Wabunge wa CCM wamzomea Lissu kwa hoja ilipitishwa tayari na bunge
Mh. Lugola leo amewasuta na kuwaonyesha wabunge kuwa ni wanafiki kwa kitendo chao cha kupitisha sheria ya mpya ya mifuko ya jamii na leo kuonekana kuunga mkono hoja ya Lusinge alietaka bunge lijadili kwa dharura kanuni hiyo ili ibadilishwe.
Baada ya mh. Lusinde kutoa hoja hiyo wabunge wengi waliiunga mkono kanakwamba sio wao waliipitisha sheria hiyo inayozuia mafao ya kujitoa mpaka mtu afikishe angalau miaka 55. Kweli hatuna bunge makini ila tuna bunge la ndio hata kwa mambo ambayo ni wazi si ya kupitisha kabisa.
Hivi sheria hii inatofauti gani na zile za kikoloni? Hivi kweli hawa ni wabunge kwa ajili ya kutete mwananchi au ni wabunge kwa ajili ya kutetea serikali? Hili bunge bora livunjwe kwani ni mzigo na ni janga la kitaifa.
Mh. Lugola aliomba muongozo na alipopewa nafasi aliwasuta wabunge na kusema bunge haliko makini. Mimi naungana na huyu mh. kwani ni wabunge hawahawa ndio walipitisha sheria mwezi Aprill mwaka huu ila baada ya kuona umma umekuja juu sasa wanajidai kutetea wananchi.
Mtu mnafiki ni hatari kuliko hata ukoma.